Tija Archives - Page 3 of 3 - Fahamu Hili
Saturday, April 20Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Tija

Programu 6  za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza

Programu 6 za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza

Tija
Kama wewe ni mwandishi wa machapisho au wa blogu, unafahamu jinsi ilivyo muhimu kuandika makala zenye ubora. Wengi wetu hutumia muda mwingi kuandika, kubuni na hata kupangilia makala au machapisho yetu kuliko muda tunaotumia kuhariri. Kuhariri ni sehemu muhimu katika uandishi wowote ili kukuwezesha kuandika makala yenye ubora. Kwa kutambua umuhimu huu nimekuandalia orodha ya programu 6 za kompyuta zitakazokuwezesha kupunguza kama siyo kuondoa kabisa makosa katika uandishi wa Kiingereza Soma pia: Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora. 1. Grammarly Hii ni programu maarufu sana yenye uwezo wa kubaini makosa mengi ambayo usingeweza kuyabaini kwa njia ya kawaida. Kiunganishi: Grammarly 2. Polishmywriting Hii ni programu nzuri ya kuhariri inayoonyesha makosa kwa rangi tatu. Nyekundu ni mako...
Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema

Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema

Kipato, Tija
Je, huwa unajisikia vibaya unapohitaji pesa kwa ajili ya matumizi yako lakini unajikuta mifuko yako ni mitupu? Haijalishi unapata pesa kiasi gani, swala la matumizi mazuri ya pesa ni jambo muhimu; hili litakuwezesha kuwa na kitu wakati wa uhitaji. Watu wengi wanapata pesa lakini si wote wanaoweza kuzitumia vyema. Wengi hujikuta wakizitumia kwenye mambo na mipango ambayo mwishoni haiwaletei tija katika maisha yao. Naamini ungependa kuwa na matumizi mazuri ya pesa; sasa fahamu njia 10 zitakazokuwezesha kutumia pesa vyema. 1. Weka bajeti Ni rahisi kusikia watu wakilalamikia bajeti za serekali na kuzikosoa lakini wao wenyewe hawana bajeti zao binafsi. Unawezaje kukosoa bajeti ya serekali wakati ya kwako mwenyewe imekushinda? Fikiri tofauti; tambua umuhimu na jinsi ya kujiwekea baje...
Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora

Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora

Tija
Hakuna uandishi bora au andiko bora pasipo uhariri bora. Hivyo uandishi mzuri hauwezi kutengwa na uhariri bora. Ni dhahiri kuwa makala au andiko lililohaririwa vyema na kwa ustadi wa hali ya juu litakubalika na kupendwa na wasomaji wengi zaidi. Watu wengi wamekuwa wakitamani kuandika matini zilizohaririwa vyema lakini wamekuwa wakikwama juu ya ni njia gani wanaweza kuwa wahariri bora. Pengine umekuwa ukitamani kunufaika kupitia kazi ya uhariri lakini hujui ufanyeje ili uweze kuwa mhariri bora. Fuatana nami katika makala hii nikueleze njia 10 zitakazokufanya kuwa mhariri bora. 1. Jifunze sarufi ya lugha na kanuni za uandishi Uhariri ni taaluma kama ilivyo kwa taaluma nyingine. Hivyo ili uwe mhariri bora basi huna budi kujifunza kanuni za sarufi ya lugha husika pamoja na kanuni za uand...
Mbinu 7 za Kuwa Mwandishi Bora

Mbinu 7 za Kuwa Mwandishi Bora

Tija
Kama umewahi kuwa na ndoto au matamanio ya kuwa mwandishi mkubwa kama vile Wole Soyinka, Ngũgĩ wa Thiong'o au pengine hata kuwa mwandishi bora kitaaluma au katika blogu yako, basi ni vyema ukajifunza namna ya kuwa mwandishi bora. Kuwa mwandishi bora si jambo la mzaha; ni jambo linalalowezekana ikiwa utaweka jitihada stahiki. Ni dhahiri kuwa jitihada utakazozifanya hazitakuwa bure kwani hivi leo kuna fursa mabalimbali zinazohitaji watu wenye uwezo mzuri wa uandishi. Hivyo basi, fuatana nami nikujuze mbinu zitakazokuwezesha kuwa mwandishi bora kabisa na kufikia malengo yako ya mbeleni. 1. Soma maandiko bora Ni dhahiri kuwa ukihitaji kufahamu nini mana ya uandishi bora ni lazima usome maandiko bora yaliyoandikwa na waandishi mahiri. Soma maandiko bora kadri uwezavyo kwani utaji...
Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako

Aina 8 za Watu Ambazo ni Sumu za Kuepuka Maishani Mwako

Tija
Watu wasiofaa wapo kila mahali, kwa hakika wanakwaza na kurudisha maendeleo ya watu nyuma. Ukiwa kama mjasiriamali au mtu mwingine yeyote unatakiwa kufanya bidii kufikia malengo yako bila kuruhusu aina za watu wasiofaa kukuvuruga. Inawezekana unawafahamu watu ambao ni sumu; yawezekana wanafanya kazi na wewe, ni marafiki zako au unaishi nao. Kadri unavyowaepuka katika maisha au kazi yako ndivyo mambo yatakavyozidi kuwa mazuri. Fuatana nami katika makala hii nikushirikishe aina 8 za watu ambazo ni sumu unazotakiwa kuziepuka katika maisha yako. 1. Watu wanaohoji kila kitu Watu wanaohoji kila kitu hutafuta njia ya kupinga na kukosoa kila unachokifanya. Utatumia muda mwingi kuwaelewesha lakini watasikia kwa sikio moja na swala hilo kutokea sikio la pili. Kujaribu kutafuta msaada na ...
Njia 8 za Kuokoa Mafuta Unapoendesha Gari

