Blog - Page 5 of 20 - Fahamu Hili
Monday, February 9Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Blog

Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu

Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu

Maendeleo Binafsi
Ni watu wachache sana ndiyo wanaopenda na wanafahamu umuhimu wa kusoma vitabu. Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma vitabu ikiwa hakuna kinachowalazimisha kufanya hivyo kama vile mtihani, kazi, n.k. Kwa hakika kuna maarifa mengi yaliyofichwa kwenye vitabu; hii ndiyo sababu watu wengi waliofanikiwa husoma au hata kuandika vitabu. Ikiwa unataka kupata maarifa na kuboresha maisha yako kwa njia ya kusoma vitabu, basi fahamu faida 15 za kusoma vitabu. 1. Hukuongezea marifa mapya Lengo kubwa linalowafanya waandishi wa vitabu kuandika vitabu ni kuweka maarifa yao kwenye maandishi. Hivyo kwa kusoma vitabu unapata maarifa mbalimbali yaliyowekwa kwenye kitabu husika. Hivi leo kuna vitabu vinavyohusu takriban kila kitu; kwa hiyo maarifa yoyote unayoyahitaji unaweza kuyapata kwenye...
Faida 19 za Kula Maharage Kiafya

Faida 19 za Kula Maharage Kiafya

Mtindo wa Maisha
Maharage ni chakula ambacho watu wengi hukichukulia kama chakula cha hadhi ya chini kisichokuwa na manufaa kiafya. Watu wengi huchukulia vyakula kama vile nyama na samaki kuwa ni vya kitajiri wakati maharage yakichukuliwa kuwa ni chakula cha kimaskini. Huu ni upotoshaji, kwani maharage yana faida nyingi sana mwilini ambazo watu wasiokula maharage wanazikosa. Kwa kuwa lengo letu ni kukupa maarifa, basi karibu ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu faida 19 za kula maharage. 1. Hupunguza lehemu (cholesterol) Moja kati ya vyakula vinavyopunguza lehemu mwilini ni maharage. Nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye maharage hujishikiza na lehemu ziwapo tumboni na kuzuia lehemu zaidi kufyonzwa mwilini. 2. Huzuia saratani Maharage ni chakula chenye madini ya manganese pamoja na vitamini K a...
Faida 7 za Kuwa na Ratiba Binafsi

Faida 7 za Kuwa na Ratiba Binafsi

Tija
Ratiba siyo muhimu tu kwa ajili ya taasisi fulani pekee; ni muhimu pia kwa mtu binafsi. Watu wengi hushindwa kutumia muda wao vyema kutokana na kutokuwa na ratiba nzuri inayoeleweka. Kuweka ratiba kutakuwezesha kupangilia kazi na mipango yako kwa namna ambayo utaweza kuitekeleza vyema. Ikiwa unataka kuwa mwenye tija na ufanisi zaidi, basi fahamu faida 7 za kuwa na ratiba binafsi. 1. Kutumia muda vyema Moja kati ya manufaa makubwa ya kuwa na ratiba ni kuweza kutumia muda vyema. Unapokuwa na ratiba ni vigumu kupata muda ambao haujapangiwa jukumu au kazi kwenye ratiba. Unapokuwa na ratiba muda wako wote utatumika vizuri tena kwa shughuli yenye tija iliyopangwa. Hivyo ni vyema kuhakikisha unajiwekea ratiba na unaifuata ipasavyo. Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumiz...
Mambo 9 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Web Host

