Eston J., Author at Fahamu Hili - Page 2 of 5
Thursday, February 21Maarifa Bila Kikomo

Author: Eston J.

Eston ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zinazohusu tija, maendeleo binafsi pamoja na afya bora. Analenga kuwahamasisha wengine pamoja na kuubadili ulimwengu kwa kupitia maarifa stahiki.
Changamoto 12 za Ujasiriamali na Jinsi ya Kuzikabili

Changamoto 12 za Ujasiriamali na Jinsi ya Kuzikabili

Ujasiriamali
Kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake nyingi. Ni wazi kuwa wajasiriamali wakubwa na wadogo, wote hukutana na changamoto; tofauti yao ni chanzo cha changamoto hizo na njia wanazozitumia kuzikabili. Wajasiriamali wadogo ndiyo wamekuwa wakikabiliwa zaidi na changamoto hizo na hata kupelekea kupoteza biashara au miradi yao. Inawezekana wewe ni mmoja wapo wa wajasiriamali wanaokabiliana na changamoto. Karibu nikushirikishe changamoto 12 za ujasiriamali na jinsi ya kuzikabili. 1. Mtaji Kila biashara inahitaji mtaji ili iweze kujiendesha na kujipanua. Wajasiriamali wengi wanashindwa kuanzisha biashara au kupanua biashara zao kutokana na kukosa mtaji. Suluhisho: Kumbuka! Siyo lazima upate mtaji wote unaouhitaji, unaweza kuanza na mtaji kidogo sana n...
Faida 25 za Kutembea kwa Miguu

Faida 25 za Kutembea kwa Miguu

Mtindo wa Maisha
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo. Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii. Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida 25 za kutembea kwa miguu. Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu. Huimarisha mifupa. Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi. Husaidia kupunguza uzito. Huzuia saratani ya utumbo mpana. Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua. Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance). Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya...
Madhara 6 ya Kutumia Dawa Bila Ushauri wa Kitaalamu

Madhara 6 ya Kutumia Dawa Bila Ushauri wa Kitaalamu

Afya
Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari. Kutokana na uwepo wa maduka ya dawa baridi, watu wengi wanapojisikia kuwa wagonjwa, hununua dawa kwenye maduka hayo na kuanza kuzitumia. Ni ukweli usiopingika kuwa dawa zimetengenezwa ili kutibu maradhi fulani ambayo yatabainika kwa mgonjwa baada ya uchunguzi wa kitaalamu. Hivyo matumizi ya dawa bila kufanya uchunguzi wa kitaalamu yanaweza kuwa na madhara makubwa kwenye afya yako. Fahamu madhara 6 ya kutumia dawa bila ushauri au uchunguzi wa kitaalamu. 1. Huongeza sumu mwilini Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo kimsingi ni sumu zinazoua vimelea vya magonjwa. Hivyo kutumia dawa bila vipimo kunaku...
Faida 15 za Kula Tunda la Embe

Faida 15 za Kula Tunda la Embe

Mtindo wa Maisha
Embe ni tunda linalofahamika na kupendwa na watu wengi. Watu hula tunda hili moja kwa moja au kulitumia kutengeneza sharubati (juice). Kwa hakika ikiwa haupendi au haufahamu umuhimu wa tunda hili katika afya yako ni wakati wa kujifunza kitu sasa. Je unajua matunda ni muhimu kwa ajili ya afya yako? Karibu nikushirikishe faida 15 za kula tunda la embe. 1. Huboresha metaboli Embe ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa kiasi kikubwa. Nyuzinuzi zinahitajika sana katika kufanya mchakato wa metaboli (mwili kutumia vrutubisho kujipa nguvu) kwenda vizuri. 2.Huboresha afya ya macho Kula embe kutakunufaisha kwa kulinda macho yako dhidi ya kudhoofu kwa misuli ya macho. Embe ni chanzo kizuri cha vitamini A ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho. Soma pia: Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo W...
Faida 20 za Kula Parachichi

Faida 20 za Kula Parachichi

Mtindo wa Maisha
Parachichi ni aina ya kipekee ya tunda. Matunda mengi kwa asili ni wanga lakini parachichi limejaa mafuta yenye manufaa makubwa kiafya. Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimebaini kuwa tunda la parachichi limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu. Ikiwa unapenda kuwa na afya bora kwa kula tunda la parachichi, basi karibu nikushirikishe faida 20 za kula tunda la parachichi. 1. Parachichi limejaa virutubisho mbalimbali Parachichi ni tunda la pekee ambalo limebeba virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa ajili ya miili yetu. Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi ni: Kalori 240 (184 inatokana na mafuta) Miligramu 11 za sodiamu Gramu 13 za wanga Gramu 10 za nyuzinyuzi za lishe Gramu 1 tu ya sukari Vitamini K: asilimia 26 Vitamini...
Sababu 10 za Kwanini Baadhi ya Watu Kamwe Hawatafanikiwa

