
Vitu Vinne Vinavyokufanya Usikamilishe Kazi Zako
Hakuna mtu anayependa kushindwa kukamilisha kazi au kitu alichokianza. Hata hivyo mara nyingi kutokukamilisha kazi hutokea kwa watu wengi. Ni ukweli usiopingika kuwa zipo sababu kadha wa kadha zinazosababisha tatizo hili. Karibu nikufahamishe vitu vinne vinavyokufanya usikamilishe kazi zako.
1. Usingizi
Kuna usemi usemao “usingizi ni mlango wa umaskini”; kwa hakika kulala kupita kiasi ni jambo ambalo litakupotezea muda mwingi pamoja na ufanisi. Unapolala sana unakosa muda wa kutosha kutimiza majukumu yako. Pia kulala muda mrefu hukufanya uamke ukiwa umechoka na kukufanya ukose ari na motisha wa kufanya kazi. Soma pia: Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi.
2. Intaneti na simu
Maendeleo yana manufaa yake na hasara zake. Kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, watu wengi...










