
Njia 7 Bora za Kushinda au Kukabiliana na Hofu
Watu wengi wanakabiliwa na kuathiriwa na hofu katika maisha yao kwa namna moja au nyingine. Hofu hizi zinaweza kusababishwa na mazingira, mtu, kitu au hata sababu za kisaikolojia. Hofu isiposhughulikiwa kwenye maisha inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya mtu husika. Wengi wanatamani kukabiliana na hofu lakini bado hawajui namna ya kukabili hofu zinazowakumba. Soma pia: Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu. Je uko tayari kushinda hofu sasa? Karibu nikushirikishe njia 7 ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hofu maishani mwako.
1. Punguza au ondoa mawazo na imani potofu
Wakati mwingine watu wanapata hofu kutokana na imani au fikra potofu pekee. Kwa mfano unaogopa kinyonga kwa sababu umesikia kuwa kikikugusa utatokwa na ngozi au kufa; je una uhakika juu ...










