
Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu
Hofu ni hisia ambazo zinatulinda na vitisho vinavyotuzunguka. Kila mtu ana hofu, lakini viwango na aina ya hofu hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Wapo watu ambao huhofu juu ya vitu na mambo mbalimbali hadi kushindwa kuendelea na majukumu au maisha yao ya kawaida. Ikiwa unapenda kufahamu aina za hofu (phobia) ili pia uchunguze kama una aina hizo basi fuatilia makala hii nikufahamishe aina 70 za hofu. Pogonophobia – Pogonophobia ni hofu ya kuogopa ndevu au kukaa karibu na mtu mwenye ndevu. Hofu hii huwapata zaidi wanawake.
Astraphobia – Hofu hii pia inajulikana kama astrapophobia, brontophobia, keraunophobia, au tonitrophobia; hii ni hofu ya kuogopa radi.
Photophobia – Hii ni hofu ya kuogopa mwanga; mara nyingi husababishwa na matatizo ya kiafya ya macho. So...










