Nukuu (Quotes) 25 za Malengo Zitakazokuhamasisha - Fahamu Hili
Saturday, April 20Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Nukuu (Quotes) 25 za Malengo Zitakazokuhamasisha

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Nukuu za malengo

Malengo ni muhimu sana kwenye maisha ili yatuongoze kufikia mafanikio yetu au kuwa yule ambaye tunapaswa kuwa. Kwa hakika, ikiwa huna malengo ni wakati wa kujiwekea malengo sasa; na ikiwa unayo basi ni wakati wa kutathimini kama unayaelekea.

Kwa kutambua umuhimu wa malengo maishani, karibu nikushirikishe nukuu (quotes) 25 za malengo ambazo zitakuhamasisha kufikia malengo yako.

 1. “Kuweka malengo ni hatua ya kwanza ya kugeuza yasiyoonekana yaoonekane.”

  Tony Robbins
 2. “Weka malengo makubwa, usiache mpaka uyafikie.”

  Bo Jackson
 3. “Nidhamu ni daraja kati ya malengo na ukamilishaji.”

  Jim Rohn
 4. “Fikiri malengo madogo na utarajie mafanikio madogo. Fikiri malengo makubwa na upate mafanikio makubwa.”

  David Joseph Schwartz
 5. “Njia pekee ya kupata msukumo wa kuendelea mbele ni kuwa na malengo makubwa kila wakati.”

  Michael Korda
 6. “Watu wenye malengo hufanikiwa kwa sababu wanajua ni wapi wanakokwenda.”

  Earl Nightingale
 7. “Pitia malengo yako mara mbili kwa siku ili kujikita kwenye kuyafanikisha.”

  Les Brown
 8. “Kinachonifanya niendelee mbele ni malengo.”

  Muhammad Ali
 9. “Malengo huamua unaelekea kuwa nani.”

  Julius Erving
 10. “Kuweka malengo na kuendelea nayo mbele kunasisimua.”

  Amber Frey
 11. “Unahitaji malengo ya juu. Kisha uyaimarishe kwa maadili mazuri ya kazi.”

  Jerry West
 12. “Malengo hukusaidia kuelekeza nguvu yako kwenye matendo.”

  Les Brown
 13. “Malengo hayaji kirahisi. Hakuna mtu anayekupa malengo.”

  Frank Lampard
 14. “Kazi yangu ni kushinda malengo.”

  Peter Bondra
 15. “Hamasa moyoni mwangu ni kufanya kazi kuelekea malengo na ndoto zangu.”

  Nonito Donaire
 16. “Unapaswa kuwa mtu unayeweka malengo yako wewe mwenyewe, na kujaribu kufikia malengo hayo.”

  Johnny Bench
 17. “Kila siku nafanya ndoto zangu kuwa malengo.”

  DJ Khaled
 18. “Unaweza ukafanya chochote kama utaweka malengo. Unahitajika tu kujisukuma wewe mwenyewe.”

  RJ Mitte
 19. “Ninafurahia kufanya kazi kwa bidii; ninapenda kuweka malengo na kuyafikia.”

  Jewel
 20. “Mungu aliniumba niwaburudishe watu kwa malengo yangu.”

  Romario
 21. “Kuweka malengo na kuyafanikisha malengo hayo — hiki ndicho tu ninachofanya.”

  Lisa Leslie
 22. “Malengo hukufanya ufanye zaidi kwa ajili yako na wengine pia.”

  Zig Ziglar
 23. “Sijawahi kuacha kutazama malengo yangu. Sijawahi kuacha kufikiri kuwa ninaweza kufika juu.”

  Robbie Lawler
 24. “Bila malengo ningekuwa nimekufa. Nahitaji kitu kinachonifanya niendelee mbele.”

  Katrina Kaif
 25. “Kama unataka kuishi maisha ya furaha, yashikize na malengo na wala si watu au vitu.”

  Albert Einstein

Naamini umefurahia nukuu hizi pamoja na kuhamasika kuendelea kupigania malengo yako.

Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako

Tafadhali andika maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Unaweza kutufuatilia kwa barua pepe au kwa kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x