Fahamu Hili Archives - Page 10 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara

Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara

Biashara na Uchumi
Kuchagua wazo la biashara ni hatua ngumu na muhimu sana. Watu wengi hawafanikiwi kwenye biashara zao kwa kuwa wanakosea katika hatua hii. Uchaguzi sahihi wa wazo la biashara ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya biashara yako. Ikiwa unataka kuanza biashara, basi karibu nikushirikishe mambo 5 ambayo unapaswa kuyazingatia kabla ya kuchagua wazo la biashara. 1. Chagua wazo unalolipenda Kanuni mojawapo ya kufanikiwa katika kile unachokifanya ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapochagua wazo unalolipenda ni wazi kuwa utalifanya kwa moyo na kwa ufanisi mkubwa hata kama utakutana na changamoto. Hivyo, usichague wazo kwa sababu fulani amelichagua au linampa faida kubwa mtu mwingine; kwako linaweza kuwa gumu na lenye hasara kubwa. 2. Chagua wazo unalolifahamu na kulimu...
Makosa 15 ya Kuepuka Katika Malezi ya Watoto

Makosa 15 ya Kuepuka Katika Malezi ya Watoto

Mahusiano na Familia
Swala la malezi ya watoto ni swala nyeti, pana, gumu, na lenye changamoto nyingi; hivyo linahitaji umakini mkubwa na maarifa stahiki. Kutokana na umuhimu huu basi, ni wazi kuwa changamoto au matatizo mengi ya kimalezi yanayotokea kwenye maisha ya watoto yanatokana na makosa yanayofanywa na wazazi katika malezi. Pamoja na kwamba hakuna kanuni ya malezi, lakini yapo makosa ambayo wazazi wanapaswa kuyaepuka katika swala la malezi ili kuhakikisha watoto wao wanakuwa katika maadili na misingi sahihi. Karibu nikufahamishe makosa 15 ambayo kila mzazi au mlezi anatakiwa kuyaepuka katika malezi ya kilasiku ya watoto. 1. Kumfurahisha mtoto Kumfurahisha mtoto ni muhimu kufanywa na kila mzazi au mlezi, lakini ni lazima kuwe na kiasi. Wazazi wengi wamekuwa wakifanya kosa la kutaka kuwafa...
Njia 10 za Kukufanya Kuwa na Furaha

Njia 10 za Kukufanya Kuwa na Furaha

Tija
Kutokana na changamoto za kimazingira, kiuchumi na kijamii, watu wengi wamejikuta wakikosa furaha. Ni wazi kuwa kukosa furaha kuna madhara makubwa kwenye afya ya mwili, akili na hata katika utendaji wako wa kazi. Watu wengi hutamani kuwa na furaha lakini bado hawapati furaha; wengi hudhani kuwa na vitu kama vile pesa ndiyo chanzo cha furaha, lakini mambo hayawi kama walivyotarajia pindi wapatapo vitu hivyo. Je unahitaji kuwa na furaha ili uboreshe afya na ufanisi wa utendaji kazi wako? Karibu nikushirikishe njia 10 za kukufanya kuwa na furaha. 1. Samehe Watu wengi hukosa furaha kutokana na kubeba uchungu na maumivu yaliyotokana na watu waliowakosea. Ikiwa unataka kuwa na furaha ni muhimu kumsamehe aliyekukosea hata kama hajaomba msamaha. Kumsamehe aliyekukosea kuna manufaa k...
Faida 20 za Kula Parachichi

