Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo - Fahamu Hili
Sunday, December 3Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Mjasiriamali

Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujipatia kipato. Hivi leo kuna wajasiriamali wengi waliofanikiwa na wengine hawajafanikiwa.

Kwa hakika wajasiriamali waliofanikiwa wanafahamu na wanaziishi sifa za wajasiriamali bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa mjasiriamali bora wakati una sifa za mwajiriwa.

Ili kuwa mjasiriamali ni lazima kuzifahamu na kuziishi sifa za mjasiriamali. Karibu nikufahamishe sifa 10 za mjasiriamali.

1. Mwenye malengo

Malengo ni mwongozo wa kukuwezesha kufanikisha jambo lolote. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Je umeamua kuwa mjasiriamali kwenye nini? Kwa ajili ya nini?

Malengo yatakuongoza ufanye nini, wapi lini na kwa ajili ya nini. Bila malengo utafanya mambo bila mwongozo wowote na ni vigumu kufanikiwa.

Soma pia: Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani

2. Nidhamu

Nidhamu ni sifa muhimu kwa mjasiriamali kwani itamtenga na mambo mengi yasiyokuwa na umuhimu. Ni lazima mjasiriamali awe na nidhamu ya maswala kama vile matumizi ya muda pamoja na pesa.

Kila mjasiriamali anapaswa kujinyima na kukataa vitu vyote ambavyo havimwezeshi kufikia malengo yake.

Soma pia: Faida 5 za Kusema “Hapana”

3. Ujasiri na uthubutu

Ujasiri na uthubutu ni sifa muhimu sana kwa mjasirimali ili aweze kutekeleza malengo yake. Ujasiriamali ni swala linalohitaji ujasiri na uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu hata kama kuna changamoto au hatari kadha wa kadha.

Huwezi kuwekeza pesa zako kwenye mradi au biashara yoyote kama hutokuwa na ujasiri na uthubutu. Ujasiri na uthubutu hautaruhusu hofu na mashaka ya kushindwa au kupata hasara vikutawale.

Soma pia: Tofauti 10 Kati ya Mwajiriwa na Mjasiriamali

4. Ubunifu

Ubunifu humtofautisha mjasiriamali mmoja na mwingine. Unahitaji ubunifu ili ubuni wazo la pekee ambalo litakupa matokeo mazuri. Wajasiriamali wengi hawana ubunifu ndiyo maana wanakwama.

Kwa mfano mjasiriamali mmoja akianzisha biashara ya kuuza maandazi, basi wengine 20 wataiga. Ni lazima mjasiriamali uwe na ubunifu utakaokuwezesha kufanya mambo yenye tija.

5. Uvumilivu

Kila jambo lina changamoto zake. Ujasiriamali una changamoto nyingi ambazo zinahitaji uvumilivu ili kuzimudu.

Hivyo basi, sifa ya kuwa na uvumilivu ni muhimu sana kwa kila mjasiriamali anayetaka kufanikiwa. Haijalishi umepata hasara au unakutana na changamoto nyingi kiasi gani, ni muhimu kuvumilia.

6. Bidii

“Mafanikio huja kwa wale ambao wanafanya bidii kubwa kuyatafuta.”

Henry David Thoreau

Bidii ni msingi wa kufanikiwa kwenye jambo au shughuli yoyote. Ni muhimu kukumbuka kuwa mjasiriamali ni mwajiri (boss) wake yeye mwenyewe. Hivyo ni muhimu kujituma na kufanya kazi kwa bidii bila kusukumwa na mtu yeyote.

7. Kupenda anachokifanya

“Fanya unachokipenda na pesa zitafuata.”

Marsha Sinetar

Watu waliofanikiwa sana duniani, wanafanya kile wanachokipenda. Unapofanya kile unachokipenda ni rahisi kufanikiwa kwani utakifanya kwa moyo, bidii pamoja na kutokata tamaa.

Kila mjasiriamali anatakiwa kuhakikisha kuwa anafanya kitu anachokipenda ili aweze kufikia malengo yake.

8. Kuishi na watu vizuri

Kila mjasiriamali anahitaji watu wengine ili kufanikisha malengo yake ya ujasiriamali. Kuishi na watu vizuri ni sifa muhimu kwa mjasiriamali kwani itamjengea soko zuri pamoja na nguvu kazi bora.

Hakuna haja ya kudharau au kutenga watu bila sababu. Usijenge chuki au ugomvi usiokuwa na sababu kati yako na watu wengine. Kumbuka kuwa watu ndio chanzo na msingi wako wa kupata faida.

Soma pia: Sababu 11 za Kwanini Watu Hawakupendi

9. Mwenye kupenda kujifunza na mtafiti

Katika swala zima la ujasiriamali, kutafiti na kupenda kujifunza ni tabia muhimu sana. Kila mjasiriamali anatakiwa kuwa na sifa hii ili aweze kujifunza na kutafiti njia na mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kumfanya mwenye tija zaidi.

Ni muhimu kukumbuka kuwa kuna wakati mjasiriamali anatakiwa kukaa chini kutafiti na kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatamwezesha kufanikiwa kwenye kile anachokifanya.

10. Kujifunza kutokana na makosa

Kama ulivyowahi kusikia mara kadhaa kuwa makosa ni shule muhimu kwa kila mtu, ndivyo ilivyo pia kwa mjasiriamali.

Mjasiriamali anapaswa kuwa na sifa ya kupenda kujifunza kutokana na makosa ili asiyarudie tena mbeleni na wala si kuyaogopa au kuyakimbia.

Kama uliwekeza pesa zako zikapotea, basi usiache ujasiriamali bali baini ni nini kilisababisha ukapoteza pesa zako ili ukiepuke mbeleni.

Soma pia: Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Neno la mwisho

Naamini ukiwachunguza vyema wajasiriamali waliofanikiwa utabaini kuwa wana tabia hizi zilizoelezwa hapa. Ni muhimu wewe kama mjasiriamali kuhakikisha unajitahidi kuwa na tabia zilizoelezwa hapa ili ufikie malengo yako.

Je wewe una tabia hizi? Je umejifunza kitu kwenye makala hii?

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Unaweza kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

4 13 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

21 Maoni
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Saighilu
Saighilu
5 years ago

Nimejifunza kitu hapa leo, mara yangu yakwanza kufatilia ukursa huu lakini nmependezwa nao sana.

Paul batevye
Paul batevye
Reply to  Kornelio Maanga
4 years ago

Mie naomba unisaidie namba yako ili tuongee vizr

Anko Musa
Anko Musa
5 years ago

Nafrahia na najifunza mengi sana kutoka kwenu

Siaga enock
Siaga enock
Reply to  Kornelio Maanga
4 years ago

Ubarikiwe

Salehegae
Salehegae
4 years ago

Asanteni kwa elimu hii mnayotupa

Nuni Hassan
Nuni Hassan
Reply to  Kornelio Maanga
3 years ago

Nimependa sana ufafanuzi mnaoutumia katika kuelisha mmenifanya nielewe vizuri na kubaki bila maswala. Asanteni kwa huduma yenu nzuri

Nuni Hassan
Nuni Hassan
3 years ago

Mpo vizuri kwel katika kutoa elimu

John kingu
John kingu
3 years ago

Kazi hii ni nzuri sana na mmeieleza kwa ustadi mkubwa ahsanteni sana

Mpine
Mpine
3 years ago

Kazi nzuri sana, napata maarifa mazur sana.

Isaya mboleka
Isaya mboleka
1 year ago

Yes

Pili
Pili
1 year ago

Saf sana

21
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x