Afya Archives - Page 2 of 2 - Fahamu Hili
Friday, April 26Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Afya

Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka

Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka

Afya
Kwanini ni muhimu kunywa maji? Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo. Ninawezaje kutumia maji kama tiba? Unaweza kutumia maji kama tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo: Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka. Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni. Kama huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza tar...
Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Afya
Watafiti wa afya nchini Marekani wamesema matumizi ya mafuta ya nazi si salama kwa afya kama ilivyo kwa nyama ya ng’ombe na siagi. Shirika la Moyo la Marekani (AHA), limeeleza kuwa mafuta yaliyoko kwenye nazi yanaweza kuongeza lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa AHA, wanadai kuwa kuna mafuta 82% katika nazi. Kuna zaidi ya 63% kwenye siagi, 50% kwenye nyama ya ng’ombe na 39% kwenye nyama ya nguruwe. Wataalamu hao wameongeza kuwa mafuta hayo yanaweza kusababisha lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu. Baadhi ya watu hudai kuwa ulaji wa mafuta ya nazi una manufaa kwa afya ya mlaji lakini AHA wamesema madai hayo hayajadhibitishwa. Wamependekeza kuwa, watu wajitahidi kupunguza kiasi cha mafuta yenye lehemu wanayoyatumia kila siku katik...