Njia 8 za Kuokoa Mafuta Unapoendesha Gari

Tija, Usafiri na Safari
Ni wazi kuwa gari linahitaji mafuta ili kusafiri toka sehemu moja hadi nyingine. Lakini swali ni je, unaweza kutawala kiwango cha mafuta kinachotumika? Ndiyo, unawea kutawana kiwango cha mafuta na kupunguza garama za matumizi ya mafuta zisizokuwa na ulazima. Kama unapenda kuokoa kiasi cha mafuta yanayopotea bila sababu ya msingi katika gari lako, basi tumia njia hizi 8 zifuatazo. 1. Kabili upepo Unapoendesha gari upepo hukinzana na gari; hivyo kadri gari linavyokinzana zaidi na upepo ndiyo pia unavyotumia mafuta mengi zaidi. Hivyo basi, usipende kuweka mizigo juu ya gari kwa nje (carrier) au kufungua vioo kwani kutasabisha ukinzani zaidi kati ya gari na upepo. Kwa kukabili upepo vyema utapunguza ukinzani na kuokoa mafuta ambayo yangetumika kukabili ukinzani huo wa upepo. 2. Pu...
Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Maendeleo Binafsi, Tija
Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha yake. Wengine wana ndoto kubwa za kubadilisha ulimwengu huu, huku wengine wakiwa na ndoto za kuishi maisha ya kupata mahitaji yao ya msingi tu. Wote hawa wanahitaji kuzitimiza ndoto zao; lakini kuna vikwazo na mambo mbalimbali ambayo huwazuia watu wasiishi ndoto zao na kuishia kulamu na kulalamika hasa uzeeni. Fuatana nami katika makala hii nikueleze dondoo tano za msingi zitakazokuwezesha kuishi ndoto zako. 1. Tambua kinachokuvuruga Maisha yetu ya kila siku yamejaa vitu na shunguli mbalimbali lakini si zote huturuhusu kuishi katika ndoto zetu. Inawezekana unapenda kitu au tabia fulani kiasi kwamba imetawala au imekuwa ya kwanza kwenye maisha yako. Nitajuaje kitu au tabia imetawala/imekuwa ya kwanza katika maisha? Jibu ni rahisi, kile una...
Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Maendeleo Binafsi, Tija
Mafanikio yana maana mbalimbali kwa kila mtu; kama vile uzuri unavyotofautiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine. Ni jukumu lako kubainisha ni nini maana ya mafanikio na ni kwa namna gani utayafikia mafaniko hayo. Fuatana nami nikushirkishe vitu 10 vinavyozuia mafaniko yako kama unataka kuona na kufikia mafanikio yako. 1. Kutoa visingizio Acha kulaumu na kulalamikia watu wengine kwa kutokupata kile unachokihitaji. Acha kusingizia serekali na jamii kuwa ndiyo kikwazo cha wewe kufikia mafanikio yako. Watu waliofanikiwa hawalalamiki bali wanafanya kazi kwa bidii kufikia malengo yao. Kumbuka hakuna mtu aliyefanikiwa sana duniani kwa kusaidiwa na serikali au mtu fulani katika jamii; ukiwepo msaada basi utumie tu kama ngazi. 2. Kutazama tu mapungufu Umejijengea dhamiri ya kutofanya c...
Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Maendeleo Binafsi, Tija
Miaka kadhaa iliyopita mawasiliano yalikuwa magumu na ya gharama kubwa. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, mawasiliano yamerahisishwa na kuwa ya uhakika zaidi huku ghrama pia ikipungua. Kuwepo wa mtandao wa intaneti pamoja na mitandao ya kijamii kumewafanya watu kukaribiana zaidi. Baada ya kuanzishwa kwa mtandao wa Facebook ambao ulianzia huko Marekani na baadaye kuenea dunia nzima maisha ya watu yamebadilika sana. Facebook ina watumiaji hai zaidi ya bilioni 1.23 na bado Facebook inalenga kuwaongeza zaidi ili kuwafikia watu wote duniani. Pamoja na maendeleo haya makubwa kumeshuhudiwa madhara au changamoto kadha wa kanda zinazotokana na mitandao ya kijamii hasa Facebook. Hivyo basi hapa nitafafanua sababu kadhaa zinazodhihirisha ni kwa namna gani Facebook inakup...
Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Maendeleo Binafsi, Tija
Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako. Ni kweli kuwa baadhi ya watu huanza maisha katika mazingira rafiki zaidi, lakini ninaamini kila mmoja ana nafasi na uwezo ya kufanikiwa. Haya ni baadhi mambo ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya na kujiambia na yamewatenga na mafanikio yao. 1. Ninahitaji shahada ya chuo kikuu ili kufanikiwa Unahitaji shahada kupata kazi katika ofisi fulani lakini si kuwa majasiriamali katika ofisi yako wewe mwenyewe. Ipo mifano kadha wa kadha duniani ya watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wakubwa bila kuwa na shahada ya chuo kikuu. Mfano wa watu hao ni Mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg. Hivyo basi fanya maamuzi leo ili ufikie kiwango bora cha...