Programu 6 za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza
Kama wewe ni mwandishi wa machapisho au wa blogu, unafahamu jinsi ilivyo muhimu kuandika makala zenye ubora. Wengi wetu hutumia muda mwingi kuandika, kubuni na hata kupangilia makala au machapisho yetu kuliko muda tunaotumia kuhariri. Kuhariri ni sehemu muhimu katika uandishi wowote ili kukuwezesha kuandika makala yenye ubora. Kwa kutambua umuhimu huu nimekuandalia orodha ya programu 6 za kompyuta zitakazokuwezesha kupunguza kama siyo kuondoa kabisa makosa katika uandishi wa Kiingereza Soma pia: Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora.
1. Grammarly
Hii ni programu maarufu sana yenye uwezo wa kubaini makosa mengi ambayo usingeweza kuyabaini kwa njia ya kawaida. Kiunganishi: Grammarly
2. Polishmywriting
Hii ni programu nzuri ya kuhariri inayoonyesha makosa kwa rangi tatu. Nyekundu ni mako...