Fahamu Hili Archives - Page 6 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Nyumba

Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Nyumba

Nyumba na Makazi
Kila binadamu anahitaji nyumba kwa ajili ya makazi. Kutokana na umuhimu wa nyumba, baadhi ya watu wamekuwa wakiamua kujenga nyumba zao wenyewe au kununua nyumba zilizojengwa tayari. Hata hivyo, bado watu hawapati nyumba bora zinazokidhi mahitaji yao kutokana na sababu mbalimbali. Ni wazi kuwa ili upate nyumba bora kuna mambo ambayo unatakiwa kuyafahamu na kuyazingatia. Ikiwa unataka kununua nyumba kwa ajili ya matumizi yako, basi fahamu mambo 10 ya kuzingatia kabla ya kununua nyumba. 1. Tambua mahitaji yako Mara nyingi nyumba hujengwa kwa kutegemea mahitaji ya mmiliki. Hivyo kabla hujanunua nyumba bainisha mahitaji yako kwa nyumba husika. Ikiwa unataka kuitumia kuishi basi hakikisha inakufaa, ikiwa pia unataka kuitumia kwa matumizi ya kibiashara, hakikisha inakidhi mahitaji ...
Tabia 10 za Watu Waliojipanga

Tabia 10 za Watu Waliojipanga

Maendeleo Binafsi
Kuna watu ukitazama utendaji wao wa kazi au maisha yao yanavutia. Ukitazama jinsi wanavyotekeleza mambo yao unaweza kufikiri kuna mfumo fulani unawaendesha au kuwaongoza kwa siri. Mara nyingi watu hawa huwa na mfuatano au mpangilio mzuri na unaoeleweka wa kazi au maamuzi yao. Kwa kifupi watu hawa hufanikiwa sana na ndiyo huitwa watu waliojipanga. Inawezekana nawe unahitaji kufahamu sifa za watu waliojipanga ili ujifunze jambo. Basi karibu nikushirikishe tabia 10 za watu waliojipanga. 1. Wanaandika kila kitu Kuandika vitu ni njia mojawapo ya kutekeleza mambo kwa mpangilio. Watu waliojipanga huandika mambo yote wanayotakiwa kufanya ili wasiyasahau na wanyafanye kwa wakati. Watu waliojipanga hukagua pale walipoandika mara kwa mara ili kuona wamekamilisha lipi na lipi bado hawaj...
Fahamu Faida 10 za Kuota Jua Kiafya

Fahamu Faida 10 za Kuota Jua Kiafya

Mtindo wa Maisha
Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua ni kitu mojawapo ambacho huwa tunakiona kila siku, lakini ni mara chache tumelichunguza. Kwa hakika kuna umuhimu mkubwa wa jua kwa mimea na viumbe vingine akiwemo binadamu. Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya, zimebaini kuwa kuna manufaa makubwa ya kuota jua angalau kwa kiasi fulani kila siku. Kwa kuwa najua unapenda afya bora, basi fahamu faida 10 za kuota jua kiafya. 1. Kuua bakteria Jua linaweza kutumiwa kuua bakteria mbalimbali katika majeraha na ngozi. Tiba hii iligunduliwa na mshindi wa tuzo ya Nobel Niels Finsen. Tiba hii ilitumiwa kuponya vidonda vya wanajeshi wa Kijerumani baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia. 2. Huondoa msongo wa mawazo Inakadiriwa mtu a...
Mambo 7 ya Kuzingatia ili Kuhifadhi Nyaraka Muhimu Salama

