Blog - Page 3 of 20 - Fahamu Hili
Thursday, April 25Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Blog

Athari au Madhara 10 ya Intaneti Unayopaswa Kuyafahamu

Athari au Madhara 10 ya Intaneti Unayopaswa Kuyafahamu

Teknolojia
Katika dunia hii ya leo ni vigumu kuishi bila kutumia intaneti kwa namna moja au nyingine. Watu hutumia intaneti kuwasiliana, kupata taarifa na habari au hata  kujipatia kipato. Kuwepo kwa intaneti kumerahisisha maisha ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa na kufanya utendaji kazi wake uwe bora zaidi. Pamoja na intaneti kuwa na manufaa kadha wa kadha, intaneti ina athari mbalimbali. Hivyo basi fahamu madhara 10 ya intaneti. 1. Taarifa za uongo Kila mtu anaweza kuweka taarifa kwenye mtandao wa intaneti, hivyo ni rahisi kukumbana na taarifa zisizo za kweli. Swala hili limepelekea baadhi ya nchi na mashirika mbalimbali kujaribu kukabili taarifa mbalimbali zinazopatikana kwenye mtandao ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na taarifa hizo. Ni vyema kuhakikisha tovuti au blog ...
Mambo 10 ya Kuzingatia Unapochagua Anwani ya Mtandao (Domain)

Mambo 10 ya Kuzingatia Unapochagua Anwani ya Mtandao (Domain)

Tovuti na Blogu
Anwani mtandao ni muhimu sana kwa ajili ya utambulisho wa tovuti au blog ya kile unachokifanya. Inawezekana unamajina mengi ambayo unataka uyatumie kama anwani ya mtandao ya tovuti au blog yako; lakini ni muhimu kufahamu kuwa ukifanya makosa kwenye kuchagua anwani ya mtandao utaathirika kwa kiasi kikubwa. Madhara ya kukosea kuchagua anwani ya mtandao (domain) Kutokutambulisha vyema kile unachokifanya Kukosa nafasi kwenye injini pekuzi Kupoteza wasomaji au watembleaji Kuingia kwenye migogoro ya kisheria ikiwa utatumia anzwani inayofanana na za wengine. Ikiwa unataka kufungua website au blog kwa ajili yako binafsi au bishara yako, basi fahamu mambo 10 ya kuzingatia unapochagua anwani ya mtandao (domain). 1. Upekee Hakikisha unapochagua domain ni ya kipekee sana na i...
Maneno 20 Ambayo Hutakiwi Kumwambia Mtoto Wako

Maneno 20 Ambayo Hutakiwi Kumwambia Mtoto Wako

Mahusiano na Familia
Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto wao maneno mbalimbali wakati wakiwa na furaha au hasira. Ipo nguvu kubwa kwenye maneno ya kutamkiwa ambayo wazazi wengi hawaifahamu. Kwa hakika maneno yanaweza kujenga au kubomoa maisha ya mtoto kwa kiasi kikubwa. Hivyo fahamu maneno 20 ambayo hutakiwi kumwambia mtoto wako. 1. Wewe ni mtoto mbaya Wazazi wengi wanapokasirishwa na mtoto humwambia wewe ni mtoto mbaya, hili humfanya mtoto ajione hafai. Hivyo ni vyema kuepuka kumwambia mtoto neno hili badala yake mweleze kosa lake na athari zake ili aliepuke. 2. Kwanini usiwe kama dada au kaka yako? Kauli hii humfanya mtoto ajione dhaifu kwa sababu unamlinganisha na wengine. Kauli hii pia humjengea chuki na wivu kwa wale unaowataja kwake kuwa ni bora. Hili husababisha watoto kuchukian...
Sababu 7 za Kwa nini Hutakiwi Kucheza Michezo ya Kubahatisha