Mambo 9 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Web Host

Tovuti na Blogu
Kuna mahali ambapo kila tovuti au blog hutunzwa, mahali hapo ndipo hufahamika kama web host. Web host bora ni muhimu sana kwa ajili ya tovuti au blog yako. Watu wengi wamekuwa wakifanya makosa wakati wa kuchagua web host kutokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa web host bora pamoja na njia za kubaini web host bora. Madhara ya web host duni ni: Kasi ndogo ya tovuti yako au blog. Athari ya kudukuliwa kutokana na miundombinu duni ya usalama. Kukosa huduma bora na muhimu. Kutokupatikana kwa tovuti yako kila wakati. Ikiwa unataka kuchagua web host bora kwa ajili ya tovuti au blog yako, basi fahamu mambo 9 muhimu ya kuzingatia wakati wa kuchagua web host. 1. Bainisha mahitaji yako Kabla ya kuchagua web host ni muhimu ubainishe mahitaji yako kwanza. Je tovuti au blo...
Sababu 7 za Kwa nini Hutakiwi Kutafuta Mpenzi Kwenye Mtandao wa Intaneti

Sababu 7 za Kwa nini Hutakiwi Kutafuta Mpenzi Kwenye Mtandao wa Intaneti

Mahusiano na Familia
Maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia hasa katika sekta ya mawasiliano yamebadili mambo mengi. Hili ni tofauti na hapo awali ambapo watu walitegemea njia duni za mawasiliano kama vile posta. Kutokana na maendeleo haya katika teknolojia ya mawasiliano, suala la mahusiano pia limebadilika kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanaweza kutafuta wapenzi kwenye mtandao wa intaneti bila kizuizi chochote. Kwa hakika bila shaka kila jambo lina uzuri na ubaya  wake; hivyo suala la kutafuta wapenzi kwenye mtandao linatakiwa kutazamwa kwa jicho la pili. Ikiwa umejiunga au unataka kujiunga na mitandao ya kutafuta wapenzi, basi fahamu sababu 7 za kwanini hutakiwi kutafuta mpenzi kwenye mtandao wa intaneti. 1. Watu wanaigiza uhalisia Katika eneo ambalo watu wanaigiza uhalisia wa maisha kw...
Mambo Matano ya Kuzingatia Kabla ya Kuajiri Mtu Kupitia Mtandao wa Intaneti

Mambo Matano ya Kuzingatia Kabla ya Kuajiri Mtu Kupitia Mtandao wa Intaneti

Biashara na Uchumi
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili maisha ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa. Sekta ya ajira nayo imepokea mabadiliko mengi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hivi leo ni rahisi mtu kuishi Afrika akafanya kazi Marekani au mtu akaishi India akaajiriwa Tanzania. Haya yote ni kutokana na teknolojia kuwezesha watu kuajiri au kuajiriwa kwa kupitia njia ya mtandao wa intaneti. Kwa kutambua kuwa kuajiri kwa njia ya mtandao ni njia nzuri ya kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni pamoja na kupata mtu mwenye sifa stahiki kwa kazi husika, basi fahamu mambo matano ya kuzingatia kabla ya kuajiri mtu kupitia mtandao. 1. Maarifa sahihi Kuna wafanyakazi wengi kwenye mtandao wa intaneti, lakini siyo wote ni bora au wana maarifa stahiki. Ni muhimu sana kufanya utafiti wa ...
Mambo 10 ya Kufanya Ili Kuepuka Ajali Unapoendesha Pikipiki

Mambo 10 ya Kufanya Ili Kuepuka Ajali Unapoendesha Pikipiki

Usafiri na Safari
Pikipiki au kwa jina maarufu bodaboda, zinatumiwa na watu wengi sana kwa usafiri. Licha ya pikipiki kutumiwa kama usafiri, wengine huzitumia kama chanzo cha kipato chao cha kila siku. Hata hivyo kila mmoja amewahi kusikia au kushudia juu ya changamoto kubwa ya ajali inayokabili usafiri wa pikipiki au bodaboda. Wengine wamepata majeraha, kupoteza maisha, kupoteza mali au hata kupata ulemavu wa kudumu. Pasipo shaka sasa ni wakati wa kutazama ni nini hasa chanzo cha ongezeko kubwa la ajali za pikipiki ili kikabiliwe. Ikiwa unaendesha pikipiki au unataka kuongeza maarifa yako, basi fahamu mambo 10 ya kufanya ili kuepuka ajali unapoendesha pikipiki au bodaboda. 1. Pata elimu sahihi ya kuendesha pikipiki Pikipiki ni chombo cha kitaalamu kinachohitaji maarifa sahihi ya kukitumia. A...
Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo

