Maarifa Archives - Page 2 of 2 - Fahamu Hili
Sunday, August 25Maarifa Bila Kikomo

Maarifa

Mambo 25 Yakushangaza Kuhusu Mwili wa Binadamu

Mambo 25 Yakushangaza Kuhusu Mwili wa Binadamu

Maarifa
Inawezekana unatazama mwili wako kwa juu juu pekee bila kufahamu mambo mengi yaliyojificha kwenye mwili wako. Ni hakika kuwa mwili umeumbwa kwa namna ya pekee sana inayouwezesha kufanya kazi pamoja na kuonekana jinsi ulivyo. Naamini unapenda kupata maarifa kwa kuufahamu mwili wako vyema. Karibu ufuatilie makala hii ili nikujuze mambo 25 yakukushangaza kuhusu mwili wa binadamu. 1. Ubongo unatumia asilimia 20 ya oksijeni pamoja na kalori Ni wazi kuwa utendaji kazi wa ubongo unahitaji oksijeni asilimia 20 pamoja na kalori kutoka kwenye mwili ili kufanya kazi jinsi ipasavyo. 2. Kila mtu ana harufu yake Mbali na mapacha wa kufanana, kila mtu ana harufu yake ya pekee inayomtofautisha kati yake na mtu mwingine. 3. Uwezo mkubwa wa kufikiri unahusiana na kiasi cha ndoto mtu anazoota In...
Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Maarifa, Teknolojia
Hivi leo kuna mambo mengi kuhusu intaneti, lakini hapa nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuvutia na kukushangaza. Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambamba na maendeleo ya kompyuta. Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi. Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua. 1. Tovuti ya kwanza bado ipo Tovuti ya kwanza kutengenezwa bado ipo na inafanya kazi hadi leo. Jambo pekee ni ku...
Mambo 15 ya Kushangaza Kuhusu Afrika

Mambo 15 ya Kushangaza Kuhusu Afrika

Maarifa
Vita, njaa, vifo, maradhi - ni vitu ambavyo wengi wamevisikia na kuvifahamu kuhusu Afrika. Lakini sasa ni wakati wa kubadili mtazamo huu. Afrika ni bara la kushangaza ambalo ni tofauti kabisa na mabara mengine saba. Afrika ina utajiri katika urithi wa utamaduni wa kipekee, utajiri wa rasilimali za asili pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii. Nakukaribisha ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu mambo 15 ya kushangaza na kusisimua kuhusu Afrika. Mlima Kilimanjaro unapatikana barani Afrika. Mlima huu una urefu wa takriban meta 5,895 kutoka usawa wa bahari. Mlima huu unapatikana kaskazini mwa Tanzania. Zaidi la asilimia 25 ya lugha huzungumzwa Afrika. Inaaminika kuwa kuna takriban lugha 2000 zinazozungumzwa barani Afrika. Lugha zote hizi zinatambuliwa na umoja wa Afrika. Nigeri...
Mambo 6 Usiyoyafahamu Kuhusu Pesa

Mambo 6 Usiyoyafahamu Kuhusu Pesa

Maarifa
Inawezekana unabeba pesa kwenye pochi au mfuko wako au pengine umezitunza benki, lakini ni kwa kiasi gani unafahamu kuhusu pesa? Ni dhahiri kuwa unaweza kuzitumia pesa hadi mwisho wa maisha yako bila hata kujua mambo fulani yanayozihusu. Fuatilia makala hii nikufahamishe mambo 6 usiyoyafahamu kuhusu pesa. 1. Pesa ya noti siyo karatasi Watu wengi wanafikiri kuwa pesa ya noti imetengenezwa kwa karatasi lakini si kweli. Malighafi zilizotengenezea pesa ya noti, mojawapo ni pamba. Imetengenezwa hivi ili iwe imara zaidi na yenye kukabiliana na mambo kama vile vimiminika na uchafu. 2. Wazo la ATM liliibuka bafuni Mgunduzi John Shepherd-Barron alipata wazo la kuweka ATM bafuni manamo miaka ya 1960 akiwa bafuni. 3. Pesa zina virusi vya mafua na cocaine Utafiti umebaini kuwa kutokana n...
Kazi za Sanaa Zitakazokushangaza

Kazi za Sanaa Zitakazokushangaza

Maarifa
Kila mtu ana kipawa chake alichopewa. Inawezekana ni kuimba, kuchora, kucheza mchezo fulani n.k. Lakini wapo watu ambao wamevitumia vipawa vyao kwa kiwango kinachostaajabisha wengi. Wapo waliofanya kazi kama vile ubunifu wa picha na maumbo kiasi cha kumfanya mtazamaji kushindwa kutofautisha kitu kilichosanifiwa na halisi. Fuatilia ukurasa huu mara kwa  mara kwani nitakuwa nikiweka kazi mbalimbali za kushangaza zilizofanywa na wabunifu mbalimbali. Anza kwa kutazama hizi zifuatazo hapo chini; pia kama una maoni, ushauri, swali, au kazi ambayo ungependa ionyeshwe hapa basi usisite kutujulisha. Karibu. Kumbuka hapa hatuonyeshi kazi feki zitokanazo na uhariri wa kompyuta! Ikumbukwe kuwa umiliki wa kazi hizi utabaki kuwa wa wamiliki na si vinginevyo. Ikiwa msanii hapendi kazi yake ionekane