Kornelio Maanga, Author at Fahamu Hili - Page 11 of 17
Friday, March 27Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Author: Kornelio Maanga

Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako

Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako

Hamasa
Yale tunayoyawaza na kuyatafakari kwenye fikra zetu yana nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu. Ikiwa tunataka kufanikiwa basi ni lazima tufikiri na kutafakari juu ya kufanikiwa. Vivyo hivyo ikiwa tunahitaji kuhamasika kufanya mambo mbalimbali maishani, ni lazima tusome, tusikilize, tutazame na hata tutafakari vitu vitakavyotuhamasisha. Karibu nikufahamishe nukuu 50 (quotes) ambazo zitakuhamasisha katika maswala mbalimbali unayoyafanya maishani mwako. Naamini umehamasika na kufurahia nukuu hizi za hamasa. Ni wazi kuwa kila kitu kinaanza kwenye fikra zetu - tunavyowaza ndivyo ...
Mbinu 7 za Uandishi Bora wa Vitabu

Mbinu 7 za Uandishi Bora wa Vitabu

Tija
Hivi leo vitabu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maarifa; ingawa bado watu wengi hawafahamu tunu inayopatikana katika vitabu. Mara nyingi umekuwa ukisoma vitabu kadha wa kadha ambavyo vimekuburudisha au hata kukufundisha mambo mengi. Lakini pia inawezekana wewe una mambo ambayo ungependa kuyaweka katika vitabu. Ni wazi kuwa kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kuandika kitabu ili kiweze kufikisha ujumbe au kutimiza lengo lililokusudiwa. Karibu ufahamu mbinu 7 zitakazokuwezesha katika uandishi wa vitabu. 1. Chagua wazo bora Hatua ya kwanza kabisa katika uandishi wa kitabu ni kuchagua mada au wazo bora. Hakikisha unachagua wazo au mada kwa makini ambayo itakuwezesha kukamilisha lengo lako. Unaweza kuzingatia haya: Chagua mada ambayo unaipenda na unaielewa vyema. Chag...
Fahamu Vitu Vilivyotengenezwa Upya (recycled) na Kuzalisha Vitu Vingine vya Kuvutia

Fahamu Vitu Vilivyotengenezwa Upya (recycled) na Kuzalisha Vitu Vingine vya Kuvutia

Maarifa
Hivi leo wabunifu mbalimbali wametokea duniani. Wabunifu wengine wamejikita kwenye kutumia ubunifu wao kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za uharibifu wa mazingira. Wapo watu na wabunifu mbalimbali walioona umuhimu wakutengeneza (recycle) tena vitu mbalimbali ambavyo matumizi yake yamekwisha, ili vifae tena kwa matumizi mengine. Mara nyingi tumeshuhudia magurudumu, chupa, mapipa, na hata vifaa vya mitambo mbalimbali vikitupwa hovyo baada ya kumalizika kwa matumizi yake. Lakini sasa ungana nami nikushirikishe vitu kadhaa vilivyotengenezwa upya (recycled) na kuzalisha vitu vya kuvutia na vyenye tija kubwa. 1. Mapipa ya kemikali na mafuta 2. Matairi yaliyozeeka 3. Injini ya gari na sehemu nyingine za gari 4. Sehemu za baisikeli 5. Chupa za plastiki Picha hizi...
Makosa 10 ya Kuepuka Unapotengeneza Logo au Nembo

Makosa 10 ya Kuepuka Unapotengeneza Logo au Nembo

Biashara na Uchumi
Nembo au logo ni jiwe la msingi la bidhaa na kampuni yako. Utambulisho wa biashara, kampuni yako au bidhaa unaonyeshwa kupitia nembo yako, ambayo ni pamoja na jina la kampuni yako. Hivyo, nembo ni moja kati ya mambo makuu ambayo yanafanya biashara yako kukumbukwa na kutambulika. Kwa kutambua umuhimu huu, kampuni na watu mbalimbali wamekuwa wakiwekeza fedha nyingi ili kupata nembo bora. Pamoja na kuwekeza pesa nyingi, bado kampuni na watu wengi hawapati nembo bora. Kwa mfano kampuni ya Pepsi iliwekeza dola milioni 1 lakini wakaishia kupata nembo iliyokumbana na ukosoaji mkubwa. Ni wazi kuwa kuna mambo unayotakiwa kuyazingatia kabla ya kuamua kulipia au kutengeneza nembo yako. Fahamu makosa 10 ambayo kama utayaepuka wakati wa kutengeneza au kuchagua nembo, basi utaweza kuwa na n...
Fahamu Njia 6 za Kulinda Akaunti Zako za Mitandao ya Kijamii

Fahamu Njia 6 za Kulinda Akaunti Zako za Mitandao ya Kijamii

Teknolojia, Tija
Mitandao ya kijamii ni kitu muhimu sana kwenye maisha binafsi na shughuli za kiuchumi kama vile biashara. Kutokana na umuhimu huu, kuna haja ya kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa salama. Je ulishawahi kufikiri nini kitatokea ikiwa mtu mbaya atapata nafasi ya kuingia kwenye akaunti zako? Ni wazi kuwa mambo kama haya hapa chini yanaweza kutokea: Kuiba wafuasi wako utakaokuwa umewakusanya muda mrefu. Kutapeli watu mbalimbali wanaokufahamu katika mitandao ya kijamii kwa kutumia akaunti yako. Kuchafua taswira yako; kumbuka mtu mbaya anaweza kuweka maudhui mabaya yatakayoshusha hadhi yako. Kuiba ama kutumia vibaya taarifa zako binafsi zilizoko kwenye akaunti yako. Ni wazi kuwa ipo sababu ya kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa sal...
Mpiga Ngoma Maarufu wa Mtaani Anayetengeneza Midundo kwa Kutumia Ndoo