Faida 20 za Kula Parachichi

Mtindo wa Maisha
Parachichi ni aina ya kipekee ya tunda. Matunda mengi kwa asili ni wanga lakini parachichi limejaa mafuta yenye manufaa makubwa kiafya. Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimebaini kuwa tunda la parachichi limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu. Ikiwa unapenda kuwa na afya bora kwa kula tunda la parachichi, basi karibu nikushirikishe faida 20 za kula tunda la parachichi. 1. Parachichi limejaa virutubisho mbalimbali Parachichi ni tunda la pekee ambalo limebeba virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa ajili ya miili yetu. Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi ni: Kalori 240 (184 inatokana na mafuta) Miligramu 11 za sodiamu Gramu 13 za wanga Gramu 10 za nyuzinyuzi za lishe Gramu 1 tu ya sukari Vitamini K: asilimia 26 Vitamini...
Athari 5 za Kutumia Vyombo vya Chakula vya Plastiki

Athari 5 za Kutumia Vyombo vya Chakula vya Plastiki

Afya
Plastiki ina nafasi kubwa kwenye jamii ya leo; hutumika kwenye magari, vyombo vya nyumbani, vifaa vya watoto vya kuchezea, simu, kompyuta n.k. Kwa hakika siyo rahisi mtu kumaliza siku nzima bila kutumia kifaa chochote cha plastiki. Pamoja na nafasi hii kubwa ya matumizi ya plastiki, plastiki imekuwa na athari mbalimbali kwenye afya ya binadamu pamoja na mazingira. Karibu nikufahamishe madhara au athari 5 zitokanazo na matumizi ya vifaa au vyombo vya chakula vilivyotengenezwa kwa plastiki. 1. Sumu zilizoko kwenye plastiki zinaweza kukufanya uugue Tafiti mbalimbali zimebainisha kuwa sumu zilizoko kwenye vifaa vya plastiki zinaweza kusababisha maradhi kama vile saratani, maradhi ya kupoteza kumbukumbu, maradhi ya moyo pamoja na kupoteza uwezo wa kuona. Wataalamu mbalimbali wali...
Faida 10 za Kuogea Maji ya Baridi

Faida 10 za Kuogea Maji ya Baridi

Mtindo wa Maisha
Watu wengi hupenda kuogea maji ya moto, hii ni kutokana na kuogopa baridi au sababu za kimazoea tu. Ingawa mara nyingi umekuwa ukisisitiziwa kuwa maji moto yana manufaa mengi, lakini hata maji ya baridi nayo yana manufaa yake. Je uko tayari kuongeza maarifa au hata kubadili mtazamo wako? Karibu nikushirikishe faida 10 za kuogea maji ya baridi. 1. Huongeza utayari Maji ya baridi hukufanya uchangamke, hili ni tofauti na maji ya moto. Mara nyingi mtu anapoogea maji ya baridi hasa baada ya kuamka humfanya awe katika hali nzuri ya kuwa tayari kuendelea na majukumu yake. Kumbuka hata wakati wa kuogea maji baridi kasi ya upumuaji hubadilika na kukufanya kuongeza kiasi cha oksijeni kinachoingia mwilini. 2. Hulainisha ngozi na nywele Maji moto huchubua ngozi na nywele, hasa kwa kuondo...
Sababu 10 za Kwanini Baadhi ya Watu Kamwe Hawatafanikiwa

Sababu 10 za Kwanini Baadhi ya Watu Kamwe Hawatafanikiwa

Maendeleo Binafsi
Kila mtu anatamani kufanikiwa, lakini siyo wote wanatimiza lengo hili. Ni wazi kuwa hakuna njia ya mkato ya kufika kwenye kitu kizuri. Ukiwachunguza sana watu waliofanikiwa, utagundua kuwa kuna tabia au mambo kadhaa yanayoshabihiana kati yao. Pia ukiwachunguza watu walioshindwa au ambao hawajafanikiwa, utabaini pia kuna tabia au mambo kadhaa yanayofanana kati yao. Je unatamani kufanikiwa? Basi fahamu sababu 10 zinazowafanya baadhi ya watu kamwe wasifanikiwe kwenye maisha yao. 1. Kutokujali muda Mafanikio yamefugwa kwenye muda. Ili mtu aweze kufanikiwa ni lazima ajifunze kutumia muda wake vyema. Watu wasiofanikiwa hawana mipaka; huchelewa kila mahali, pia hawathamini muda wa wengine. Hawana vipaumbele wala muda wa kuweka malengo na vipaumbele kwenye maisha yao; wao huishi tu ...
Sababu 7 za Kwanini Kila Mwanaume Anatakiwa Kujua kupika