Sababu 7 za Kwa nini Hutakiwi Kucheza Michezo ya Kubahatisha

Kipato
Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi au changamoto za maisha watu wengi hutekwa na mambo mbalimbali hasa yale yanayohusu kupata pesa za haraka. Nilipofanya utafiti mdogo nilibaini kuwa “njia za kupata pesa kwa haraka” pamoja na “njia za kupata utajiri kwa haraka” ni moja kati ya vitu vinavyotafutwa sana na watu kwenye mtandao. Hii inadhihirisha uhitaji mkubwa wa watu kutaka kupata pesa, tena kwa muda mfupi. Hivyo basi, hili limepelekea watu wengi kutekwa na michezo ya bahati nasibu wakifikiri kuwa inaweza kuwatoa katika matatizo au mahitaji yao ya kifedha. Haijalishi unacheza au huchezi michezo ya kubahatisha, karibu nikufahamishe sababu 7 za kwanini hutakiwi kucheza michezo ya kubahatisha. 1. Ni biashara Hakuna mtu atakayetoka China, India au Marekani ili aje Afrika kukugawia...
Madhara 8 ya Kusikiliza au Kutazama Mziki

Madhara 8 ya Kusikiliza au Kutazama Mziki

Mtindo wa Maisha
Kwa hakika kila jambo lenye uzuri au faida lina hasara zake. Nafahamu umekuwa ukisikia faida kede kede za kusikiliza mziki, lakini haujasikia kuwa kwa upande mwingine mziki unaweza kuwa na madhara kwako. Ikiwa wewe ni mpenzi wa muziki, ni vyema ukafahamu madhara ya kusikiliza au kutazama mziki ili uutawale mziki usikuathiri. 1. Huathiri afya ya masikio Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kumeibuka vifaa mbalimbali katika swala la utengenezaji, usambazaji na hata usikilizaji wa mziki. Kutokea kwa teknolojia ya vifaa vya kusikilizia mziki vijulikanavyo kama headphones au earphones kumesababisha watu wengi hasa vijana kusikiliza mziki karibu kila mahali na kila wakati. Taarifa mbalimbali za kitabibu zinaeleza kuwa vifaa hivi vimechangia sana kuharibu masikio au mfum...
Sababu 10 za Kwa Nini Baadhi ya Watu Wanafahamu Mambo Mengi

Sababu 10 za Kwa Nini Baadhi ya Watu Wanafahamu Mambo Mengi

Maendeleo Binafsi
Kwa hakika kuna watu ukiwatazama au kuwasikiliza unaweza kufikiri wana akili ya ziada. Maamuzi na ujenzi wao wa hoja ni wa hali ya juu sana. Watu hawa wanajua mambo kwa undani na kwa usahihi. Ukiwauliza hiki au kile watakujibu bila wasiwasi tena hata na ziada yake. Naamini sote tunatamani kuwa kama watu hawa. Je ni sababu gani zinawafanya watu hawa kufahamu mambo mengi? Karibu nikushirikishe sababu 10 zinazowafanya baadhi ya watu kufahamu mambo mengi zaidi kuliko wengine. 1. Wanasoma sana Kusoma ni chanzo kimoja kikuu cha maarifa. Watu wanaojua mambo mengi husoma vitabu na makala nyingi kadri wawezavyo. Hawasomi tu vitabu au makala, bali wanasoma vile ambavyo vina ubora na maarifa stahiki. Kwa njia hii wanafahamu mambo mengi na kuwafanya kutoa hoja zenye ushahidi na ufaf...
Mambo ya Kuzingatia Ili Kuchagua Kichwa Kizuri cha Kitabu

Mambo ya Kuzingatia Ili Kuchagua Kichwa Kizuri cha Kitabu

Tija
Swala la uandishi wa vitabu ni swala linalohitaji kuzingatia hatua kadhaa muhimu. Moja kati ya hatua hizi ni uchaguzi wa wazo au kichwa cha kitabu. Haijalishi ni kitabu cha kifasihi au kisicho cha kifasihi, utahitajika kuchagua kichwa kizuri au bora cha kitabu chako. Ikiwa wewe ni mwandishi au unajiandaa kuwa mwandishi wa vitabu, basi fahamu mambo ya kuzingatia ili kuchagua kichwa kizuri cha kitabu. 1. Fanya utafiti Utafiti ni msingi mkuu wa kupata kichwa kizuri cha kitabu. Ni muhimu kufanya utafiti katika vitabu au makala nyingine mbalimbali zinazohusiana na kile unachotaka kukiandikia. Unaweza kuzingatia haya wakati wa utafiti: Fanya utafiti kwenye vitabu vilivyochapishwa pamoja na vile vilivyoko kwenye mtandao wa intaneti ili kubaini kama kichwa unachokitaka kimeshatumi...
Mambo 7 ya Kuzingatia ili Kulinda Tovuti Yako Dhidi ya Wadukuzi

