Fahamu Hili Archives - Page 14 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Mambo 18 ya Kushangaza Kuhusu Intaneti Usiyoyajua

Maarifa, Teknolojia
Hivi leo kuna mambo mengi kuhusu intaneti, lakini hapa nitakuonyesha baadhi ya mambo ambayo naamini yatakuvutia na kukushangaza. Historia ya intaneti inaanzia miaka ya 1950 ikienda sambamba na maendeleo ya kompyuta. Ni wazi kuwa, ulimwengu wa intaneti wa leo ulianzwa na mwanasayansi wa kompyuta wa Uingereza Tim Berners-Lee. Kuundwa kwa intaneti yake ya kwanza, moja kwa moja kulibadili ulimwengu, vyombo vya habari, mahusiano, burudani na mambo mengine mengi. Tunapotazama intaneti leo, ni wazi kuwa tunaona mambo mengi ambayo intaneti imepitia tokea kuanzishwa kwake hadi hivi leo. Karibu ufuatilie makala hii ili ufahamu mambo 18 ya kushangaza kuhusu intaneti usiyoyajua. 1. Tovuti ya kwanza bado ipo Tovuti ya kwanza kutengenezwa bado ipo na inafanya kazi hadi leo. Jambo pekee ni ku...
Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao

Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao

Biashara na Uchumi
Kufanya biashara kwenye mtandao ni jambo lenye faida na changamoto zake. Unaweza ukawa na bidhaa nzuri sana, lakini ukumbuke kuwa kila siku kunaanzishwa tovuti za kuuza bidhaa mtandaoni. Haijalishi kuwa wewe ni muuzaji wa bidhaa wa siku nyingi au wa karibuni, ni wazi kuwa utakutana na changamoto kadha wa kadha. Sasa utafanyaje? Hakuna jibu rahisi, bali ni wazi kuwa makosa unayofanya wakati wa kuendesha biashara kwenye mtandao, ndiyo yanayokugharimu wewe na mapato yako. Yafuatayo ni makosa 8 ambayo unatakiwa kufanya juu chini ili kuhakikisha unayaepuka unapofanya biashara kwenye mtandao. 1. Kukosa kitengo cha huduma kwa wateja Ni rahisi mtu kukaa dukani kwake siku nzima ili kuwahudumia wateja; lakini unaona hakuna umuhimu wa kukaa karibu na wateja wake wa kwenye mtandao. Kumbuka ha...
Mambo 20 Yakushukuru Kwa Ajili Yake Kwenye Maisha

Mambo 20 Yakushukuru Kwa Ajili Yake Kwenye Maisha

Hamasa
Wakati mwingine tunatazama tu mambo ambayo hatuna kwenye maisha, kuliko yale tuliyo nayo. Mara nyingi huwa hatutambui umuhimu wa kitu hadi pale tunapokikosa. Niwazi kuwa wapo watu wanaotafuta vile tunavyoviona ni vidogo lakini hawavipati. Ni muhimu kutenga muda wa kukumbuka yale mambo yote ambayo tunapaswa kushukuru kwa ajili yake. Kama una chochote kati ya hivi basi yakupasa kushukuru. Afya njema Mara nyingi hatutambui kuwa na afya njema pekee ni jambo muhimu na kubwa sana. Kuna wengi wanaotamani kuwa na afya kama ya kwako lakini hawana; hivyo yakupasa kushukuru kwa afya njema. Pesa ulizonazo Unaweza kufikiri kiasi cha pesa ulizonazo ni kidogo sana hivyo hauhitaji kushukuru. Kuna mahali pengine wewe ni tajiri mkubwa sana. Wapo wasiokuwa na pesa wala chochote kile wanachow...
Njia 4 za Kujilinda Unapofanya Miamala au Manunuzi Kwenye Mtandao

Njia 4 za Kujilinda Unapofanya Miamala au Manunuzi Kwenye Mtandao

Teknolojia
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari mawasiliano (TEHAMA), mfumo wa biashara pia umebadilika. Hivi leo ni rahisi kutuma na kupokea pesa, kuuza au hata kununua bidhaa kwa njia ya mtandao. Watu wengi hupenda kufanya manunuzi na mauzo ya bidhaa kwenye mtandao kutokana na urahisi wa upatikanaji wa bidhaa na huduma kupitia mtandao. Pamoja na nafasi hii kubwa ya mtandao katika maswala yanayohusu fedha, zipo changamoto mbalimbali zinazoandamana na miamala na manunuzi ya kwenye mtandao. Fahamu jinsi unavyoweza kujilinda unapofanya miamala au manunuzi mbalimbali kupitia mtandao. 1. Tumia kinga-virusi (antivirus) bora Mtandao wa intanet ni chanzo kikubwa cha virusi na wadukuzi. Hivyo ni vyema ukatumia programu madhubuti kwa ajili ya kukukinga na virusi na wadukuzi mara unapofanya manu...
Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa

