Fahamu Hili Archives - Page 9 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Madhara 6 ya Kutumia Dawa Bila Ushauri wa Kitaalamu

Madhara 6 ya Kutumia Dawa Bila Ushauri wa Kitaalamu

Afya
Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari. Kutokana na uwepo wa maduka ya dawa baridi, watu wengi wanapojisikia kuwa wagonjwa, hununua dawa kwenye maduka hayo na kuanza kuzitumia. Ni ukweli usiopingika kuwa dawa zimetengenezwa ili kutibu maradhi fulani ambayo yatabainika kwa mgonjwa baada ya uchunguzi wa kitaalamu. Hivyo matumizi ya dawa bila kufanya uchunguzi wa kitaalamu yanaweza kuwa na madhara makubwa kwenye afya yako. Fahamu madhara 6 ya kutumia dawa bila ushauri au uchunguzi wa kitaalamu. 1. Huongeza sumu mwilini Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo kimsingi ni sumu zinazoua vimelea vya magonjwa. Hivyo kutumia dawa bila vipimo kunaku...
Mbinu 10  za Kuongeza au Kuvutia Wateja Kwenye Biashara

Mbinu 10 za Kuongeza au Kuvutia Wateja Kwenye Biashara

Biashara na Uchumi
Haijalishi huduma au bidhaa yako ni kubwa kiasi gani, biashara yako haitazalisha pesa kama wateja hawatakuwa tayari kununua bidhaa au huduma yako. Hakuna wateja, hakuna biashara. Tatizo la kukosa wateja hukabili sana biashara ndogo, na hata kusababisha biashara hizo kufa. Siyo kwamba wateja hawapendi kununua bidhaa za biashara hizi, bali tatizo kubwa ni mbinu duni za kujitangaza na masoko. Katika makala hii nitakueleza mbinu 10 rahisi na za gharama nafuu ambazo unaweza kuzitekeleza na ukaongeza au kuvutia wateja zaidi kwenye biashara yako. 1. Lugha nzuri Katika mambo yanayowapotezea wafanyabiashara wengi wateja ni lugha mbaya kwa wateja. Hakuna mteja anayependa kupokelewa au kujibiwa vibaya. Hakikisha unazungumza na wateja wako kwa namna bora ambayo wataona unawajali, unawathamini na ...
Faida 5 za Kuvaa Kofia Ngumu (Helmet)

Faida 5 za Kuvaa Kofia Ngumu (Helmet)

Usafiri na Safari
Usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda, umeenea sana hivi leo. Karibu kila mtu ameshatumia au anatumia usafiri huu. Hata hivyo kumekuwepo na changamoto kubwa ya ajali zitokanazo na pikipiki. Kutokana na tatizo hili, mara nyingi tumekuwa tukisikia vyombo mbalimbali hasa vile vya usalama barabarani, vikisisitiza juu ya kuvaa kofia ngumu (helmet). Je kuna manufaa gani yaliyoko kwenye swala hili? Ni ukweli usiopingika kuwa kuna manufaa makubwa sana kwenye swala la kuvaa kofia ngumu. Karibu nikushirikishe faida 5 za kuvaa kofia ngumu. 1. Unatii sheria Kabla ya kuzungumzia faida binafsi anazozipata mtu anayevaa kofia ngumu; kwanza anapata faida ya kutii sheria. Hii ina maana kuwa ataepuka adhabu ya tozo au kifungo. Sheria zimewekwa ili zifuatwe, hivyo kutokufuata au kutii sheri...
Sababu 6 za Kwanini Hutakiwi kununua Followers na Likes

