Kornelio Maanga, Author at Fahamu Hili - Page 7 of 17
Friday, March 27Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Author: Kornelio Maanga

Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Njia 10 za Kuepuka Majanga ya Moto Kwenye Nyumba

Njia 10 za Kuepuka Majanga ya Moto Kwenye Nyumba

Nyumba na Makazi
Kwa siku za usoni kumekuwa na matukio mengi ya majanga ya moto. Matukio haya husababisha uharibifu mkubwa wa mali au hata kugharimu maisha ya watu. Kwa hakika kuunguliwa na nyumba au mali zako unazozipenda ni jambo baya ambalo usingependa litokee. Kutokana na mazingira na miundombinu duni ya majengo, majanga ya moto yameendelea kuwakumba watu wengi. Hata hivyo zipo njia kadhaa unazoweza kutumia kukabili majanga ya moto. Karibu ufuatilie makala hii ili nikushirikishe njia 10 za kuepuka majanga ya moto kwenye nyumba pamoja na tahadhari unazoweza kuchukua. 1. Tumia mfumo bora na salama wa umeme Majanga mengi ya moto husababishwa na hitilafu zinazotokana na mifumo duni ya umeme. Kutokana na ukosefu wa elimu au uhaba wa pesa, watu wengi hutumia vifaa duni wakati wa kuweka umeme k...
Njia 9 za Kutangaza Biashara Yako Bila Pesa

Njia 9 za Kutangaza Biashara Yako Bila Pesa

Biashara na Uchumi
Matangazo ni swala muhimu kwa kila biashara. Tatizo linatokea pale ambapo biashara inashindwa kumudu gharama za matangazo, hasa matangazo ya gharama kubwa. Naamini wewe kama mjasiriamali unafahamu kuwa kuna wakati bajeti ya biashara inakuwa imebana. Hivyo swala la kujitangaza linakuwa na changamoto. Fuatilia makala hii kwa karibu ili nikufahamishe njia 9 unazoweza kuzitumia kutangaza biashara yako bure au kwa gharama nafuu sana. 1. Tumia tovuti Tovuti au blog ni njia rahisi na ya gharama nafuu ya kujitangaza. Ikiwa una blog au tovuti ambayo inaidadi nzuri ya watembeleaji, unaweza kuweka tangazo la biashara yako hapo na likaonekana kwa watu wengi zaidi. 2. Tumia mitandao ya kijamii Kama ilivyo wenye njia ya blog, vivyo hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebo...
Madhara 8 ya Kunakili Machapisho kutoka Kwenye Blog au Tovuti Nyingine

Madhara 8 ya Kunakili Machapisho kutoka Kwenye Blog au Tovuti Nyingine

Tovuti na Blogu
Uandishi ni kazi ngumu na inayochosha, uandishi unahitaji kutafiti, muda, maarifa sahihi na hata rasilimali fedha. Kutokana na sababu hizi wamiliki wengi wa blog au tovuti hujikuta wakinakili maudhui kutoka kwenye blog au tovuti nyingine. Swala la kunakili maudhui kutoka kwenye blog au tovuti nyingine limekuwa likisababishwa pia na kukosa lengo, uvivu, kukosa ubunifu pamoja na kutokujua madhara ya kunakili. Ikiwa wewe ni blogger au mmiliki wa tovuti, basi karibu nikushirikishe madhara 8 yatokanayo na kunakili machapisho (post) kutoka kwenye blog au tovuti nyingine. 1. Hukufanya uonekane duni Unaponakili machapisho kutoka kwenye tovuti au blog nyingine, moja kwa moja unawaambia wasomaji wako kuwa huna cha kuwaambia kama usipomnakili mtu mwingine. Hivyo wasomaji wako watak...
Mambo 10 ya Kuepuka Unapokuwa Kwenye Nchi ya Kigeni

