Hivi leo wabunifu mbalimbali wametokea duniani. Wabunifu wengine wamejikita kwenye kutumia ubunifu wao kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za uharibifu wa mazingira.
Wapo watu na wabunifu mbalimbali walioona umuhimu wakutengeneza (recycle) tena vitu mbalimbali ambavyo matumizi yake yamekwisha, ili vifae tena kwa matumizi mengine.
Mara nyingi tumeshuhudia magurudumu, chupa, mapipa, na hata vifaa vya mitambo mbalimbali vikitupwa hovyo baada ya kumalizika kwa matumizi yake.
Lakini sasa ungana nami nikushirikishe vitu kadhaa vilivyotengenezwa upya (recycled) na kuzalisha vitu vya kuvutia na vyenye tija kubwa.
1. Mapipa ya kemikali na mafuta
2. Matairi yaliyozeeka
3. Injini ya gari na sehemu nyingine za gari
4. Sehemu za baisikeli
5. Chupa za plastiki
Picha hizi zinaletwa kwako kwa hisani ya Kurdsat TV pamoja na Architecturendesign.
Je umejifunza kitu? Je umehamasika kutunza mazingira kwa kuunda upya vitu vilivyomaliza matumizi yake? Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini. Usisahau pia kuwashirikisha wengine makala hii na kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili ufahamu mengi zaidi.
Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.