Sababu 10 za Kwanini Baadhi ya Watu Kamwe Hawatafanikiwa

Maendeleo Binafsi
Kila mtu anatamani kufanikiwa, lakini siyo wote wanatimiza lengo hili. Ni wazi kuwa hakuna njia ya mkato ya kufika kwenye kitu kizuri. Ukiwachunguza sana watu waliofanikiwa, utagundua kuwa kuna tabia au mambo kadhaa yanayoshabihiana kati yao. Pia ukiwachunguza watu walioshindwa au ambao hawajafanikiwa, utabaini pia kuna tabia au mambo kadhaa yanayofanana kati yao. Je unatamani kufanikiwa? Basi fahamu sababu 10 zinazowafanya baadhi ya watu kamwe wasifanikiwe kwenye maisha yao. 1. Kutokujali muda Mafanikio yamefugwa kwenye muda. Ili mtu aweze kufanikiwa ni lazima ajifunze kutumia muda wake vyema. Watu wasiofanikiwa hawana mipaka; huchelewa kila mahali, pia hawathamini muda wa wengine. Hawana vipaumbele wala muda wa kuweka malengo na vipaumbele kwenye maisha yao; wao huishi tu ...
Sababu 7 za Kwanini Kila Mwanaume Anatakiwa Kujua kupika

Sababu 7 za Kwanini Kila Mwanaume Anatakiwa Kujua kupika

Mtindo wa Maisha
Kutokana na asili ya utamaduni wa Kiafrika, bado kwa kiasi kikubwa swala la kupika linachukuliwa kama kazi ya mwanamke. Wanaume wengi hawafahamu kupika wala hawataki kujifunza kupika. Nimeshuhudia wengi wakiwa tayari kula hotelini au kula mikate pindi wakosapo watu wa kuwapikia chakula. Kwa hakika yapo mambo mengi mazuri ambayo mwanaume asiyejua kupika anayakosa. Karibu nikushirikishe sababu 7 za kwanini kila mwanaume anatakiwa kujua kupika; nami naamini baada ya makala hii utajifunza mengi na kuhamasika. 1. Kuweza kula unachokitaka Kwa njia ya kufahamu kupika unaweza kula chakula unachotaka ambacho isingekuwa rahisi kukipata hotelini au kupikiwa na mtu mwingine. Ikiwa pia kuna aina fulani ya upishi unaipenda, basi kwa njia ya kufahamu kupika utaweza kuifanya wewe mwenyewe. ...
Faida 11 za Push Up Kiafya Unazotakiwa Kuzijua

Faida 11 za Push Up Kiafya Unazotakiwa Kuzijua

Mtindo wa Maisha
Mazoezi ni njia moja wapo ya kutufanya tuwe vizuri na wenye afya njema. Kama unahitaji zoezi ambalo litanufaisha sehemu mbalimbali za mwili wako, push ups ni zoezi moja wapo. Push up ni zoezi ambalo linaweza kufanywa na wanaume na wanawake bila gharama yoyote; na faida zake ni zaidi ya kunyoosha tu misuli. Naamini unapenda afya njema pamoja na maarifa; fuatilia makala hii nikufahamishe faida 11 za zoezi la push up kiafya ikiwa utalifanya mara kwa mara. 1. Huboresha mkao na mwonekano wako Push up ni njia bora ya kuufanya mgongo wako unyooke. Push up huimarisha na kuweka sehemu mbalimbali za mwili wako kukaa jinsi ipasavyo; kwa njiaa hii huufanya mwili wako uwe na mwonekano mzuri. 2. Huimarisha misuli Unapopiga push up unahusisha misuli mbalimbali kwenye mwili wako; misuli hii ni ...
Mbinu 10 za Uhakika  za Kufahamu Kiingereza/English kwa Muda Mfupi

Mbinu 10 za Uhakika za Kufahamu Kiingereza/English kwa Muda Mfupi

Tija
Kujifunza lugha mpya kunaweza kuwa ni kugumu, lakini inawezekana. Je unatamani kufahamu na kumudu lugha ya Kiingereza kwa muda mfupi? Kumudu Kiingereza inawezekana lakini kuna mambo kadhaa unatakiwa kuyafahamu na kuyafanya kwa uhakika. Ikiwa unapenda kuwa wa kimataifa, basi fuatilia mbinu 10 za uhakika zitakazo kuwezesha kufahamu Kiingereza/English kwa muda mfupi. 1. Penda na furahia Kiingereza Ili uweze kufanya au kujifunza kitu chochote ni lazima kwanza ukipende. Ikiwa unataka kufahamu Kiingereza kwa muda mfupi ni lazima ukipende kwani ndipo utaweza kujifunza kila mara bila kuchoka wala kukata tamaa. Kila mara jihamasishe kwa kutafakari manufaa utakayoyapata baada ya kufahamu Kiingereza vizuri. 2. Jifunze Kiingereza kila siku Huwezi kufahamu Kiingereza kama hutojifunza kila si...
Rangi 11 za Mkojo na Maana Zake Kwenye Mwili wako

Rangi 11 za Mkojo na Maana Zake Kwenye Mwili wako

Afya
Ni watu wachache sana ndiyo hupenda kuchunguza rangi za mikojo yao. Lakini kiuhalisia rangi hizi zinaeleza mambo mengi kuhusu afya yako; Ikiwa hunywi maji ya kutosha au una maradhi fulani, basi utafahamu kupitia rangi hizi. Hapa chini kuna mchoro-taarifa (infographic) unaoonyesha kinachomaanishwa na rangi 11 za mkojo na nini unachotakiwa ufanye. Naamini sasa umepata maarifa; pia naamini sasa hutopuuzia tena kuchunguza mkojo wako. Je una swali au maoni yoyote? Tafadhali tuandikie hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Usisahau pia kufuatilia ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.