Mambo 10 ya Kuepuka Unapokuwa Kwenye Nchi ya Kigeni

Usafiri na Safari
Kila mahali pana taratibu na mambo yake. Mtindo wa maisha ulioouzoea kwenye nchi yako ya nyumbani, unaweza usikubalike kwenye nchi ya kigeni. Inawezekana umepanga kutembelea nchi ya kigeni hivi karibuni, au tayari uko kwenye nchi ya kigeni. Karibu nikufahamishe mambo 10 ambayo kama utayaepuka utaweza kukaa kwenye nchi ya kigeni bila tatizo. 1. Kukiuka utamaduni wa nchi husika Kila nchi ina tamaduni na taratibu zake. Kuna nchi haziruhusu kuvaa mavazi fulani au kufanya matendo fulani. Ni vyema ukahakikisha mambo unayoyafanya hayakiuki tamaduni za nchi husika. Kwa mfano nchi nyingi za Kiarabu haziruhusu kubusu au kukumbatiana hadharani baina ya mwanamke na mwanaume. Ukikamatwa ukifanya kosa hili, unaweza kuchukuliwa hatua kali. Soma pia: Maeneo 10 Ambayo ni Marufuku Kubusu au K...
Mambo 10 ya Kuzingatia Unapomtafutia Mtoto Shule

Mambo 10 ya Kuzingatia Unapomtafutia Mtoto Shule

Mahusiano na Familia
Hivi leo kuna shule nyingi, lakini siyo shule zote ni bora au zinafaa kwa ajili ya mtoto wako. Hii ni kutokana na shule nyingi kuanzishwa na kuendeshwa kwa misingi ya kibiashara kuliko huduma. Swala la kuhakikisha mtoto wako anapata elimu bora ni swala la msingi. Hii ni kutokana na nafasi na umuhimu wa elimu kwa maisha ya sasa na ya baadaye ya mtoto. Ikiwa unataka kupata shule nzuri kwa ajili ya mtoto wako, karibu nikufahamishe mambo 10 ya kuzingatia unapomtafutia au kumchagulia mtoto wako shule. 1. Kiwango cha ufaulu Hakuna mzazi au mlezi ambaye anapenda mtoto wake asifanikiwe kwenye masomo. Kufanikiwa kwa mtoto kwa kiasi kikubwa kunategemea kiwango cha ufaulu cha shule. Ni wazi kuwa shule inayofaulisha vyema itakuwa inafundisha vyema pia. Hivyo kagua kwanza matokeo ya miti...
Changamoto 12 za Ujasiriamali na Jinsi ya Kuzikabili

Changamoto 12 za Ujasiriamali na Jinsi ya Kuzikabili

Ujasiriamali
Kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake nyingi. Ni wazi kuwa wajasiriamali wakubwa na wadogo, wote hukutana na changamoto; tofauti yao ni chanzo cha changamoto hizo na njia wanazozitumia kuzikabili. Wajasiriamali wadogo ndiyo wamekuwa wakikabiliwa zaidi na changamoto hizo na hata kupelekea kupoteza biashara au miradi yao. Inawezekana wewe ni mmoja wapo wa wajasiriamali wanaokabiliana na changamoto. Karibu nikushirikishe changamoto 12 za ujasiriamali na jinsi ya kuzikabili. 1. Mtaji Kila biashara inahitaji mtaji ili iweze kujiendesha na kujipanua. Wajasiriamali wengi wanashindwa kuanzisha biashara au kupanua biashara zao kutokana na kukosa mtaji. Suluhisho: Kumbuka! Siyo lazima upate mtaji wote unaouhitaji, unaweza kuanza na mtaji kidogo sana n...
Yafahamu Majengo 10 Marefu Zaidi Duniani

