Teknolojia Archives - Page 2 of 2 - Fahamu Hili
Saturday, July 2Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Teknolojia

Vitu 11 Unavyotakiwa Kutoviweka Kwenye Mitandao ya Kijamii

Vitu 11 Unavyotakiwa Kutoviweka Kwenye Mitandao ya Kijamii

Teknolojia
Kuna taarifa nyingi tunazoweka kwenye mtandao; lakini je, sasa ni wakati wa kuweka mipaka juu ya ni lipi la kuweka na kutoweka kwenye mitandao? Ndiyo; huu ni wakati sahihi. Hivyo basi, tambua vitu 11 ambavyo haupaswi kuviweka kwenye mitandao ya kijamii. 1. Tarehe kamili ya kuzaliwa Wakati mwingine unaweza kuvutiwa na namna marafiki zako wanavyoweka taarifa za kuzaliwa kwenye mtandao, au hata misisitizo ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook juu ya kukamilisha akaunti yako kwa kuweka tarehe ya kuzaliwa. Kuweka tarehe halisi au kamili ya kuzaliwa kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kutoa mwanya kwa wahalifu kupata taarifa zako muhimu na hata kufungua au kuingilia akaunti zako zinazotumia tarehe yako ya kuzaliwa. Mambo ya kufanya: Ficha au ondoa tarehe yako halisi ya kuzal...
Hatimaye Ghana Yarusha Satelaiti Yake ya Kwanza Kwenda Anga za Juu

Hatimaye Ghana Yarusha Satelaiti Yake ya Kwanza Kwenda Anga za Juu

Habari, Teknolojia
Satelaiti ijulikanayo kama GhanaSat-1, ambayo iliundwa na wanafunzi kutoka katika Chuo Kikuu cha All Nations cha Koforidua, ilirushwa kwenda kwenye mzingo wa dunia kutoka kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu. Shange na vifijo vya watu takriban 400 wakiwemo wanafunzi na waandisi walikokuwa wakishuhudia tukio hili zilisikika katika mji wa kusini mwa Ghana. Mji huo ndipo lilipofanyika zoezi hilo la urushaji wa satelaiti hiyo. Mawasiliano na chombo hicho yalianza kupokelewa muda mfupi baada ya chombo hicho kurushwa. Maradi huo uligharimu dola za kimarekani 50,000 ulifadhiliwa na shirika la Japan Aerospace Exploration Agency (JAXA). Satelaiti hiyo itatumika katika mambo mabalimbali kama vile kufwatilia ukanda wa pwani wa Ghana, kuchora ramani na kuijengea nchi hiyo uwezo kati...
China Kujenga “Mji Msitu” Ambao Utakuwa na Mamilioni ya Mimea na Miti 40,000

China Kujenga “Mji Msitu” Ambao Utakuwa na Mamilioni ya Mimea na Miti 40,000

Teknolojia
China kujenga “mji msitu” ambao utakuwa na mamilioni ya mimea na miti 40,000. Kazi hii inatarajiwa kutekelezwa kwenye Mji Msitu wa Liuzhou ulioko katika milima ya kusini mwa Guangxi kabla ya 2020. Mji huu uliobuniwa na msanifu majengo Stefano Boeri unatekelezwa sasa, ambapo nyumba, ofisi, shule na hosipitali zitafunikwa kabisa na miti na mimea mingine. Mjii huu unatarajiwa kuchukua eneo la hekta 175, na utakapokamilika utaweza kuchukua watu takriban 30,000. Mji huo utakapokamilika utatumia usafiri wa treni ya umeme kutoka Liuzhou. Mji huo pia utatumia nishaji ya joto ardhi (geothemal) kwa matumizi ya ndani nyumba pamoja na umeme jua (solar). Wanaamini kuwa kupanda miti zaidi kutanyonya tani 10,000 za hewa ukaa (C02) na tani 75 za hewa chafuzi nyingine, wakati huo ikizalisha ta...
Kilimo cha Kisasa: Kilimo bila Jua, Udongo wala Maji Mengi

Kilimo cha Kisasa: Kilimo bila Jua, Udongo wala Maji Mengi

Teknolojia
Kwa kawaida kilimo kinahitaji maji, urdhi ya kutosha, jua n.k. Lakini hali ni tofauti kwa kampuni ya AeroFarms ambayo imekuja na mawazo tofauti ya kulima mazao mbalimbali bila kutumia udongo, jua wala maji mengi. Kilimo chao hufanyika ndani ya nyumba tena kwenye ghala la zamani; hii ina maana kuwa kilimo hiki kinaweza kufanyika popote bila kuathiriwa na hali ya hewa. Wazo hili lilianzishwa na Ed Harwood, ambaye ni profesa kwenye Chuo cha kilimo cha Cornel aliyetaka kupanda vitu bila kutumia vitu vinavyokuza vitu. Kilimo bila ardhi au udongo AeroFarms wametengeneza vitu kama rafu au shelfu ambavo zina vitambaa maalumu ambavyo mbegu husiwia juu yake badala ya udongo. Mizizi ya mmea husika hujishikiza katika kitambaa hicho kuelekea chini kujipatia virutubisho na maji. Rafu/...
Usalama wa Msingi wa Kompyuta: Jinsi ya Kujilinda na Virusi, Wadukuzi na Wezi

Usalama wa Msingi wa Kompyuta: Jinsi ya Kujilinda na Virusi, Wadukuzi na Wezi

Teknolojia
Watu wengi hufikiri kuwa usalama wa kompyuta ni swala gumu lenye changamoto kubwa. Inaweza kuwa hivyo kama hukuchukua hatua sahihi mapema. Katika makala hii utafahamu hatua tano muhimu ambazo zitakuwezesha kujilinda na virusi, wadukuzi na wezi katika kifaa chako cha kielektroniki. 1. Wezesha automatiki sasishi (automatic updates) Programu mbalimbali za kompyuta hutoa masasisho (updates) mara kwa mara ili kuziba mianya mbalimbali hasa ya kiusalama iliyobainika katika matoleo ya awali. Program kama Microsoft Window, Mozilla na Chrome ni baadhi ya programu muhimu zinazohitajika kusasishwa kwa wakati. Hivi leo programu mbalimbali huja na usasishaji wa automatiki lakini watu wengi hupenda kuuzima usasishaji huu bila kuzingatia umuhimu wake wa kiusalama. Hivyo basi, ili kuwa salama zing...
Wanasayansi Wagundua  Rangi inayotumia Jua Kuzalisha Nishati

Wanasayansi Wagundua Rangi inayotumia Jua Kuzalisha Nishati

Habari, Teknolojia
Timu ya wanasayansi nchini Australia imegundua rangi ya sola ambayo inaweza kuzalisha nishati kwa ajili ya matumizi ya majumbani na magari. Timu hiyo iliyoongozwa na Torben Daeneke imesema kuwa inaamini kuwa njia hiyo itatoa nishati nafuu na safi kwa dunia. Nishati kwa ajili ya magari siku za mbeleni Inaweza kufikiriwa kuwa, kuendesha gari kwa nishati itokanayo na rangi ni kichekesho lakini wanayansi hao wamesema inawezekana. Wamesema kwa kuchanganya katalisti yenye rangi nyeupe inayotumika kwenye dawa ya meno, wanasyansi waliweza kutengeneza rangi ambayo ikikutana na jua inabadili maji kuwa hydrojeni ambayo itatumika kuendesha gari. Wamesema changamoto waliyonayo ni namna ya kuhamisha nishati hiyo na kuitumia kwenye gari; pamoja na hili wamesema wameshapata njia kadhaa wanazozifa...