Mambo 7 ya Kuzingatia ili Kulinda Tovuti Yako Dhidi ya Wadukuzi

Tovuti na Blogu
Kutengeneza tovuti ni jambo moja na kuilinda ni jambo la pili. Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia, kumepelekea kukua na kushamiri kwa uhalifu kwa njia ya mtandao. Visa kadha wa kadha vimeripotiwa vikieleza juu ya udukuzi uliofanyika kwenye makampuni mbalimbali na kusababisha hasara kubwa. Kwa mfano kampuni ya Sony ilidukuliwa mnamo mwaka 2014 na kupata hasara ya takriban dola milioni 15 za Marekani. Ni muhimu kulinda tovuti au blog yako dhidi ya wadukuzi ili kuepusha hasara na uharibifu unaoweza kutokea. Ikiwa unataka kulinda tovuti yako, basi fahamu mambo 7 ya kufanya ili kulinda tovuti yako dhidi ya wadukuzi. 1. Hakikisha unazingatia usasishaji (updating) Ikiwa unatumia programu yoyote katika website yako, hakikisha unaisasisha kwa wakati. Programu kama vile Wordp...
Mambo 7 ya Kuzingatia Unapoendesha Gari Wakati wa Mvua au Ukungu

Mambo 7 ya Kuzingatia Unapoendesha Gari Wakati wa Mvua au Ukungu

Usafiri na Safari
Kama ambavyo nimekuwa nikieleza kwenye makala nyingine kuwa gari ni chombo kinachorahisisha usafiri lakini kinatakiwa kutumiwa kwa umakini na tahadhari kubwa. Umakini na tahadhari zaidi vinahitajika ikiwa utaamua kuendesha gari wakati hali ya hewa ikiwa siyo nzuri, yaani kuna maswala kama vile mvua au ukungu. Taarifa mbalimbali za usalama barabarani zinaeleza kuwa zipo ajali nyingi zinazogharimu maisha na mali za watu ambazo husababishwa na mvua au ukungu. Hivyo ikiwa unataka kuongeza maarifa pamoja na kulinda usalama wako, basi fahamu mambo ya kuzingatia unapoendesha gari wakati wa mvua  au ukungu. 1. Punguza mwendo Mwendo mkubwa ni hatari sana, lakini ni hatari zaidi mara hali ya hewa inapokuwa mbaya. Kumbuka kuwa wakati wa mvua au ukungu barabara huteleza na ni vigumu...
Mambo Yanayosababisha Baadhi ya Watoto Wasifanye Vizuri Kwenye Masomo

Mambo Yanayosababisha Baadhi ya Watoto Wasifanye Vizuri Kwenye Masomo

Mahusiano na Familia
Mara kadhaa imeshuhudiwa baadhi ya watoto wakishindwa kufanya vizuri kwenye masomo. Jambo hili siyo zuri kwani linaathiri maisha ya watoto wenyewe pamoja na wazazi au walezi. Wakati mwingine swala hili limekuwa kubwa kiasi cha kuwafanya baadhi ya watoto kupata shida hata kufanya mambo madogo kama vile kusoma na kuandika. Hata hivyo kila jambo linalotokea duniani hutokea kwa sababu. Hivyo ukiwa wewe umeguswa na swala la baadhi ya watoto kutokufanya vizuri shuleni, basi karibu nikushirikishe mambo yanayosababisha baadhi ya watoto wasifanye vizuri kwenye masomo. 1. Matatizo ya kisaikolojia Watoto wanaweza kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisaikolojia ambayo huathiri uwezo wao wa kujifunza shuleni. Baadhi ya watoto huzaliwa na matatizo haya huku mengine hutokana na matendo k...