
Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta
Kuandika kwa kasi na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta kuna manufaa mengi kama vile kuweza kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi, kuweza kuandika mambo mbalimbali kwa kutumia kompyuta na hata sifa ya kukuwezesha kupata kazi mbalimbali. Hivyo, najua unatamani kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta; lakini tatizo bado hujaweza kuacha kasi ya kudonoa na kuweza kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi. Karibu ufahamu njia 5 ambazo unaweza kuzitumia ili kuboresha uwezo wako wa kuandika kwa kutumia kompyuta.
1. Elewa na tumia baobonye (keyboard) vyema
Ili uweze kuongeza kasi yako ya kuandika pamoja na usahihi ni lazima uelewe baobonye vyema na kuitumia vyema. Zingatia haya yafuatayo: Elewa mpangilio wa vitufe kwenye baobonye.
Panga vidole kulingana na vitufe sta...