Fahamu Hili Archives - Page 15 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Njia 14 Halali za Kupata Pesa Kupitia Blog

Njia 14 Halali za Kupata Pesa Kupitia Blog

Kipato, Tovuti na Blogu
Je unatafuta njia ya kujipatia pesa kwenye mtandao ambayo siyo ya utapeli? Blog ni njia moja wapo unayoweza kuitumia kujipatia fedha huku ukifanya kile ukipendacho. Katika makala hii nitakushirikisha njia 14 unazoweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia blog yako. Kumbuka! Hizi si njia za kupata pesa za mteremko haraka haraka kwa usiku mmoja. Kamwe usidanganywe na matangazo ya kuwa utafanywa kuwa tajiri mkubwa siku moja. Mambo hayaendi hivyo. Awali ya yote utahitaji kuwa na blog yako; pia utahitajika kuwekeza rasilimali ya muda au pesa kiasi fulani ili kuweza kuona matokeo kutokana na blog yako. 1. Kuwa wakala Unaweza kupata pesa kwenye blog yako kwa njia ya kuwa wakala wa wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mara mtu anunuapo kitu kwa kukifikia kupitia blog yako basi utapata ...
Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako

Mambo 12 ya Kufanya kwa Ajili ya Kesho Yako

Maendeleo Binafsi
Ni mara ngapi umejiambia kuwa kesho itakuwa siku nzuri na unatamani kuiona na kuiishi? Ni mara chache sana. Hofu na mashaka vimetawala na kuchukua nafasi katika kesho za watu wengi. Jambo zuri kwenye maisha ni kuwa una nafasi ya kutawala mambo mengi yanayotokea katika maisha yako. Kama kesho inafanana na leo hakuna maana; ikiwa leo ulikuwa na huzuni basi angalau kesho iwe na furaha. Hivyo kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya leo na kuhakikisha kuwa kesho inakuwa nzuri. Hapa kuna mambo 12 ambayo unayoweza kuyafanya na kuifanya kesho yako kuwa nzuri na yenye tija. 1. Panga kwa ajili ya kesho. George anatukumbusha  kuwa maandalizi bora ya kesho hufanywa leo. Kuwa na mpango wa kesho leo kutakuwezesha kufanya mambo kwa kutegemea mwongozo na mpangilio uliopo badala ya kuamka na kufan...
Vitu 15 Vinavyofanywa na Watu Werevu (Smart)

Vitu 15 Vinavyofanywa na Watu Werevu (Smart)

Tija
Unaweza kujiuliza ni mambo gani yanayomfanya mtu kuwa mwerevu (smart). Je ni wingi wa maarifa anayoyafahamu? Au je ni kiwango cha wastani au cha juu cha kufikiri kwake? Ukweli ni kuwa ni werevu ni uwezo wa kufanya maamuzi yatakayofaa wakati wote; au ni kuweza kuibua kitu kizuri katika kitu kibaya au wakati mbaya. Watu werevu huweza kufanya maamuzi ambayo yanazingatia matokeo ya mbeleni ya maamuzi hayo. Ni dhahiri kuwa watu werevu (smart) ni tofauti na watu wengine kutokana na yale wanayoyafanya au kutofanya. Fahamu mambo 10 ambayo watu werevu hawayafanyi. 1. Hawapuuzi uwekaji akiba Katika maisha ya kiuchumi kuna vipindi viwili; kipindi cha mavuno(shibe) na kipindi cha ukame(njaa). Ni watu wachache sana ndio wanaoweza kuishi katika vipindi hivi viwili bila shida. Watu werevu hawapu...
Mambo 10 Unayoweza Kujifunza Kutoka kwa Lionel Messi

