
Faida 8 za Kuweka Akiba Unazopaswa Kuzifahamu
Kuweka akiba ni kanuni mojawapo ya matumizi mazuri ya pesa. Hata hivyo kutokana na watu wengi kutokuwa na matumizi mazuri ya pesa, bado wengi wanashindwa kuweka akiba. Baadhi ya watu hufikiri kuwa ili uweze kuweka akiba ni lazima uwe na pesa nyingi, lakini ukweli ni kuwa kuweka akiba ni maamuzi tu na siyo kuwa na pesa nyingi. Ikiwa umekuwa ukipuuza suala la kuweka akiba na kuliona kuwa halina maana, basi fahamu faida 8 za kuweka akiba.
1. Uhuru wa kifedha
Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani. Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye swala la uhuru wa kifedha, ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi. Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kuji...