Sababu 6 za Kwanini Hutakiwi kununua Followers na Likes

Tovuti na Blogu
Nitatumia maneno haya kwenye makala hii: Followers - Wafuatiliaji Likes - Penda au Poa Post - Chapisho Comment - Maoni Kumbuka! Nitatumia pia ukurasa wetu wa Facebook kwa mifano ili uelewe kwa uhalisia zaidi. Inawezekana umeanzisha ukurasa wa Facebook au Twitter, na unashauku kubwa ya kuuendeleza. Lakini tatizo ni kuwa unauona ni dhaifu kutokana na kukosa likes au followers. Mara moja wazo linalokuja kwenye akili yako ni kutafuta njia za kuongeza likes na followers, ama kwa kununua au kwa njia nyingine. Unapofikiri hivyo jiulize maswali haya: Maana ya likes na followers kwenye ukurasa wangu ni nini? Je lengo langu ni nini? Je likes na followers vitanisaidia kufikia lengo? Je followers au likes za kununuliwa zinatokana na nini? Je kurasa au watu ...
Maeneo 10 Ambayo ni Marufuku Kubusu au Kukumbatiana Hadharani

Maeneo 10 Ambayo ni Marufuku Kubusu au Kukumbatiana Hadharani

Maarifa
Wakati kwenye maeneo mengine kubusu au kukumbatiana kati ya mwanamke na mwanaume ni jambo la kawaida, kwenye maeneo mengine ni kosa kubwa. Baadhi ya nchi za kimagharibi zimewapa raia wake uhuru kiasi cha kuweza hata kufanya matendo ya faragha hadharani. Lakini baadi ya nchi, hasa zile zenye misingi imara ya kidini, zimepiga marufuku kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani. Kwa kuwa lengo letu ni kukupa maarifa, basi fahamu maeneo 10 ambayo ni marufuku kubusu au kukumbatiana baina ya mwanamke na mwanaume hadharani. 1. Qatar Qatar ni nchi yenye utamaduni wa Kiislamu ambayo hairuhusu mtu kubusu au kukumbatiana hadharani. Hata hivyo matendo haya baina ya wanafamilia au marafiki wa jinsia moja (wasio mashoga) siyo jambo baya. 2. India Kwa mujibu wa sheria za India, mtu atak...
Faida 15 za Kula Tunda la Embe

Faida 15 za Kula Tunda la Embe

Mtindo wa Maisha
Embe ni tunda linalofahamika na kupendwa na watu wengi. Watu hula tunda hili moja kwa moja au kulitumia kutengeneza sharubati (juice). Kwa hakika ikiwa haupendi au haufahamu umuhimu wa tunda hili katika afya yako ni wakati wa kujifunza kitu sasa. Je unajua matunda ni muhimu kwa ajili ya afya yako? Karibu nikushirikishe faida 15 za kula tunda la embe. 1. Huboresha metaboli Embe ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa kiasi kikubwa. Nyuzinuzi zinahitajika sana katika kufanya mchakato wa metaboli (mwili kutumia vrutubisho kujipa nguvu) kwenda vizuri. 2.Huboresha afya ya macho Kula embe kutakunufaisha kwa kulinda macho yako dhidi ya kudhoofu kwa misuli ya macho. Embe ni chanzo kizuri cha vitamini A ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho. Soma pia: Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo W...
Mambo 17 ya Kuzingatia Kabla ya Kusafiri Kwenda Nchi Nyingine

Mambo 17 ya Kuzingatia Kabla ya Kusafiri Kwenda Nchi Nyingine

Usafiri na Safari
Safari ni jambo linalohitaji maandalizi, hasa safari ya kwenda nchi nyingine. Watu wengi hujikuta wakiingia kwenye matatizo mbalimbali kutokana na kutokufahamu mambo ya kuzingatia kabla ya safari. Ikiwa umeshasafiri, au ni mara yako ya kwanza kusafiri kwenda nchi nyingine, basi karibu nikushirikishe mambo 17 ya kuzingatia kabla ya kusafiri kwenda nchi nyingine. 1. Hakiki muda wa mwisho wa pasi yako ya kusafiria Kama una pasi ya kusafiria, hakikisha muda wake wa matumizi haujakaribia kwisha. Hakikisha pia kurasa zilizo wazi hazijakaribia kwisha. Kumbuka kuwa baadhi ya nchi haziruhusu watu kuingia au kutoka kwa kutumia pasi za kusafiria zilizobakiza muda wa miezi 6 kuisha muda wake. 2. Fahamu nyaraka zinazohitajika Kila nchi ina taratibu na sheria zake. Hivyo hakikisha nyaraka ...
Njia 10 za Kuepuka Madeni

