
Madhara 12 ya Pombe Kiafya
Siyo siri kuwa pombe husababisha matatizo makuwa ya kiafya, yakiwemo magonjwa ya moyo, ini pamoja na majeraha yatokanayo na ajali zitokanazo na ulevi. Ni dhahiri kuwa vinywaji halisi vilivyotengenezwa kwa matunda bila kilevi ni bora zaidi kwa afya yako kuliko vile vyenye kilevi. Licha ya kuwepo kwa kampeni kadha wa kadha zinazopinga matumizi ya pombe, bado watu wengi wameendelea kushikilia kinywaji hiki bila kufahamu athari zake kwenye afya zao. Fuatilia hapa chini athari 12 za pombe kiafya.
1. Matatizo ya moyo
Unywaji mkubwa wa pombe husababisha matatizo mbalimbali ya moyo kama vile cardiomyopathy, ambapo mishipa ya moyo hudhoofika na kushindwa kusukuma damu. Jambo hili huweza kusababisha damu kuganda na kusababisha kiharusi (stroke). Pombe huchangia sana katika kudhoofisha mish...