Kahawa ni kinywaji maarufu na kinachopendwa sana na watu wengi. Kahawa pia imekuwa ni zao mashuhuri la kibiashara duniani kwa muda mrefu.
Kwa hakika umaarufu na kupendwa kwa kinywaji cha kahawa unatokana na manufaa kadhaa yanayopatikana ndani ya kinywaji hiki.
Ikiwa unapenda kunywa kahawa au unapenda kuongeza maarifa yako, basi fahamu faida 10 za kunywa kahawa.
1. Huchangamsha mwili
Kahawa huwafanya watu wasijisikie kuchoka na huwaongezea kiwango cha nguvu za mwili. Caffeine inayopatikana kwenye kahawa huuchangamsha ubongo na kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.
Hii ndiyo sababu watu wengi wenye kazi nyingi hupenda kunywa kahawa wakati wa kazi au baada ya kazi zao.
2. Huyeyusha mafuta mwilini
Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kahawa huchangia katika kuyeyusha mafuta mwilini na kupelekea kupunguza uzito wa mwili.
Utafiti mmoja uliofanyika ulibaini kuwa kahawa iliweza kusaidia kupunguza mafuta kwa watu wanene kwa asilimia 10 na kwa asilimia 29 kwa watu wembamba.
3. Kahawa ina virutubisho muhimu
Kahawa ni kinywaji chenye virutubisho muhimu kwa ajili ya afya za miili yetu.
Inaelezwa kuwa kikombe kimoja cha kahawa kina virutubisho vifuatavyo:
- Riboflavin (Vitamini B2): 11%.
- Asidi ya Pantothenic (Vitamini B5): 6%.
- Manganese na Potasiamu: 3%.
- Magnesiamu na Niacin (B3): 2%.
Hivyo kunywa vikombe 2-3 kwa siku kutaongeza kiwango cha virutubisho hivi.
4. Hukabili aina ya pili ya kisukari
Kisukari ni ugonjwa ambao mwili hushindwa kutawala kiwango cha sukari mwilini. Inakadiriwa kuwa ugonjwa huu unawatesa zaidi ya watu milioni 300 duniani kote.
Hata hivyo, inasadikiwa kuwa watumiaji wa kahawa wana hatari ndogo ya kupata aina ya pili ya kisukari (type 2 diabetes).
5. Huzuia maradhi ya kupoteza kumbukumbu
Maradhi ya kupoteza kumbukumbu huwakabili watu wengi hasa wenye umri wa kuanzia miaka 65.
Kwa sasa hakuna tiba ya maradhi haya lakini yanaweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa lishe bora pamoja na mazoezi.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa watu wanaokunywa kahawa hupunguza kama siyo kukabili athari za maradhi haya kwa asilimia 65.
6. Hulinda afya ya ini
Ini ni kiungo muhimu sana kwenye mwili wa binadamu. Hata hivyo maradhi kama vile uvimbe kwenye ini (hepatitis) pamoja na tatizo la seli za ini kugeuka makovu (cirrhosis), huathiri afya ya ini kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande mwingine tafiti zinaeleza kuwa kahawa hupunguza uwezo wa seli za ini kuwa makovu (cirrhosis) kwa asilimia 80.
Soma pia: Madhara 12 ya Pombe Kiafya
7. Huondoa msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo ni tatizo baya la kiakili na kisaikolojia ambalo linaweza kuathiri maisha kwa kiasi kikubwa hata kusababisha kifo.
Inaelezwa kuwa watu wanaokunywa angalau vikombe vinne vya kahawa kila siku hupunguza msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa.
8. Hukabili baadhi ya saratani
Saratani ni maradhi yanayoua watu wengi sana duniani ambayo husababishwa na kukua kwa seli zisizo za kawaida ndani ya mwili wa binadamu.
Kahawa husaidia kupunguza kutokea kwa saratani ya ini na ile ya utumbo kwa asilimia 40.
9. Hukabili maradhi ya moyo na kiharusi
Watafiti mbalimbali wa afya wanaeleza kuwa kahawa haisababishi maradhi ya moyo pia huzuia kwa asilimia 20 uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kiharusi (stroke).
10. Hukufanya uishi muda mrefu
Kama ulivyotangulia kusoma katika hoja zilizotangulia kuwa kahawa huzuia maradhi mbalimbali. Hivyo huwafanya watu wanaokunywa kahawa kuishi muda mrefu zaidi kwa kuwaepushia kufa mapema.
Watafiti wanaeleza kuwa hatari ya kifo hupungua kwa silimia 20 kwa wanaume na asilimia 26 kwa wanawake wanaokunywa kahawa.
Soma pia: Sababu 6 za Kwanini Mara Nyingi Wanawake Huishi Zaidi ya Wanaume
Hitimisho
Naamini baada ya kusoma makala hii hutokunywa tena kahawa kwa mazoea au kupuuza unywaji wa kahawa kwani una manufaa kemkem.
Sanjari na hayo ni muhimu kukumbuka kuwa kila kitu chenye uzuri kina ubaya wake, hivyo ni muhimu kuwa na kiasi katika mambo yote ikiwemo unywaji wa kahawa.
Soma pia: Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini
Je wewe huwa unakunywa kahawa? Je unanufaika vipi? Tafadhali tuandikie maoni yako kisha washirikishe wengine makala hii.
Eston ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zinazohusu tija, maendeleo binafsi pamoja na afya bora. Analenga kuwahamasisha wengine pamoja na kuubadili ulimwengu kwa kupitia maarifa stahiki.
ina faida nyingi hasa katika kujenga mwili
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Asante kwa somo zuri
Tunashukuru sana kwa kuwa msomaji wetu; pia tunashukuru kwa maoni yako ya thamani; tunakutakia kila la heri katika kutimiza malengo yako…karibu sana Fahamuhili.
mimi bila kunywa kahawa nakuwa mchovu sana nasinzia hovyo hovyo ukweli kahawa ni mkombozi wangu kimawazo kiakili
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Asante jmn nlikuwa sijui
Asante sana; karibu sana Fahamuhili.com
Aisee kahawa n nzur Sana. Inaondoa usingiz
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; karibu sana Fahamuhili.com
Asante kwa somo !
Swali.
Nini madhara ya utumiaji kahawa kupitiliza?
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Tutajitahidi kuandaa makala juu ya hilo. Karibu sana Fahamuhili.com
Nimefurah sana.Taratiiiiibu naanzisha utaratibu wa kunywa kahawa.
Asante sana kwa maoni yako ya thamani; na kwa kuwa msomaji wetu. Karibu sana Fahamuhili.com
Hongeraihho