
Mambo Matano ya Kufanya ili Kuharakisha Kupona Majeraha
Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia. Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.
1. Kula vizuri
Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi. Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.
2. Pumzika vya kutosha
Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. K...










