Maendeleo Binafsi Archives - Page 2 of 3 - Fahamu Hili
Wednesday, October 23Maarifa Bila Kikomo

Maendeleo Binafsi

Sababu 11 za Kwanini Watu Hawakupendi

Sababu 11 za Kwanini Watu Hawakupendi

Maendeleo Binafsi
Kuna baadhi ya watu wanapendwa sana kwenye jamii au mazingira yanayowazunguka, kwa ujumla tunaweza kusema wanapendwa takriban na watu wote. Lakini wapo wengine wasiopendwa kabisa, na hata kama wanapendwa, basi wanapendwa na watu wachache sana. Kuishi katika jamii inayokupenda kunakufanya kuwa mwenye furaha na ufanisi katika yale unayoyafanya. Wapo baadhi ya watu wanatambua kuwa hawapendwi, lakini hawajui sababu za tatizo hilo wala njia ya kulitatua. Ikiwa unataka kufahamu kwanini baadhi ya watu hawakupendi, basi fahamu sababu 11 zinazosababisha watu wasikupende. 1. Siyo msikivu Kama unavyopenda kusikilizwa, ndivyo na watu wengine wanavyopenda kusikilizwa. Ikiwa huna muda wa kusikiliza mawazo au matatizo ya watu wengine, nao pia hawatakuwa na muda wa kupenda kukusikiliza. Epuka tabia z...
Mbinu 9 za Kuacha Tabia Mbaya

Mbinu 9 za Kuacha Tabia Mbaya

Maendeleo Binafsi
  Tabia mbaya zimekuwa zikiwakabili na kuwatesa watu wengi. Haipingiki kuwa tabia mbaya huwazuia watu wengi kufikia malengo yao kwenye maisha. Tabia kama vile uvivu, ulevi, madawa ya kulevya, uzinzi, matumizi mabaya ya pesa, ugomvi, kupoteza muda, n.k. ni baadhi tu ya tabia ambazo zimekuwa zikiwaathiri watu wengi. Hata hivyo, waathiriwa wa tabia hizi wengi hutamani kuziacha, lakini wanashindwa kufahamu waanzie wapi na watumie njia gani ili kuacha tabia hizo. Ikiwa basi unataka kuboresha maisha yako, karibu nikufahamishe mbinu 9 unazoweza kuzitumia ili kuacha tabia mbaya. 1. Jikumbushe na tafakari madhara ya tabia hiyo Ili kupata motisha wa kuacha tabia mbaya, kila mara jikumbushe na tafakari madhara unayoyapata kutokana na tabia hiyo. Kwa mfano ikiwa ni tabia ya u...
Sababu 10 za Kwanini Baadhi ya Watu Kamwe Hawatafanikiwa

Sababu 10 za Kwanini Baadhi ya Watu Kamwe Hawatafanikiwa

Maendeleo Binafsi
Kila mtu anatamani kufanikiwa, lakini siyo wote wanatimiza lengo hili. Ni wazi kuwa hakuna njia ya mkato ya kufika kwenye kitu kizuri. Ukiwachunguza sana watu waliofanikiwa, utagundua kuwa kuna tabia au mambo kadhaa yanayoshabihiana kati yao. Pia ukiwachunguza watu walioshindwa au ambao hawajafanikiwa, utabaini pia kuna tabia au mambo kadhaa yanayofanana kati yao. Je unatamani kufanikiwa? Basi fahamu sababu 10 zinazowafanya baadhi ya watu kamwe wasifanikiwe kwenye maisha yao. 1. Kutokujali muda Mafanikio yamefugwa kwenye muda. Ili mtu aweze kufanikiwa ni lazima ajifunze kutumia muda wake vyema. Watu wasiofanikiwa hawana mipaka; huchelewa kila mahali, pia hawathamini muda wa wengine. Hawana vipaumbele wala muda wa kuweka malengo na vipaumbele kwenye maisha yao; wao huishi tu ...
Njia 7 Bora za Kushinda au Kukabiliana na Hofu