Njia 10 za Kuepuka Madeni

Kipato, Tija
Hakuna mtu anayependa kuwa na madeni, lakini mara nyingi watu hujikuta katika madeni makubwa. Kwa kiasi kikubwa watu wengi huingia kwenye madeni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi kuliko kipato. Madeni siyo kitu kizuri hasa ikiwa hayatalipwa kwa wakati. Swala la kuepuka madeni ni swala linalohitaji maamuzi sahihi ya kifikra pamoja na mikakati stahiki. Je unapenda kuepuka au kupunguza kiwango chako cha madeni? Karibu nikufahamishe njia 10 za kuepuka madeni. 1. Jiwekee bajeti binafsi Utawasikia watu wakikosoa bajeti ya serekali lakini hawana bajeti zao binafsi. Bajeti binafsi ni muhimu kwani hukuwezesha kupanga juu ya mapato na matumizi yako. Ili kuepuka madeni, ni muhimu kuweka bajeti binafsi ambayo itakuongoza juu ya matumizi yako ya pesa ili usije ukatumia kul...
Shindano la Picha la Wikipedia – Wiki Loves Africa 2017

Shindano la Picha la Wikipedia – Wiki Loves Africa 2017

Fursa
Kama Fahamuhili.com tulivyoahidi kwenye ukurasa wa kutuhusu, tutakuwa tukikufahamisha fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuboresha uchumi na maisha yako kwa ujumla. Karibu tukufahamishe fursa ya shindano la picha linaloendeshwa na tovuti ya Wikipedia. Ikiwa wewe una uwezo wa kupiga picha, video au kurekodi sauti nzuri yenye ubora wa hali ya juu, basi unaweza kushiriki shindano hili. Maelezo kuhusu shindano Wikipedia kwa kutambua nafasi na umuhimu wa Afrika, wameanzisha shindano ambalo washiriki watatakiwa kutuma picha, video au hata sauti za watu wakiwa kazini kutoka barani Afrika. Washindi wanaweza kujishindia fedha na zawadi nyingine kemkem. Ni lini shindano litafanyika? Shindano limeanza tarehe 1 Oktoba 2017 na litafungwa mnamo tarehe 30 Novemba 2017. Washindi watatangazwa ...
Kampuni 7 za China Zilizofanikiwa Sana Barani Afrika (2017)

Kampuni 7 za China Zilizofanikiwa Sana Barani Afrika (2017)

Nyinginezo
China ni moja kati ya nchi zenye makampuni mengi yaliyowekeza barani Afrika. Takwimu zinaeleza kuwa zaidi ya kampuni 10,000 za kichina zipo barani Afrika kwa sasa. Inaelezwa kuwa kampuni hizo zimefanikiwa sana na kujipatia faida kubwa kwa muda mfupi. Takwimu hizo zinaeleza kuwa robo ya kampuni hizo zilirudisha mtaji wake ndani ya miezi 12, wakati asilimia 50 zilitumia takriban miaka mitatu au pungufu kurudisha mtaji wake. Fahamuhili tunapenda kukupa maarifa, hivyo fahamu kampuni 7 za China zilizofanikiwa sana barani Afrika kwa mwaka 2017. 1. TECNO Hii ni kampuni ya kuuza vifaa vya kielektroniki, hasa simu kutoka China. Inaelezwa kuwa kampuni hii imefanikiwa kushika asilimia 40 ya soko katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki. Pamoja na ushindani mkubwa kutoka kwa wazalishaj...