
China Kujenga “Mji Msitu” Ambao Utakuwa na Mamilioni ya Mimea na Miti 40,000
China kujenga “mji msitu” ambao utakuwa na mamilioni ya mimea na miti 40,000. Kazi hii inatarajiwa kutekelezwa kwenye Mji Msitu wa Liuzhou ulioko katika milima ya kusini mwa Guangxi kabla ya 2020. Mji huu uliobuniwa na msanifu majengo Stefano Boeri unatekelezwa sasa, ambapo nyumba, ofisi, shule na hosipitali zitafunikwa kabisa na miti na mimea mingine. Mjii huu unatarajiwa kuchukua eneo la hekta 175, na utakapokamilika utaweza kuchukua watu takriban 30,000. Mji huo utakapokamilika utatumia usafiri wa treni ya umeme kutoka Liuzhou. Mji huo pia utatumia nishaji ya joto ardhi (geothemal) kwa matumizi ya ndani nyumba pamoja na umeme jua (solar). Wanaamini kuwa kupanda miti zaidi kutanyonya tani 10,000 za hewa ukaa (C02) na tani 75 za hewa chafuzi nyingine, wakati huo ikizalisha ta...