Njia 7 Bora za Kushinda au Kukabiliana na Hofu

Maendeleo Binafsi
Watu wengi wanakabiliwa na kuathiriwa na hofu katika maisha yao kwa namna moja au nyingine. Hofu hizi zinaweza kusababishwa na mazingira, mtu, kitu au hata sababu za kisaikolojia. Hofu isiposhughulikiwa kwenye maisha inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya mtu husika. Wengi wanatamani kukabiliana na hofu lakini bado hawajui namna ya kukabili hofu zinazowakumba. Soma pia: Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu. Je uko tayari kushinda hofu sasa? Karibu nikushirikishe njia 7 ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hofu maishani mwako. 1. Punguza au ondoa mawazo na imani potofu Wakati mwingine watu wanapata hofu kutokana na imani au fikra potofu pekee. Kwa mfano unaogopa kinyonga kwa sababu umesikia kuwa kikikugusa utatokwa na ngozi au kufa; je una uhakika juu ...
Mambo 25 Unayoweza Kujifunza Kutokana na Makosa

Mambo 25 Unayoweza Kujifunza Kutokana na Makosa

Maendeleo Binafsi
Je wewe unapenda kufanya makosa? Mimi binafsi sipendi kufanya makosa. Ingawa watu wengi wamekuwa wakijaribu kujitahidi kuepuka makosa; bado wamejikuta wakiendelea kufanya makosa. Ni wazi kuwa makosa hayaepukiki kwenye maisha ya kila siku ya binadamu. Kutokana na sababu za kibinadamu, maamuzi na matendo tunayoyafanya yana mapungufu mbalimbali; hivyo haiwezekani kuepuka makosa. Kama haiwezekani  kuepuka makosa sasa tunafanyaje? Jibu ni wazi kabisa kuwa tunajifunza kutokana na makosa hayo ili tuyaepuke au tuboreshe mambo mbalimbali mbeleni. Karibu nikufahamishe mambo 25 ambayo unaweza kujifunza kutokana na makosa mbalimbali unayoyafanya kila mara maishani mwako. 1. Hutuonyesha vitu na mambo tusiyoyafahamu Ni wazi kuwa makosa mengine hutokea kwa kufanya vitu au maamuzi tu
Mambo 15 ya Kufanya ili Kuwa Bora Zaidi

Mambo 15 ya Kufanya ili Kuwa Bora Zaidi

Maendeleo Binafsi
Kama mtu mwenye shauku kubwa ya maendeleo binafsi, kila siku huwa nachunguza njia bora za kunifanya niwe bora zaidi. Naamini wewe pia unapenda kuwa bora zaidi ili uongeze tija na ufanisi wako. Karibu nikufahamishe mambo 15 ambayo unaweza kuyafanya kuanzia sasa ili uweze kuwa bora zaidi. 1. Soma vitabu Vitabu ni chanzo kikubwa cha hekima; Kadri unavyosoma vitabu ndivyo unavyozidi kupata hekima hii. Kupitia vitabu unaweza kujifunza mambo mbali mbali kama vile: Njia za kukabiliana na matatizo mbalimbali. Njia za kufanya mambo mbalimbali kwa ufanisi. Jinsi ya kuboresha maisha yako. Hamasa kutoka kwa waliofanikiwa n.k. Maarifa mapya usiyoyajua. Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo unaweza kujifunza au kuyapata kutoka kwenye vitabu. Hivyo ikiwa unataka kuwa bora zaid...
Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa

Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa

Maendeleo Binafsi
Ikiwa wewe ni mjasiriamali unayeanza au umeajiriwa sehemu fulani, kuna tabia ambazo unatakiwa kuzifahamu na kuzifanya ili uwe na mafanikio. Watu wengi hufikiri kuwa mafanikio ni jambo linalotokea kwa bahati tu; lakini mafanikio ni matokeo ya tabia au mikakati inayofanywa mara kwa mara. Hivi leo kuna watu tunaowachukulia kuwa wamefanikiwa; watu hawa wana tabia fulani za msingi zinazofanana. Karibu nikufahamishe tabia 10 za watu waliofanikiwa ambazo unaweza kujifunza ili uweze kufanikiwa. 1. Wana mipango Watu waliofanikiwa hawafanyi kazi bila mipango madhubuti. Watu hawa hupanga mipango mbalimbali wanayotakiwa kuitekeleza; mwishoni hukagua kama mipango yao wameitekeleza jinsi ipasavyo. Ni muhimu kujifunza tabia hii ya kujiwekea mipango na kufanya mambo kulingana na mipango husika bi...
Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani

Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani

Maendeleo Binafsi
Kabla hujakamilisha chochote maishani, ni lazima ufahamu unahitaji nini. Ni lazima ukae chini utafakari kama kile unachokifanya kina thamani kwako; ikiwa hakina thamani, basi tenga muda ujiwekee malengo yenye maana kwako. Kujiwekea malengo maishani kuna umuhimu mkubwa kwani hutufanya tujikite sawasawa kwenye kila tunachokifanya. Je uko tayari kuweka malengo? Karibu nikufahamishe faida 10 utakazozipata ikiwa utajiwekea malengo maishani mwako. 1. Hukupa mwongozo Awali ya yote, malengo hukupa mwongozo na mwelekeo maishani mwako. Malengo hukuwezesha kubaini kitu unachokilenga, na hukufanya uelekeze nguvu zako kwenye kitu husika. Badala ya kushika hiki na kile au kuwa huyu na yule, malengo yatakuwezesha kufahamu unatakiwa kufanya nini au kuwa nani. 2. Hukuwezesha kufanya...
Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kwenye Maisha ya Watoto

Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kwenye Maisha ya Watoto

Maendeleo Binafsi
Ingawa watu wengine huwachukulia watoto kama watu wasiofaa, watoto ni malaika wa kweli wanaoweza kutufundisha jinsi ya kuishi maisha mazuri. Ingawa wakati mwingine hawatambui wanachokuwa wakikifanya, lakini wanatupa nafasi ya kujifunza vitu vingi ambavyo tunavisahau tunapokuwa watu wazima. Kuna sababu ya kwanini watoto wanaitwa zawadi kutoka kwa Mungu. Wanatufundisha kuboresha maisha yetu, kuona vitu vizuri kwenye maisha pamoja na kujaa tabasamu kila siku. Ni wazi kuwa yapo mambo mengi mazuri na yenye manufaa makubwa ambayo kila mtu anaweza kujifunza kutoka kwa watoto; yafahamu mambo hayo sasa. 1. Kuwa na furaha Maisha ya watoto yamejaa furaha. Mara nyingi utawakuta watoto wakiimba, wakikimbia, wakiruka, wakitaniana kwa furaha bila wasiwasi. Hili limefanya maisha ya utoto kuwa saw...
Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako

Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako

Maendeleo Binafsi
Ni mara ngapi umejiambia kuwa kesho itakuwa siku nzuri na unatamani kuiona na kuiishi? Ni mara chache sana. Hofu na mashaka vimetawala na kuchukua nafasi katika kesho za watu wengi. Jambo zuri kwenye maisha ni kuwa una nafasi ya kutawala mambo mengi yanayotokea katika maisha yako. Kama kesho inafanana na leo hakuna maana; ikiwa leo ulikuwa na huzuni basi angalau kesho iwe na furaha. Hivyo kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya leo na kuhakikisha kuwa kesho inakuwa nzuri. Hapa kuna mambo 12 ambayo unayoweza kuyafanya na kuifanya kesho yako kuwa nzuri na yenye tija. 1. Panga kwa ajili ya kesho. George anatukumbusha  kuwa maandalizi bora ya kesho hufanywa leo. Kuwa na mpango wa kesho leo kutakuwezesha kufanya mambo kwa kutegemea mwongozo na mpangilio uliopo badala ya kuamka na kufan