Maendeleo Binafsi Archives - Page 3 of 3 - Fahamu Hili
Tuesday, January 21Maarifa Bila Kikomo

Maendeleo Binafsi

Sababu 9 za Kwanini Umsamehe Aliyekukosea

Sababu 9 za Kwanini Umsamehe Aliyekukosea

Maendeleo Binafsi
Umesikia mara nyingi sana kuwa “Unatakiwa kusamehe na kusahau”. Nini maana halisi ya kusamehe? Kusamehe ni kuamua kutomchukulia mtu hatua na kuondoa kinyongo moyoni mwako kutokana na jambo baya ulilofanyiwa na mtu huyo. Kusamehe kunasema hutakiwi kusikia neno “nisamehe” ndipo uendelee na maisha yako. Kusamehe kumewekwa na ni kwa manufaa zaidi kwa yule aliyekosewa. Ni wazi kuwa katika maisha kuna kukoseana kwa namna mbalimbali. Wapo watu wasiopenda suluhu wala msamaha. Ni dhahiri kuwa ni lazima wewe uliyekosea ufahamu manufaa na sababu za kumsamehe na kumsahau aliyekukosea; manufaa hayo ni haya yafuatayo. 1. Hukuweka huru Kutokusamehe kunakufanya ujisikie vibaya na kuwa kama mfungwa. Jambo baya ni pale utakapomwona yule aliyekukosea anafuraha na anaendelea na maisha yake bila ta
Namna ya Kuwa Mzungumzaji Hamasa (Motivational Speaker)

Namna ya Kuwa Mzungumzaji Hamasa (Motivational Speaker)

Maendeleo Binafsi
Ninapotaja wazungumzaji hamasa (Motivational Speakers) naamini unafahamu kuwa ni watu wanaowasaidia watu kuendeleza na kuwezesha maono au utoto wao wa ndani ili watu husika waweze kufanikiwa. Mzungumzaji hamasa anaweza kuzungumzia mada yoyote ile kulingana na uzoefu wake. Wengi hutamani kuwa wazungumzaji hamasa lakini wameshindwa kujua waanzie wapi. Jambo la msingi katika uzungumzaji hamasa ni shauku yako ya ndani katika mada unayotaka kuizungumzia. Kuwa mzungumzaji hamasa kunahitaji kubaini mada na walengwa wa mada yako bila kusahau kunoa uwezo wako wa kuzungumza mbele ya watu pamoja na kuielewa vyema mada husika. Kama unatamani kuwa mzungumzaji hamasa, fuatilia hoja jadiliwa hapa chini kwa makini ili sasa uweze kuwa mzungumzaji hamasa. 1. Bainisha mada utakayozungumzia Huwezi ku...
Njia 10 za Kujenga Uwezo wa Kuzungumza Mbele ya Watu

Njia 10 za Kujenga Uwezo wa Kuzungumza Mbele ya Watu

Maendeleo Binafsi
Kuzungumza mbele ya watu kunaweza kuwa ni tatizo ikiwa hujiamini au hujajiandaa vyema. Hata hivyo, mazoezi na mtazamo chanya vinaweza kukusaidia kuwa mzungumzaji bora mbele ya watu. Ikiwa unazungumza katika mazingira ya kitaaluma au katika mazingira ya kijamii, tumia njia hizi 10 ili kuboresha uwezo wako vya kuzungumza mbele ya watu. Kumbuka, kuzungumza mbele ya watu kunahusisha kuandaa, kufikiria na kutenda kwa ujasiri, huku ukizingatia sauti yako na lugha ya mwili (body language). 1. Jiandae na fanya mazoezi Watu wengi wamekuwa wakikumbwa na hofu, wasiwasi na hata kutokwa na jasho sana wanapokuwa wanazungumza mbele za watu. Hii inatokana na kuwa na uzoefu mdogo unaoletwa na kutofanya mazoezi ya kutosha ya kuzungumza mbele ya watu. Jitahidi kufanya mazoezi ya kuzungumza mbele za ...
Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Dondoo 5 za Kuishi Ndoto Zako

Maendeleo Binafsi, Tija
Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha yake. Wengine wana ndoto kubwa za kubadilisha ulimwengu huu, huku wengine wakiwa na ndoto za kuishi maisha ya kupata mahitaji yao ya msingi tu. Wote hawa wanahitaji kuzitimiza ndoto zao; lakini kuna vikwazo na mambo mbalimbali ambayo huwazuia watu wasiishi ndoto zao na kuishia kulamu na kulalamika hasa uzeeni. Fuatana nami katika makala hii nikueleze dondoo tano za msingi zitakazokuwezesha kuishi ndoto zako. 1. Tambua kinachokuvuruga Maisha yetu ya kila siku yamejaa vitu na shunguli mbalimbali lakini si zote huturuhusu kuishi katika ndoto zetu. Inawezekana unapenda kitu au tabia fulani kiasi kwamba imetawala au imekuwa ya kwanza kwenye maisha yako. Nitajuaje kitu au tabia imetawala/imekuwa ya kwanza katika maisha? Jibu ni rahisi, kile una...
Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Vitu 10 unavyotakiwa Kuacha Kama Unataka Kufanikiwa