Sababu 7 za Kwanini Kila Mwanaume Anatakiwa Kujua kupika

Mtindo wa Maisha
Kutokana na asili ya utamaduni wa Kiafrika, bado kwa kiasi kikubwa swala la kupika linachukuliwa kama kazi ya mwanamke. Wanaume wengi hawafahamu kupika wala hawataki kujifunza kupika. Nimeshuhudia wengi wakiwa tayari kula hotelini au kula mikate pindi wakosapo watu wa kuwapikia chakula. Kwa hakika yapo mambo mengi mazuri ambayo mwanaume asiyejua kupika anayakosa. Karibu nikushirikishe sababu 7 za kwanini kila mwanaume anatakiwa kujua kupika; nami naamini baada ya makala hii utajifunza mengi na kuhamasika. 1. Kuweza kula unachokitaka Kwa njia ya kufahamu kupika unaweza kula chakula unachotaka ambacho isingekuwa rahisi kukipata hotelini au kupikiwa na mtu mwingine. Ikiwa pia kuna aina fulani ya upishi unaipenda, basi kwa njia ya kufahamu kupika utaweza kuifanya wewe mwenyewe. ...
Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta

Njia 5 za Kuongeza Kasi na Usahihi wa Kuandika (Typing) kwa Kutumia Kompyuta

Tija
Kuandika kwa kasi na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta kuna manufaa mengi kama vile kuweza kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi, kuweza kuandika mambo mbalimbali kwa kutumia kompyuta na hata sifa ya kukuwezesha kupata kazi mbalimbali. Hivyo, najua unatamani kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi kwa kutumia kompyuta; lakini tatizo bado hujaweza kuacha kasi ya kudonoa na kuweza kuandika kwa kasi kubwa na kwa usahihi. Karibu ufahamu njia 5 ambazo unaweza kuzitumia ili kuboresha uwezo wako wa kuandika kwa kutumia kompyuta. 1. Elewa na tumia baobonye (keyboard) vyema Ili uweze kuongeza kasi yako ya kuandika pamoja na usahihi ni lazima uelewe baobonye vyema na kuitumia vyema. Zingatia haya yafuatayo: Elewa mpangilio wa vitufe kwenye baobonye. Panga vidole kulingana na vitufe sta...
Virusi 10 vya Kompyuta Hatari Zaidi Kuwahi Kutokea

Virusi 10 vya Kompyuta Hatari Zaidi Kuwahi Kutokea

Maarifa
Virusi vya kompyuta ni tatizo la muda mrefu ambalo limeathiri watu wengi kwa namna moja au nyingine. Inawezekana wewe ni mmojawapo kati ya wale waliowahi kuathiriwa na virusi vya kompyuta; inawezekana pia hujawahi kuathiriwa au hata kusikia swala hili kabisa. Katika muda ambao Mungu amenijalia kutumia kompyuta (2002 - hadi sasa), nimeshuhudia mengi na kukabiliana na mengi kuhusu virusi vya kompyuta. Nimewahi kuona watu wakilia kwa kupoteza taarifa muhimu, wengine wakitoa fedha nyingi kutengeneza kompyuta zao zilizoathirika. Mimi mwenyewe nimewahi kuathiriwa mara kadhaa na virusi hivi. Hivyo basi, hebu leo tutazame virusi 10 vya kompyuta vilivyowahi kutokea ambavyo ni hatari zaidi. 1. Code Red Kirusi cha Code Red kiliibuka mnamo mwaka 2001 na kubainiwa na wafanyakazi wawi...