Sifa 10 Ambazo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuwa Nazo

Ujasiriamali
Kwa hakika ujasiriamali ni chaguo muhimu sana kwenye karne hii ya sasa ili kujipatia kipato. Hivi leo kuna wajasiriamali wengi waliofanikiwa na wengine hawajafanikiwa. Kwa hakika wajasiriamali waliofanikiwa wanafahamu na wanaziishi sifa za wajasiriamali bora. Ni wazi kuwa huwezi kuwa mjasiriamali bora wakati una sifa za mwajiriwa. Ili kuwa mjasiriamali ni lazima kuzifahamu na kuziishi sifa za mjasiriamali. Karibu nikufahamishe sifa 10 za mjasiriamali. 1. Mwenye malengo Malengo ni mwongozo wa kukuwezesha kufanikisha jambo lolote. Kuwa na malengo ni sifa muhimu ambayo kila mjasiriamali anapaswa kuwa nayo. Je umeamua kuwa mjasiriamali kwenye nini? Kwa ajili ya nini? Malengo yatakuongoza ufanye nini, wapi lini na kwa ajili ya nini. Bila malengo utafanya mambo bila mwongozo wowot...
Sababu 6 za Kwanini Mara Nyingi Wanawake Huishi Zaidi ya Wanaume

Sababu 6 za Kwanini Mara Nyingi Wanawake Huishi Zaidi ya Wanaume

Afya
  Mara nyingi tumeshuhudia katika familia nyingi mwanaume akitangulia kufa kabla ya mwanamke. Simaanishi kuwa wanaume wote wanakufa mapema, lakini mara nyingi wanawake huishi zaidi kuliko wanaume. Swala hili limepelekea kuibua shauku ya kufanya utafiti zaidi juu ya sababu za wanaume wengi kufa mapema kuliko wanawake. Kwa kuwa lengo la Fahamuhili.com ni kukupa maarifa, basi karibu ufahamu kwanini mara nyingi wanawake huishi miaka mingi zaidi ya wanaume. 1. Wanawake hujali afya zao zaidi Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya zilibaini kuwa wanawake hujali afya zao zaidi. Tafiti hizo zinaeleza kuwa wanawake wengi wanapojihisi kuumwa huenda hosipitalini ili kupata ushauri wa kitaalamu. Hali ni tofauti kwa wanaume, kwani wao huvumilia maumizu au hata kutumia...
Mambo 6 Muhimu ya Kufanya Kabla ya Kustaafu

Mambo 6 Muhimu ya Kufanya Kabla ya Kustaafu

Kipato
Kustaafu ni msimu mpya ambao kila mwajiriwa anapaswa kuufahamu na kujiandaa kwa msimu huo vyema. Kumeshuhudiwa watu wakiishi maisha ya taabu na mahangaiko makubwa baada ya kustaafu. Hili linatokana na kutokujiandaa vyema kabla ya kustaafu. Kwa kufahamu umuhimu wa kujiandaa vyema kabla ya kustaafu; karibu ufahamu mambo 6 muhimu ya kufanya kabla ya kustaafu. 1. Jiandae kisaikolojia Kustaafu ni kipindi tofauti sana na kipindi ulichokuwa kwenye ajira. Kipindi hiki utakutana na mtindo mpya wamaisha tofauti na ule uliouzoea. Ni muhimu kujiandaa kisaikolojia kwa maswala kama vile kukaa bila kupata mshahara, ofisi, gari la kampuni au taasisi, nyumba ya taasisi au kampuni pamoja na manufaa mengine ya wafanyakazi. Andaa fikra zako kutambua kuwa wakati wa kufaidi mambo mbalimbali ku...