Mpiga Ngoma Maarufu wa Mtaani Anayetengeneza Midundo kwa Kutumia Ndoo

Hamasa
Nani anahitaji ngoma wakati anaweza kutumia ndoo kutengeneza sauti na midundo ya pekee? Mpiga ngoma wa mtaani kule Australia aitwaye Gordo, ambaye awali alisoma nchini Japan, anafahamu kuwa inawezekana kutengeneza muziki kutoka kwenye kila kitu bila tatizo lolote. Akiwa mwenye nguvu, nia na shauku, Gordo anaonekana akitumia ndoo, vijiti vya kupigia ngoma na miguu yake kutengeneza midundo mizuri ya ngoma. Ikiwa hana shughuli na wasanii wengine, mwaliko kwenye tukio au sherehe basi utamkuta Gordo akiwa kwenye mitaa ya Sydney akidhihirisha kipaji chake katika jamii. Watu wengi huvutiwa na kipaji chake na hata kumzawadia pesa na vitu vingine; naamini hata wewe utakapotazama video zake hapa chini, hakika atakuvutia na kukuhamasisha sana. Karibu! https://www.youtube.com/watch?v=s...
Kanuni 15 za Ujasiriamali Ambazo ni Lazima Uzifahamu

Kanuni 15 za Ujasiriamali Ambazo ni Lazima Uzifahamu

Ujasiriamali
Ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa ajira umekuwa wa shida sana, watu wengi hujikuta wakiwa na chaguo la kuwa wajasiriamali pekee kwenye maisha yao. Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo. Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali. 1. Kuwa mtatuzi wa matatizo Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajiki...
Mambo 20 ya Kukushangaza Kuhusu Dhahabu

Mambo 20 ya Kukushangaza Kuhusu Dhahabu

Maarifa
Dhahabu ni moja kati ya madini ya thamani duniani. Dhahabu huchimbwa katika sehemu mbalimbali duniani na kisha kutumiwa kutengeneza vitu mbalimbali kama vile fedha, medali, vito vya thamani n.k Nchi nyingi zimejizolea utajiri mkubwa kutokana na madini haya; pamoja na utajiri huu pia nchi nyingi zimesababishiwa uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na uchimbaji wa dhahabu. Naamini umewahi kusikia mengi kuhusu dhahabu, lakini sasa fuatilia makala hii nikufahamishe mambo 20 yakushangaza kuhusu dhahabu. Katika tani moja ya simu za mkononi unaweza kupata dhahabu nyingi zaidi kuliko ambayo ungeipata kutoka kwenye gwangala la dhahabu (gold ore). Ikiwa utafanikiwa kukusanya dhahabu yote iliyoko baharini, basi kila mtu duniani anaweza kupata dhahabu takriban kilo 4. Inakadiriwa k...
Mambo 20 Usiyoyajua Kuhusu Jengo Refu Zaidi Duniani la Burj Khalifa

Mambo 20 Usiyoyajua Kuhusu Jengo Refu Zaidi Duniani la Burj Khalifa

Maarifa
Je unalifahamu jengo la Burj Khalifa lililoko Dubai? Burj Khalifa ni jengo refu zaidi duniani linalodhihirisha uwezo mkubwa wa wahandisi majengo wa karne ya 21. Unapozungumzia urefu wake au kutazama muundo wake, kwa hakika jengo hili litakushangaza; jengo hili liligharimu takriban dola bilioni 1.5 za Kimarekani kulijenga. Pamoja na kuwa ni jengo refu zaidi duniani, jengo hili limevunja rekodi nyingine kadha wa kadha zilizokuwa zimewekwa na majengo mengine. Naamini unapenda kulifahamu zaidi ili kuongeza maarifa yako. Karibu ufuatilie makala hii ili nikujulishe mambo 20 usiyoyajua kuhusu jengo hili la Burj Khalifa. Burj Khalifa ni jengo refu zaidi lililotengenezwa na binadamu duniani, lina urefu wa futi 2,723 au mita 829.8 kutoka kwenye kilele chake hadi ardhini. Hivyo kulifanya ...
Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema

Tovuti 20 Ambazo Ungetamani Kuzijua Mapema

Tija
Unaweza ukawa unajiuliza tovuti hizo ni zipi? Intaneti imejaa tovuti nyingi sana, za maana na zisizo za maana. Hata hivyo bado tovuti za maana na zenye manufaa zimeweza kujibainisha wazi kati ya zile zisizofaa. Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe tovuti 20 ambazo kwa namna moja au nyingine zitakufaa katika maisha yako ya kila siku. 1. Have I Been Pwned? Tovuti: https://haveibeenpwned.com/ Hii ni tovuti nzuri sana kwa ajili ya kukagua kama barua pepe yako imeshavuja kwenye taarifa za siri zilizoibiwa. Hivi leo kuna makampuni na tovuti nyingi zinazodukuliwa na kuibiwa taarifa za watumiaji wake. Hivyo unaweza kuwa ni moja kati ya watu ambao barua pepe zao ziliibiwa. Ikiwa utaambiwa kua barua pepe yako imeonekana kwenye taarifa zilizodukuliwa basi badili neno la siri hara...