Fahamu Hili Archives - Page 16 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka

Ujasiriamali
Kuanza biashara kutoka kiwango cha sifuri siyo kazi rahisi. Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni. Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua. Unapokuwa kwenye biashara ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako; ili ujitahidi kuyaepuka ama kuyapunguza kadri iwezekanavyo. Ni dhahiri kuwa wajasiriamali wengi wamekwama kutokana na kupuuzia au kutofahamu makosa haya 15 ambayo hata wewe unatakiwa kuyafahamu na kuyaepuka. 1.Kujifanya unafahamu kila kitu Usijifanye unajua kila kitu, hasa kama ndiyo umeingia kwenye ulimwengu wa kibiashara. Kwanini? Kwa sababu kuendesha biashara ni kujifunza na kupata uzoefu. Jitahidi ku...
Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini

Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini

Afya
Asilimia kubwa ya maradhi yanayowasumbua watu hivi leo yanatokana na sumu zilizopo katika miili yao. Inawezekana umewahi kusikia mambo mengi kuhusu sumu kwenye mwili, lakini hufahamu chazo halisi cha sumu hizi. Mabadiliko ya mazingira na mtindo wa maisha hupelekea kutengenezeka na kuingia kwa sumu nyingi ndani ya mwili wa binadamu. Sumu hizi hutokana na vyakula, vinywaji na hata mazingira tunayoishi. Sumu hizi huweza kuleta madhara makubwa mwilini kama vile kushindwa kufanya kazi kwa viungo vya mwili na hata aina mbalimbali za saratani. Ni vyema ukafahamu njia bora za kuondoa sumu mwilini mwako ambazo unaweza kuzifanya wewe mwenyewe bila gharama za ziada. 1. Kula vyakula vya asili Hivi leo watu hufikiri kula vyakula vya asili ni kupitwa na wakati. Wengi husifu vyakula vya vi...
Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema

Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema

Kipato, Tija
Je, huwa unajisikia vibaya unapohitaji pesa kwa ajili ya matumizi yako lakini unajikuta mifuko yako ni mitupu? Haijalishi unapata pesa kiasi gani, swala la matumizi mazuri ya pesa ni jambo muhimu; hili litakuwezesha kuwa na kitu wakati wa uhitaji. Watu wengi wanapata pesa lakini si wote wanaoweza kuzitumia vyema. Wengi hujikuta wakizitumia kwenye mambo na mipango ambayo mwishoni haiwaletei tija katika maisha yao. Naamini ungependa kuwa na matumizi mazuri ya pesa; sasa fahamu njia 10 zitakazokuwezesha kutumia pesa vyema. 1. Weka bajeti Ni rahisi kusikia watu wakilalamikia bajeti za serekali na kuzikosoa lakini wao wenyewe hawana bajeti zao binafsi. Unawezaje kukosoa bajeti ya serekali wakati ya kwako mwenyewe imekushinda? Fikiri tofauti; tambua umuhimu na jinsi ya kujiwekea baje...
Njia 8 Rahisi za Kupunguza Matumizi ya Umeme

Njia 8 Rahisi za Kupunguza Matumizi ya Umeme

Nyumba na Makazi
Matumizi hayaepukiki kwenye maisha lakini kubana matumizi inawezekana. Yapo mambo mengi ambayo hugarimu fedha ili kuyamudu yakiwemo huduma kama maji, umeme, gesi na mafuta. Ni dhahiri kuwa ili kupunguza ugumu na changamoto za maisha ni vyema kujifunza namna ya kutumia vitu vyema. Unaweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingepotea kwa kulipia gharama zisizo na sababu za matumizi ya umeme. Hivyo fahamu njia 8 rahisi za kupunguza matumizi ya umeme. 1. Zima taa na vifaa visivyokuwa na uhitaji Mara nyingi umeme mwingi hupotea kutokana na kuacha vifaa mbalimbali vikiwa vimewashwa bila sababu. Si jambo la kustajabisha watu kusahau taa za nje ya nyumba hadi saa sita mchana; au hata kuacha vifaa kama vile redio, televisheni au kompyuta vikiwa vimewashwa mchana au usiku kucha bila sababu ya m...
Nembo/Logo za Kibiashara Zilizobeba Maana Usizozijua

Nembo/Logo za Kibiashara Zilizobeba Maana Usizozijua

Biashara na Uchumi
Kama unavyojua nembo au logo ya kibiashara ina nafasi kubwa katika utambulisho wa kampuni. Nembo iliyobuniwa vizuri inaweza kuwafanya watu wengi kutambua huduma au bidhaa unayotoa. Hii ndiyo sababu logo nyingi hupitia usanifu na maboresho mbalimbali ili kuhakikisha zinawakilisha kampuni au biashara vyema. Hata hivyo, zipo logo zilizofanikiwa kufanya vizuri  wakati nyingine hazijafanikiwa. Kwa zile zilizofanikiwa unaweza kushangaa ni kwa namna gani wabunifu wake wameweza kuficha maana fulani muhimu kuhusu kampuni husika. Fahamuhili kwa kutambua umuhimu wa utambulisho katika biashara au kampuni, tumekuletea orodha hii ya nembo zaidi ya 10 pamoja na maana zilizojificha ndani yake. Tunaamini makala hii itakupa mwangaza muhimu pale utakapokuwa unatengeneza logo yako. Soma pia: Mamb...
Tovuti 15 za Kufanya Kazi Kwenye Mtandao

