
Faida 20 za Kula Parachichi
Parachichi ni aina ya kipekee ya tunda. Matunda mengi kwa asili ni wanga lakini parachichi limejaa mafuta yenye manufaa makubwa kiafya. Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimebaini kuwa tunda la parachichi limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu. Ikiwa unapenda kuwa na afya bora kwa kula tunda la parachichi, basi karibu nikushirikishe faida 20 za kula tunda la parachichi.
1. Parachichi limejaa virutubisho mbalimbali
Parachichi ni tunda la pekee ambalo limebeba virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa ajili ya miili yetu. Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi ni: Kalori 240 (184 inatokana na mafuta)
Miligramu 11 za sodiamu
Gramu 13 za wanga
Gramu 10 za nyuzinyuzi za lishe
Gramu 1 tu ya sukari
Vitamini K: asilimia 26
Vitamini...