Mambo 7 ya Kuzingatia ili Kuhifadhi Nyaraka Muhimu Salama

Tija
Katika maisha yetu ya kila siku hatuwezi kuepuka kuwa na nyaraka mbalimbali. Baadhi ya nyaraka ni za muhimu sana kwetu kiasi cha kutoweza kuzipata tena iwapo zitaharibika au kupotea. Ni ukweli usiopingika kuwa nyaraka kama vile vyeti ya taaluma, bima, hati za kusafiria, leseni, wosia, vyeti vya ndoa, talaka, mikataba, hati za nyumba na viwanja ni baadhi ya nyaraka zinazotakiwa kutunzwa sana. Kutokana na watu wengi kutofahamu umuhimu wa nyaraka mbalimbali au kutokuzihifadhi vyema, wengi wamejikuta kwenye matatizo makubwa baada ya nyaraka zao muhimu kuharibika au kupotea. Ikiwa basi unataka kuweka nyaraka zako salama, karibu nikushirikishe mambo 7 ya kuzingatia ili kuhifadhi nyaraka muhimu salama. 1. Tumia kabati au sanduku maalumu ya kuhifadhi nyaraka Zipo kabati na masan...
Mambo 9 ya Kuzingatia Wakati Wa Kuchagua Kampuni ya Matangazo Kwenye Blog

Mambo 9 ya Kuzingatia Wakati Wa Kuchagua Kampuni ya Matangazo Kwenye Blog

Tovuti na Blogu
Kuweka matangazo kwenye blog ni njia mojawapo ya kupata pesa kupitia blog ambayo inafahamika kwa watu wengi. Kuna baadhi ya blog au tovuti ambazo zimefanikiwa kutengeneza pesa nyingi sana wakati nyingine zikiwa hazipati pesa za maana au hazipati kabisa kupitia njia hii ya matangazo. Kwa hakika watu wengi huchagua njia ya kuweka matangazo ya kampuni mbalimbali kwenye blog zao ili kujipatia kipato kutokana na kutokufahamu njia nyingine za kupata pesa au kutokana na kuona blog nyingine zikitumia njia hiyo. Ikiwa basi wewe ni mmojawapo wa watu wanaotaka kutumia njia ya kuweka matangazo kwenye blog ili kupata pesa, basi fahamu mambo 9 ya kuzingatia wakati wa kuchagua kampuni ya matangazo kwenye blog au tovuti yako. 1. Wakati sahihi Kuna wakati sahihi wa kujiunga na kampuni ya matang...
Njia 12 za Kupunguza Gharama za Uendeshaji wa Kampuni

Njia 12 za Kupunguza Gharama za Uendeshaji wa Kampuni

Biashara na Uchumi
Mbinu mojawapo ya kuongeza faida katika kampuni au biashara yako ni kwa kupunguza matumizi ya kampuni yako. Suala la kupunguza matumizi ya pesa ni muhimu zaidi hasa pale ambapo kampuni inakuwa inakabiliwa na changamoto za kifedha. Kwa hakika kupunguza matumizi ya uendeshaji wa kampuni ni jambo linalowezekana ikiwa mikakati na hatua stahiki zitachukuliwa. Ikiwa unapenda kufahamu jinsi ya kupunguza gharama za uendeshaji wa kampuni, basi fahamu njia 12 unazoweza kuzitumia kufanikisha lengo hili. 1. Tathimini upya matumizi Kuna matumizi mbalimbali kwenye kila kampuni lakini siyo yote ni ya muhimu. Matumizi mengine ni ya lazima lakini yamepewa kipaumbele kuliko umuhimu wake. Kwa kupunguza matumizi ya vitu kama vile simu, umeme, maji, mafuta au hata intaneti, kutaokoa kiasi kikubw...
Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla na Wakati wa Kuendesha Gari Umbali Mrefu

Mambo 10 ya Kuzingatia Kabla na Wakati wa Kuendesha Gari Umbali Mrefu

Usafiri na Safari
Kuendesha gari ni suala linalohitaji umakini na utulivu mkubwa, hasa pale unapoendesha gari umbali mrefu. Mara kwa mara kumeshuhudiwa ajali mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na madereva kutokuzingatia kanuni muhimu katika utumiaji wa vyombo vya usafiri. Ili kuhakikisha usalama wako pamoja na watumiaji wengine wa barabara, yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyazingatia kabla na wakati wa kuendesha gari umbali mrefu. 1. Kagua na andaa gari Kabla ya safari yoyote gari linahitaji kukaguliwa na kuandaliwa, hasa kabla ya safari ndefu. Kuna mambo kadhaa unayohitaji kuyakagua kwenye gari lako: Kagua hali na ubora wa magurudumu. Hakikisha magurudumu yamejaa vizuri na hayajazeeka. Kagua mafuta lainishi (oil). Hakikisha gari yako ina mafuta lainishi ya kutosha tena ya ubora unaotakiwa...
Kikombe cha Kisasa Kinachozuia Vitu Kumwagika