Mambo 10 Unayoweza Kujifunza Kutoka kwa Lionel Messi

Hamasa
Lionel Messi alizaliwa tarehe 24 Juni 1987 huko Rosario, Jimbo la Santa Fe huko Argentina. Akiwa na miaka mitano Messi alianza kucheza mpira wa miguu kwenye klabu ya Grandol iliyokuwa ikifundishwa na baba yake. Wakati Messi akiwa mdogo, alibainika kuwa na tatizo au maradhi ya kuwa na upungufu wa seli za ukuaji. Akiwa na umri wa miaka 13 alihamia Uhispania na kujiunga na klabu ya Barcelona ambayo ilikubali kugharamia matibabu yake. Pamoja na changamoto alizokuwa nazo Messi amefanikiwa kupata mafanikio makubwa sana. Messi anachukuliwa kama mchezaji bora zaidi duniani na mmoja kati ya wachezaji bora waliowahi kuwepo. Messi ni mchezaji pekee aliyeshinda tuzo ya FIFA ya Ballon d'Or  mara tano, zikiwemo nne mfulilizo. Pia ni mchezaji pekee aliyeshinda tuzo ya kiatu cha dhahabu (European Gol...
Sababu 9 za Kwanini Umsamehe Aliyekukosea

Sababu 9 za Kwanini Umsamehe Aliyekukosea

Maendeleo Binafsi
Umesikia mara nyingi sana kuwa “Unatakiwa kusamehe na kusahau”. Nini maana halisi ya kusamehe? Kusamehe ni kuamua kutomchukulia mtu hatua na kuondoa kinyongo moyoni mwako kutokana na jambo baya ulilofanyiwa na mtu huyo. Kusamehe kunasema hutakiwi kusikia neno “nisamehe” ndipo uendelee na maisha yako. Kusamehe kumewekwa na ni kwa manufaa zaidi kwa yule aliyekosewa. Ni wazi kuwa katika maisha kuna kukoseana kwa namna mbalimbali. Wapo watu wasiopenda suluhu wala msamaha. Ni dhahiri kuwa ni lazima wewe uliyekosea ufahamu manufaa na sababu za kumsamehe na kumsahau aliyekukosea; manufaa hayo ni haya yafuatayo. 1. Hukuweka huru Kutokusamehe kunakufanya ujisikie vibaya na kuwa kama mfungwa. Jambo baya ni pale utakapomwona yule aliyekukosea anafuraha na anaendelea na maisha yake bila ta...
Mambo 15 ya Kushangaza Kuhusu Afrika

Mambo 15 ya Kushangaza Kuhusu Afrika

Maarifa
Vita, njaa, vifo, maradhi - ni vitu ambavyo wengi wamevisikia na kuvifahamu kuhusu Afrika. Lakini sasa ni wakati wa kubadili mtazamo huu. Afrika ni bara la kushangaza ambalo ni tofauti kabisa na mabara mengine saba. Afrika ina utajiri katika urithi wa utamaduni wa kipekee, utajiri wa rasilimali za asili pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii. Nakukaribisha ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu mambo 15 ya kushangaza na kusisimua kuhusu Afrika. Mlima Kilimanjaro unapatikana barani Afrika. Mlima huu una urefu wa takriban meta 5,895 kutoka usawa wa bahari. Mlima huu unapatikana kaskazini mwa Tanzania. Zaidi la asilimia 25 ya lugha huzungumzwa Afrika. Inaaminika kuwa kuna takriban lugha 2000 zinazozungumzwa barani Afrika. Lugha zote hizi zinatambuliwa na umoja wa Afrika. Nigeri...
Namna ya Kuwa Mzungumzaji Hamasa (Motivational Speaker)

Namna ya Kuwa Mzungumzaji Hamasa (Motivational Speaker)

Maendeleo Binafsi
Ninapotaja wazungumzaji hamasa (Motivational Speakers) naamini unafahamu kuwa ni watu wanaowasaidia watu kuendeleza na kuwezesha maono au utoto wao wa ndani ili watu husika waweze kufanikiwa. Mzungumzaji hamasa anaweza kuzungumzia mada yoyote ile kulingana na uzoefu wake. Wengi hutamani kuwa wazungumzaji hamasa lakini wameshindwa kujua waanzie wapi. Jambo la msingi katika uzungumzaji hamasa ni shauku yako ya ndani katika mada unayotaka kuizungumzia. Kuwa mzungumzaji hamasa kunahitaji kubaini mada na walengwa wa mada yako bila kusahau kunoa uwezo wako wa kuzungumza mbele ya watu pamoja na kuielewa vyema mada husika. Kama unatamani kuwa mzungumzaji hamasa, fuatilia hoja jadiliwa hapa chini kwa makini ili sasa uweze kuwa mzungumzaji hamasa. 1. Bainisha mada utakayozungumzia Huwezi ku...
Misamiati 20 ya Kiswahili Unayoitumia Kimakosa

