Shindano la Picha la Wikipedia - Wiki Loves Africa 2017 - Fahamu Hili
Friday, April 19Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Shindano la Picha la Wikipedia – Wiki Loves Africa 2017

Washirikishe Wengine Makala Hii:

Wiki Loves Africa 2017

Kama Fahamuhili.com tulivyoahidi kwenye ukurasa wa kutuhusu, tutakuwa tukikufahamisha fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuboresha uchumi na maisha yako kwa ujumla.

Karibu tukufahamishe fursa ya shindano la picha linaloendeshwa na tovuti ya Wikipedia. Ikiwa wewe una uwezo wa kupiga picha, video au kurekodi sauti nzuri yenye ubora wa hali ya juu, basi unaweza kushiriki shindano hili.

Maelezo kuhusu shindano

Wikipedia kwa kutambua nafasi na umuhimu wa Afrika, wameanzisha shindano ambalo washiriki watatakiwa kutuma picha, video au hata sauti za watu wakiwa kazini kutoka barani Afrika. Washindi wanaweza kujishindia fedha na zawadi nyingine kemkem.

Ni lini shindano litafanyika?

Shindano limeanza tarehe 1 Oktoba 2017 na litafungwa mnamo tarehe 30 Novemba 2017. Washindi watatangazwa mnamo wezi Februari 2018.

Zawadi

 • Mshindi wa kwanza $600
 • Mshindi wa pili $400
 • Mshindi wa tatu $200
 • Mpangiliaji $200
 • Insha ya picha ya wanawake wakiwa kazini: $200
 • Insha ya picha ya mambo adimu, utamaduni na sanaa au watu wakiwa kazini: $200

Zawadi nyingine ni Wiki Loves Africa powerpack  pamoja na Tisheti

Vigezo na Masharti

Kuna vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa ili kuwa mshindi.

 • Picha zote ni lazima ziwe zimepigwa na mtu anayezituma. Zinaweza kupakiwa (uploaded) moja moja au zote kwa mkupuo.
 • Upakiaji wa picha ni lazima ufanyike kati ya tarehe 1 Oktoba hadi 30 Novemba 2017. Picha zililzopigwa wakati wowote zinaweza kupakiwa; jambo la kuzingatia ni kuhakikisha mtumaji au mpakiaji ana umiliki kamili wa picha hizo.
 • Picha hazitakiwi kuwa na maandishi, nembo au alama yoyote (watermarks). Picha zote zitakuwa chini ya leseni ya bure ya Creative Commons.
 • Picha zote zitawekwa chini ya kategoria ya Wiki Loves Africa 2017. Hata hivyo mshiriki anaweza kupendekeza kategoria nyingine wakati wa upakiaji.
 • Mshiriki ni lazima aruhusu au awezeshe barua pepe kwenye Wikimedia Commons ili Wikipedia waweze kuwasiliana naye.

Kuhusu video

Ikumbukwe pia Wikipedia wanapokea video na sauti katika shindano hili. Hivyo unaweza kutuma mafaili ya aina hizi.

 • .ogg
 • .ogm
 • .webm

Kutokana na sababu za haki miliki, Wikipedia hawatapokea aina (format) nyingine tofauti na hizi zilizoorodheshwa hapa.

Mfano wa picha kama unazoweza kutuma:

Unaweza kusoma maelezo zaidi ya shindano hili hapa.

Je bado unasubiri nini? Ikiwa unauwezo wa kushiriki, shiriki sasa kwani inaweza kuwa ndiyo nafasi yako ya kushinda. Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini na usisahau kuwashirikisha wengine fursa hii. Unaweza pia kulike ukurasa wetu wa Facebook ili kufahamu mengi zaidi.

0 0 votes
Pendekeza Ubora wa Makala Hii
Washirikishe Wengine Makala Hii:
Subscribe
Notify of
guest

0 Maoni
Inline Feedbacks
View all comments
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x