Maendeleo Binafsi, Tija
Mafanikio yana maana mbalimbali kwa kila mtu; kama vile uzuri unavyotofautiana kati ya mtu mmoja hadi mwingine. Ni jukumu lako kubainisha ni nini maana ya mafanikio na ni kwa namna gani utayafikia mafaniko hayo. Fuatana nami nikushirkishe vitu 10 vinavyozuia mafaniko yako kama unataka kuona na kufikia mafanikio yako. 1. Kutoa visingizio Acha kulaumu na kulalamikia watu wengine kwa kutokupata kile unachokihitaji. Acha kusingizia serekali na jamii kuwa ndiyo kikwazo cha wewe kufikia mafanikio yako. Watu waliofanikiwa hawalalamiki bali wanafanya kazi kwa bidii kufikia malengo yao. Kumbuka hakuna mtu aliyefanikiwa sana duniani kwa kusaidiwa na serikali au mtu fulani katika jamii; ukiwepo msaada basi utumie tu kama ngazi. 2. Kutazama tu mapungufu Umejijengea dhamiri ya kutofanya c...
Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Sababu 7 za Kwanini Uachane na Facebook Sasa Kwa Ajili ya Baadaye Yako

Maendeleo Binafsi, Tija
Miaka kadhaa iliyopita mawasiliano yalikuwa magumu na ya gharama kubwa. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, mawasiliano yamerahisishwa na kuwa ya uhakika zaidi huku ghrama pia ikipungua. Kuwepo wa mtandao wa intaneti pamoja na mitandao ya kijamii kumewafanya watu kukaribiana zaidi. Baada ya kuanzishwa kwa mtandao wa Facebook ambao ulianzia huko Marekani na baadaye kuenea dunia nzima maisha ya watu yamebadilika sana. Facebook ina watumiaji hai zaidi ya bilioni 1.23 na bado Facebook inalenga kuwaongeza zaidi ili kuwafikia watu wote duniani. Pamoja na maendeleo haya makubwa kumeshuhudiwa madhara au changamoto kadha wa kanda zinazotokana na mitandao ya kijamii hasa Facebook. Hivyo basi hapa nitafafanua sababu kadhaa zinazodhihirisha ni kwa namna gani Facebook inakup...
Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Mambo Manne Yatakayokutenga na Mafanikio Yako

Maendeleo Binafsi, Tija
Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako. Ni kweli kuwa baadhi ya watu huanza maisha katika mazingira rafiki zaidi, lakini ninaamini kila mmoja ana nafasi na uwezo ya kufanikiwa. Haya ni baadhi mambo ambayo watu wengi wamekuwa wakiyafanya na kujiambia na yamewatenga na mafanikio yao. 1. Ninahitaji shahada ya chuo kikuu ili kufanikiwa Unahitaji shahada kupata kazi katika ofisi fulani lakini si kuwa majasiriamali katika ofisi yako wewe mwenyewe. Ipo mifano kadha wa kadha duniani ya watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wakubwa bila kuwa na shahada ya chuo kikuu. Mfano wa watu hao ni Mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg. Hivyo basi fanya maamuzi leo ili ufikie kiwango bora cha...
Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda

Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda

Maendeleo Binafsi
Mambo yote katika maisha yetu yamefungwa kwenye muda, hivyo ni vyema kufahamu namna bora ya kutumia muda kwa njia yenye mafanikio. Kutumia muda vyema siyo tu kutakuwezesha kufanya kazi vyema, bali kutakuwezesha kuishi maisha vyema. Ni muhimu kupata muda wa kufanya mambo yote ya muhimu kwenye maisha yako, kwani kila moja lina nafasi na umuhimu wake. Hapa nitaeleza kanuni 9 yatakayokuwezesha kutawala muda vyema. 1. Anza na panga siku yako vyema Usikimbilie kuanza majuku yako ya siku bila kukaa chini na kutumia dakika chache za kutafakari mambo kadhaa. Tafakari ni jambo gani muhimu zaidi ili uweze kulipa kipaumbele katika siku yako. Jifunze kujiwekea malengo, haya yatakuwezesha kujua nini unachotakiwa kukitimiza ndani ya siku yako. Kwa njia hii utaweza kukamilisha vitu kulin...
Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora

Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora

Maendeleo Binafsi
Je kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wengi au miaka mingi katika uongozi? La hasha, kiongozi bora hujengwa kwa sifa anuwai. Ni rahisi kufikiri kuwa kiongozi bora hutokea kwa bahati tu au hakuna haja ya kujifunza jinsi ya kuwa kiongozi bora. Wewe kama mtu anayehitaji kusimamia na kuratibu shughuli mbalimbali ni lazima ufahamu sifa zinazomfanya mtu kuwa kiongozi bora ili uwe na mafaniko. Katika makala hii utaweza kufahamu sifa 10 zitakazokufanya kuwa kiongozi bora. 1. Uwazi Uwazi ni sifa muhimu inayomfanya mtu kuwa kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima awe wazi katika utendaji kazi wake. Uwapo kiongozi kuna siri za kazi lakini namna ya utendaji kazi hautakiwi uwe siri au usioeleweka kwa wale unaowaongoza. Kiongozi bora anatakiwa kuwa na mpangilio mzuri na unaoeleweka w...