
Makosa 15 ya Kuepuka Katika Malezi ya Watoto
Swala la malezi ya watoto ni swala nyeti, pana, gumu, na lenye changamoto nyingi; hivyo linahitaji umakini mkubwa na maarifa stahiki. Kutokana na umuhimu huu basi, ni wazi kuwa changamoto au matatizo mengi ya kimalezi yanayotokea kwenye maisha ya watoto yanatokana na makosa yanayofanywa na wazazi katika malezi. Pamoja na kwamba hakuna kanuni ya malezi, lakini yapo makosa ambayo wazazi wanapaswa kuyaepuka katika swala la malezi ili kuhakikisha watoto wao wanakuwa katika maadili na misingi sahihi. Karibu nikufahamishe makosa 15 ambayo kila mzazi au mlezi anatakiwa kuyaepuka katika malezi ya kilasiku ya watoto.
1. Kumfurahisha mtoto
Kumfurahisha mtoto ni muhimu kufanywa na kila mzazi au mlezi, lakini ni lazima kuwe na kiasi. Wazazi wengi wamekuwa wakifanya kosa la kutaka kuwafa...