Misamiati 20 ya Kiswahili Unayoitumia Kimakosa

Mtindo wa Maisha
Ni wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakijitahidi kutumia lugha za kigeni kwa usahihi kuliko Kiswahili. Ni rahisi mtu kuona aibu kufanya makosa katika lugha kama vile Kiingereza na Kifaransa lakini siyo Kiswahili. Ni dhahiri kuwa yapo makosa mengi yanayofanywa na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutokana na kutotilia maanani swala la umahiri katika lugha. Makosa haya yasipotiliwa maanani yanaweza kukufanya uonekane duni katika uwezo wako wa kutumia lugha. Yapo makosa mbalimbali ambayo hufanywa na watumiaji wa lugha yakiwemo yale ya kimsamiati, kimatamshi, kimuundo n.k. Katika makala hii nitaonyesha misamiati takriban 20 ambayo pengine unaitumia au inatumiwa vibaya na wazungumzaji wa lugha hasa kutokana na makosa ya kimsamiati. 1. Lisaa na Masaa Lisaa na Masaa ni misamiati au...
Programu 6  za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza

Programu 6 za Kuondoa Makosa Katika Uandishi wa Kiingereza

Tija
Kama wewe ni mwandishi wa machapisho au wa blogu, unafahamu jinsi ilivyo muhimu kuandika makala zenye ubora. Wengi wetu hutumia muda mwingi kuandika, kubuni na hata kupangilia makala au machapisho yetu kuliko muda tunaotumia kuhariri. Kuhariri ni sehemu muhimu katika uandishi wowote ili kukuwezesha kuandika makala yenye ubora. Kwa kutambua umuhimu huu nimekuandalia orodha ya programu 6 za kompyuta zitakazokuwezesha kupunguza kama siyo kuondoa kabisa makosa katika uandishi wa Kiingereza Soma pia: Njia 10 za Kuwa Mhariri Bora. 1. Grammarly Hii ni programu maarufu sana yenye uwezo wa kubaini makosa mengi ambayo usingeweza kuyabaini kwa njia ya kawaida. Kiunganishi: Grammarly 2. Polishmywriting Hii ni programu nzuri ya kuhariri inayoonyesha makosa kwa rangi tatu. Nyekundu ni mako...
Mambo 6 Usiyoyafahamu Kuhusu Pesa

Mambo 6 Usiyoyafahamu Kuhusu Pesa

Maarifa
Inawezekana unabeba pesa kwenye pochi au mfuko wako au pengine umezitunza benki, lakini ni kwa kiasi gani unafahamu kuhusu pesa? Ni dhahiri kuwa unaweza kuzitumia pesa hadi mwisho wa maisha yako bila hata kujua mambo fulani yanayozihusu. Fuatilia makala hii nikufahamishe mambo 6 usiyoyafahamu kuhusu pesa. 1. Pesa ya noti siyo karatasi Watu wengi wanafikiri kuwa pesa ya noti imetengenezwa kwa karatasi lakini si kweli. Malighafi zilizotengenezea pesa ya noti, mojawapo ni pamba. Imetengenezwa hivi ili iwe imara zaidi na yenye kukabiliana na mambo kama vile vimiminika na uchafu. 2. Wazo la ATM liliibuka bafuni Mgunduzi John Shepherd-Barron alipata wazo la kuweka ATM bafuni manamo miaka ya 1960 akiwa bafuni. 3. Pesa zina virusi vya mafua na cocaine Utafiti umebaini kuwa kutokana n...