Sababu 11 za Kwa nini Utumie WordPres Kwenye Blog Yako - Fahamu Hili
Tuesday, February 27Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Sababu 11 za Kwa nini Utumie WordPres Kwenye Blog Yako

Washirikishe Wengine Makala Hii:

WordPress

Mara unapotaka kutengeneza blog au tovuti, swali gumu linalokuja kichwani mwako ni njia, teknolojia, mfumo au programu ipi utakayoitumia kutengenezea tovuti au blog yako.

Kwa hakika kuna teknolojia mbalimbali zinazoweza kutumiwa kutengeneza blog na tovuti, WordPress kama Content Management System ni mojawapo.

WordPress ni programu ya bure (open source software) inayotumika kutengenezea tovuti na blogs ambayo unaweza kuisambaza, kuitumia au hata kuibadilisha bila kizuizi chochote. Unaweza kupakua WordPress na kuihost wewe mwenyewe au kwenye huduma yoyote nzuri ya kuhost website

Karibu ufuatilie makala hii nikufahamishe sababu 11 za msingi za kwanini utumie WordPress kwenye blog au tovuti yako.

1. WordPress inatumiwa na zaidi ya asilimia 25 ya tovuti

Zaidi ya asilimia 25 za tovuti kote ulimwenguni zinatumia programu ya WordPress kuendesha tovuti zao. Hii ina maana kuwa WordPress inaaminika na kukidhi mahitaji ya tovuti nyingi vyema.

2. WordPress inaweza kupanuliwa kwa urahisi

Kwa kutumia plugins mbalimbali unaweza kupanua programu ya WordPress ili kukidhi mahitaji yoyote ya blog yako. Ikilinganishwa na mifumo mingine ya kutawala maudhui (Content Management System – CMS), WordPress ina plugins nyingi zaidi.

3. Ina violezo (templates) vya kutosha

WordPress inaweza kubadiliwa muonekano wake kwa kutumia violezo vingi vilivyoko bila kuhitaji kuandika au kufahamu lugha za usanifu mtandao (Web programming languages).

Unaweza kupata mwonekano mzuri wa blog yako bila gharama au kupoteza muda.

4. Inaweza kutumika kwenye lugha mbalimbali

Kwa wale wanaotaka kutengeneza blog au tovuti za lugha zaidi ya moja ni muhimu kuchagua programu ambayo ina uwezo wa kuhimili lugha zaidi ya moja.

WordPress imeshatafsiriwa kwenye lugha zaidi ya 169 pamoja na plugins zake nyingi.

5. Inatumiwa na kampuni kubwa

Programu ya WordPress inatumiwa na kampuni na taasisi kubwa duniani kama vile Sony Music, Mercedes Benz, BBC America, Reuters, Chuo Kikuu cha Harvard na Chuo Kikuu cha Washington.

Hii ni kudhihirisha kuwa WordPress inaweza kubeba tovuti kubwa bila tatizo lolote.

6. WordPress ni gharama nafuu

Kwa kuwa WordPress ni ya bure, hili linaifanya kuwa ni programu ya kutengenezea tovuti au blog ya gharama nafuu.

Unakachohitajika kulipia ni anwani mtandao pamoja na huduma ya webhost tu.

7. Ni rahisi kupata msaada

Kutokana na umaarufu huu wa WordPress, upatapo tatizo ni rahisi kupata utatuzi wa tatizo lako kwenye mtandao kwa urahisi kabisa.

Unaweza kutembelea pia ukurasa rasmi wa WordPress ili kupata usaidizi, WordPress Support.

8. WordPress imeboreshwa kwa ajili ya injini pekuzi

Uboreshaji wa injini pekuzi (Search Engine Optimization SEO) ni swala muhimu kwenye tovuti au blog yoyote. WordPress imetengenezwa kwa namna ambayo inakidhi vigezo vya uboreshaji wa injini pekuzi.

Kumbuka tovuti au blog yako haiwezi kuwafikia walengwa vyema kama haitafanyiwa uboreshaji wa injini pekuzi sawasawa.

9. Ni salama

WordPress ni programu inayoaminika na salama kwa ajili ya tovuti au blog yako. Hata hivyo kuna mambo unayotakiwa kuyafanya ili kuhakikisha usalama huo:

  • Fanya masasisho kwa wakati.
  • Pakua na weka plugins zinazoaminika.
  • Weka violezo vinavyoaminika.
  • Tumia web host bora na salama.

Soma pia: Mambo 9 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Web Host

10. Ina kasi nzuri

Kasi nzuri ni swala muhimu sana kwenye tovuti au blog yoyote ili kutokuathiri watumiaji pamoja na injini pekuzi. Wordpres imetengenezwa kwa njia ambayo haiathiri kasi ya utendaji kazi wa tovuti au blog yako labda kama utakuwa umeongeza plugins mbaya wewe mwenyewe.

11. Inaweza kuunganishwa na huduma mbalimbali

Kwa wale ambao ni wasanifu mtandao wanafahamu kuhusu thirdpart application; WordPress inaweza kuungwanishwa na program au huduma nyingine kwa njia ya API bila shida.

Hitimisho

Je kutokana na makala hii umevutiwa kutumia WordPress? Je ina sifa na vigezo unavyovihitaji? Jambo muhimu katika kuchagua programu ya kutumia kwenye tovuti au blog yako ni kubainisha mahitaji yako kisha kukagua kama programu husika inakidhi mahitaji hayo.

Je una swali au unahitaji msaada wowote? Tafadhali tuandikie maoni na maswali yako hapo chini. Unaweza pia kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x