Kikombe cha Kisasa Kinachozuia Vitu Kumwagika

Teknolojia
Lengo kubwa la teknolojia ni kurahisisha maisha pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi. Kila siku kumekuwa kukibuniwa teknolojia mbalimbali hasa kwa lengo la kutatua matatizo mbalimbali yanayomkabili mwanadamu. Inawezekana umewahi kupoteza nyaraka zako muhimu au hata kuharibu vifaa vyako vya thamani kama vile simu au kompyuta kutokana na kumwagikiwa vimiminika kama vile maji, kahawa au chai. Teknolojia kutoka MightyMug inakuja na kikombe maalumu ambacho huzuia kinywaji kilichoko ndani yake kumwagika. Inawezekana una mtoto mkorofi au unafanya kazi kwenye eneo lenye mitikisiko mingi; sasa kwa kutumia kikombe kutoka MightyMug utaepusha vitu vyako vya thamani kumwagikiwa vimiminika. Sifa  za kikombe cha MightyMug Kikombe cha MightyMug kina uwezo wa kujishikiza kw...
Tofauti 10 Kati ya Mwajiriwa na Mjasiriamali

Tofauti 10 Kati ya Mwajiriwa na Mjasiriamali

Ujasiriamali
Kwa hakika kuna tofauti kubwa kati ya mwajiriwa na mjasriamali; tofauti hii inahusisha tabia, fikra, maamuzi au hata matendo. Kuna baadhi ya watu ni wajasiriamali kwa mwonekano lakini kitabia ni waajiriwa; wapo pia wengine ni waajiriwa kimwonekano lakini ni wajasiriamali kitabia. Ikiwa basi unataka kuwa mjasiriamali, ni muhimu ufahamu tofauti 10 za msingi zilizopo kati ya mwajiriwa na mjasiriamali. 1. Mwajiriwa hupumzika kwenye likizo lakini mjasiriamali hutumia likizo kufanya kazi zaidi Kwa kawaida waajiriwa hufurahia muda wa likizo kwa sababu ndipo hupata muda wa kupumzika. Hali ni tofauti kwa mjasiriamali kwani hana likizo, na ikiwa ni mjasiriamali aliyeajiriwa, basi atatumia likizo yake kuendeleza mradi au biashara yake. 2. Mwajiriwa hulenga kupanda cheo lakini mjasiriamal...
Sababu 10 za Kwa nini Unatakiwa Kuacha Kuvuta Sigara

Sababu 10 za Kwa nini Unatakiwa Kuacha Kuvuta Sigara

Afya
Kuna baadhi ya tabia kuzianza ni rahisi sana, lakini kuziacha kunakuwa ni kugumu. Watu wengi hasa vijana, hushawishiwa na marafiki kuingia kwenye tabia kama vile unywaji wa pombe, uvutaji sigara au kutumia madawa ya kulevya bila kufahamu madhara yake. Hakika kuna madhara mengi sana yatokanayo na uvutaji wa sigara kiafya, kiakili, kijamii na kiuchumi. Ikiwa basi unataka kufahamu sababu za kwanini unatakiwa kuacha kuvuta sigara, basi karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe sababu 10 za kuacha kuvuta sigara. 1. Unaokoa pesa Moja kati ya mambo yanayowapotezea watu pesa ni tabia kama vile uvutaji wa sigara. Kwa kuacha kuvuta sigara utaweza kuokoa pesa ambazo huwa unazitumia kwa ajili ya kununua sigara, na kuzitumia kufanya mambo mengine yenye manufaa kwako. Soma pia: Njia 10 Zitakaz...