Tovuti 15 za Kufanya Kazi Kwenye Mtandao

Kipato
Mara nyingi milango ya matumizi ya fedha ni mingi kuliko milango ya mapato. Hivyo ni vyema kufikiri namna ya kuongeza milango mingi zaidi ya kipato. Inawezekana wewe ni mwajiriwa, mjasiriamali, mwanafunzi au hujaajiriwa bado; ni vyema ukafahamu kuwa zipo kazi zinazopatikana kwenye mtandao ambazo zinaweza kukuzalishia kipato kizuri. Hakuna sababu ya kukaa na maarifa au ujuzi ulionao ambao ungeweza kuutoa na ukajipatia kipato. Kufanya kazi kwa njia ya mtandao ni rahisi zaidi na kunakupa uhuru mkubwa wa mazingira ya kufanyia kazi. Fahamu kuwa unaweza kupata kazi nzuri zenye kipato kizuri katika tovuti 15 nilizoziorodhesha hapa. Soma Pia: Mambo 5 ya Kufahamu Kabla ya Kulenga Kupata Pesa kupita Kazi za Kwenye Mtandao. 1. Upwork Upwork ni tovuti ambayo awali ilifahamika kama Odesk, k...
Kazi za Sanaa Zitakazokushangaza

Kazi za Sanaa Zitakazokushangaza

Maarifa
Kila mtu ana kipawa chake alichopewa. Inawezekana ni kuimba, kuchora, kucheza mchezo fulani n.k. Lakini wapo watu ambao wamevitumia vipawa vyao kwa kiwango kinachostaajabisha wengi. Wapo waliofanya kazi kama vile ubunifu wa picha na maumbo kiasi cha kumfanya mtazamaji kushindwa kutofautisha kitu kilichosanifiwa na halisi. Fuatilia ukurasa huu mara kwa  mara kwani nitakuwa nikiweka kazi mbalimbali za kushangaza zilizofanywa na wabunifu mbalimbali. Anza kwa kutazama hizi zifuatazo hapo chini; pia kama una maoni, ushauri, swali, au kazi ambayo ungependa ionyeshwe hapa basi usisite kutujulisha. Karibu. Kumbuka hapa hatuonyeshi kazi feki zitokanazo na uhariri wa kompyuta! Ikumbukwe kuwa umiliki wa kazi hizi utabaki kuwa wa wamiliki na si vinginevyo. Ikiwa msanii hapendi kazi yake ionekane...
Kitu Muhimu Mark Zuckerberg Alichokijenga Harvard

Kitu Muhimu Mark Zuckerberg Alichokijenga Harvard

Hamasa
Mark Zuckerberg akiwa chuoni Harvard Ukimuuliza Mark Zuckerberg juu ya alichokikamilisha alipokuwa akisoma chuoni Harvard jibu lake linaweza kukushangaza. Unaweza kufikiri ni Facemash ambayo baadaye ilikuja kuwa Facebook lakini siyo. "Priscilla ni mtu muhimu zaidi katika maisha yangu, na jambo muhimu zaidi nililojenga wakati wangu hapa." Zuckerberg alisema hayo kuhusu mke wake wakati wa hotuba ya ufunguzi wa mahafali huko kwenye chuo cha Harvard mwaka huu. Mkurugenzi huyu mkuu wa Facebook mwenye miaka 33 alitumia kiasi kikubwa cha muda wake wakati wa hotuba hiyo akionyesha jinsi alivyokutana na Priscilla Chan, daktari wa watoto ambaye hatimaye walifunga ndoa mwaka 2012. Mark Zuckerberg na mke wake Priscilla Chan Zuckerberg alikutana na Chan kwenye sherehe na akampenda. Chan ...
Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora

Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora

Tija
Hakuna uandishi bora au andiko bora pasipo uhariri bora. Hivyo uandishi mzuri hauwezi kutengwa na uhariri bora. Ni dhahiri kuwa makala au andiko lililohaririwa vyema na kwa ustadi wa hali ya juu litakubalika na kupendwa na wasomaji wengi zaidi. Watu wengi wamekuwa wakitamani kuandika matini zilizohaririwa vyema lakini wamekuwa wakikwama juu ya ni njia gani wanaweza kuwa wahariri bora. Pengine umekuwa ukitamani kunufaika kupitia kazi ya uhariri lakini hujui ufanyeje ili uweze kuwa mhariri bora. Fuatana nami katika makala hii nikueleze njia 10 zitakazokufanya kuwa mhariri bora. 1. Jifunze sarufi ya lugha na kanuni za uandishi Uhariri ni taaluma kama ilivyo kwa taaluma nyingine. Hivyo ili uwe mhariri bora basi huna budi kujifunza kanuni za sarufi ya lugha husika pamoja na kanuni za uand...
Mbinu 7 za Kuwa Mwandishi Bora

Mbinu 7 za Kuwa Mwandishi Bora

Tija
Kama umewahi kuwa na ndoto au matamanio ya kuwa mwandishi mkubwa kama vile Wole Soyinka, Ngũgĩ wa Thiong'o au pengine hata kuwa mwandishi bora kitaaluma au katika blogu yako, basi ni vyema ukajifunza namna ya kuwa mwandishi bora. Kuwa mwandishi bora si jambo la mzaha; ni jambo linalalowezekana ikiwa utaweka jitihada stahiki. Ni dhahiri kuwa jitihada utakazozifanya hazitakuwa bure kwani hivi leo kuna fursa mabalimbali zinazohitaji watu wenye uwezo mzuri wa uandishi. Hivyo basi, fuatana nami nikujuze mbinu zitakazokuwezesha kuwa mwandishi bora kabisa na kufikia malengo yako ya mbeleni. 1. Soma maandiko bora Ni dhahiri kuwa ukihitaji kufahamu nini mana ya uandishi bora ni lazima usome maandiko bora yaliyoandikwa na waandishi mahiri. Soma maandiko bora kadri uwezavyo kwani utaji...