Sababu 13 za Kwa Nini Biashara Nyingi Hufa

Biashara na Uchumi
Hakuna mtu anayeanzisha biashara akitegemea ife, lakini wakati mwingine hili hutokea. Utafiti umebaini kuwa biashara na kampuni nyingi hufa ndani ya kipindi cha miaka miwili hadi mitano tangu kuanzishwa kwake. Kufa kwa biashara siyo jambo zuri, ni wazi kuwa kila mtu nayefanya biashara atatamani kufanya juu chini ili ainusuru biashara yake isife. Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha biashara mbalimbali kufa. Fahamu sababu 13 zinazosababisha biashara nyingi kufa pamoja na jinsi ya kuziepuka. 1. Mipango duni Ili ufanikiwe katika biashara unahitaji mpango mzuri wa biashara. Biashara nyingi zinazoanzishwa Afrika hazina mipango madhubuti ya kibiashara inayoonyesha maswala kama vile muundo wa utawala, mtaji, mikakati au mipango ya mauzo, n.k Biashara nyingi pia hukosa lengo; jambo a...
Njia 8 za Kutambua Bidhaa Feki au Bandia

Njia 8 za Kutambua Bidhaa Feki au Bandia

Tija
Mara nyingi tunanunua vitu na bidhaa mbalimbali bila kuzifahamu au kuzichunguza vyema. Hili limepelekea watu wengi kununua bidhaa zisizofaa kwao au zenye madhara kwenye afya zao. Kutokana na ukosefu wa elimu pamoja na kuishi kwa mazoea, watu wengi hawajui wala hawachunguzi vyema bidhaa wanazozinunua ili kuhakikisha ubora wake. Madhara ya kutumia bidhaa feki au bandia: Matatizo ya kiafya kama vile saratani na ulemavu. Upotevu wa fedha. Ajali (Milipuko, shoti ya umeme, n.k). Huathiri uchumi. Ni wazi kuwa yapo madhara mengi yatokanayo na matumizi ya bidhaa feki. Hivyo ni vyema ukafahamu njia za kubaini bidhaa hizi. 1. Ofa na matangazo yasiyo ya kawaida Wahenga walisema “Chema chajiuza kibaya chajitembeza”; ni vyema ukawa makini na bidhaa zenye punguzo kubwa la bei ku...
Makosa 8 ya Kuepuka Kabla na Wakati wa Kujenga Nyumba

Makosa 8 ya Kuepuka Kabla na Wakati wa Kujenga Nyumba

Nyumba na Makazi
Nyumba ni hitaji muhimu kwa watu wote. Kila mmoja anatamani na ana ndoto za kununua au kujenga nyumba nzuri na ya kisasa. Ni kweli kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji rasilimali nyingi hasa fedha. Pamoja na gharama hizi za ujenzi wa nyumba bado watu wengi wamekuwa wakishindwa kupata nyumba nzuri huku wakiwa tayari wamepoteza kiasi kikubwa cha pesa. Ni wazi kuwa yapo makosa mbalimbali yanayosababisha hali hii yakiwemo yale ya ukosefu wa elimu pamoja na uzembe wa aina mbalimbali. Karibu ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu makosa 8 unayoweza kuyaepuka wakati wa kujenga nyumba ili hatimaye uwe na nyumba bora. 1. Kutozingatia kanuni za kununua kiwanja Watu wengi hawafahamu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wanaponunua kiwanja. Hivyo hujikuta wakiingia katika matatizo mbalimbali kama vile ku...
Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Kiwanja au Ardhi

Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Kiwanja au Ardhi

Nyumba na Makazi
Ardhi ni rasilimali muhimu ambayo kila mtu anaihitaji kwa namna moja au nyingine. Watu wengi hununua ardhi kwa ajili ya kufanyia shughuli mbalimbali kama vile ujenzi na kilimo. Pamoja na umuhimu huu mkubwa wa ardhi bado watu wengi wanakumbana na changamoto mbalimbali katika maswala yanayohusu kununua na kumiliki ardhi. Wengi hujikuta wakinyang’anywa ardhi zao, kuharibiwa mali, au wakiingia kwenye migogoro mikubwa ya kisheria. Ni wazi kuwa zipo sababu mbalimbali zinazosababisha matatizo haya. Fuatilia makala hii kwa makini ili uweze kufahamu mambo 10 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kununua kiwanja au ardhi. 1. Ona kiwanja husika mwenyewe Ni vyema ukafika kwenye eneo la kiwanja husika na kukiona wewe mwenyewe kama kinakuridhisha na kukufaa kwa mahitaji yako. Fahamu mipaka, na ...
Aina 9 za Vyakula  Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona

Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona

Mtindo wa Maisha
Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti. Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona. 1.Samaki Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3. 2.Mboga za majani Watu ...
Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kwenye Maisha ya Watoto

Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kwenye Maisha ya Watoto

Maendeleo Binafsi
Ingawa watu wengine huwachukulia watoto kama watu wasiofaa, watoto ni malaika wa kweli wanaoweza kutufundisha jinsi ya kuishi maisha mazuri. Ingawa wakati mwingine hawatambui wanachokuwa wakikifanya, lakini wanatupa nafasi ya kujifunza vitu vingi ambavyo tunavisahau tunapokuwa watu wazima. Kuna sababu ya kwanini watoto wanaitwa zawadi kutoka kwa Mungu. Wanatufundisha kuboresha maisha yetu, kuona vitu vizuri kwenye maisha pamoja na kujaa tabasamu kila siku. Ni wazi kuwa yapo mambo mengi mazuri na yenye manufaa makubwa ambayo kila mtu anaweza kujifunza kutoka kwa watoto; yafahamu mambo hayo sasa. 1. Kuwa na furaha Maisha ya watoto yamejaa furaha. Mara nyingi utawakuta watoto wakiimba, wakikimbia, wakiruka, wakitaniana kwa furaha bila wasiwasi. Hili limefanya maisha ya utoto kuwa saw...