Yafahamu Majengo 10 Marefu Zaidi Duniani

Maarifa
Dunia imeendelea kushuhudia uhaba mkubwa wa rasilimali mbalimbali kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu. Moja ya rasilimali ambazo zimekua adimu sana duniani kwa wakati huu ni ardhi, uhaba wa ardhi umefanya wahandisi kote duniani kuumiza vichwa vyao kufikiri namna ambavyo ardhi iliyopo itatumika vyema na kwa manufaa zaidi kwa wengi. Pamoja na sababu nyingine lukuki, ufinyu wa ardhi umechangia kwa kiasi kikubwa kujengwa kwa majengo marefu na ya kushangaza katika maeneo mbalimbali duniani. Yafuatayo ni majengo kumi marefu zaidi duniani maarufu kama sky scrapers kwa lugha ya kimombo. 10. International Commerce Centre Jengo hili linashika nafasi ya kumi kwa majengo marefu zaidi duniani. Lina urefu wa mita 484 pamoja na ghorofa 108; lilijengwa mwaka 2010. 09. Shanghai worl...
Mbinu 9 za Kuacha Tabia Mbaya

Mbinu 9 za Kuacha Tabia Mbaya

Maendeleo Binafsi
  Tabia mbaya zimekuwa zikiwakabili na kuwatesa watu wengi. Haipingiki kuwa tabia mbaya huwazuia watu wengi kufikia malengo yao kwenye maisha. Tabia kama vile uvivu, ulevi, madawa ya kulevya, uzinzi, matumizi mabaya ya pesa, ugomvi, kupoteza muda, n.k. ni baadhi tu ya tabia ambazo zimekuwa zikiwaathiri watu wengi. Hata hivyo, waathiriwa wa tabia hizi wengi hutamani kuziacha, lakini wanashindwa kufahamu waanzie wapi na watumie njia gani ili kuacha tabia hizo. Ikiwa basi unataka kuboresha maisha yako, karibu nikufahamishe mbinu 9 unazoweza kuzitumia ili kuacha tabia mbaya. 1. Jikumbushe na tafakari madhara ya tabia hiyo Ili kupata motisha wa kuacha tabia mbaya, kila mara jikumbushe na tafakari madhara unayoyapata kutokana na tabia hiyo. Kwa mfano ikiwa ni tabia ya u...
Maswali 10 Muhimu ya Kujiuliza Kabla ya Kuacha Kazi

Maswali 10 Muhimu ya Kujiuliza Kabla ya Kuacha Kazi

Kipato
Wakati wengine wakitafuta kazi usiku na mchana, wengine wanatamani kuacha kazi mara moja. Kutokana na sababu mbalimbali, swala la kuacha kazi linawakabili watu wengi. Mazingira mabaya ya kazi, matatizo ya kifamilia au kiafya yamekuwa chanzo kikubwa cha watu kutamani au kutaka kuacha kazi. Swala la kuacha kazi ni swala nyeti ambalo linahitaji utulivu na maamuzi yenye kuhusisha utafiti na busara kubwa. Wengi huacha kazi kutokana na misukosuko midogo na kujikuta wakiingia kwenye matatizo makubwa zaidi. Ikiwa unataka kuacha kazi unayoifanya ili utafute nyingine au ujiajiri mwenyewe, basi jiulize maswali haya 10 kabla ya kumpungia mwajiri wako mkono. 1. Je unaacha kwa sababu sahihi? Inawezekana umekaripiwa na mwajiri wako kutokana na kosa ulilolifanya, swala hili limekukasirisha ...
Mambo 12 Unayoweza Kujifunza Kutoka kwa Bill Gates

Mambo 12 Unayoweza Kujifunza Kutoka kwa Bill Gates

Hamasa
Kwa mujibu wa Forbes 2017, Bill Gates ndiye mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri unaokadiriwa kuwa dola za Marekani bilioni 86. Bill Gates ndiye mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya Microsoft. Microsoft ni kampuni iliyotengeneza programu endeshi (operating system) maarufu na mashuhuri sana duniani ya Window. Kampuni hii pia inazalisha bidhaa nyingine kama vile vifaa vya michezo ya kielektroniki, pogramu mbalimbali pamoja na vifaa vingine vya kiteknolojia. Kwa hakika Bill Gates ni mtu aliyefanikiwa sana ambaye kila mtu anayetaka kufanikiwa anaweza kujifunza mambo kadhaa kutoka kwake. Kwa kutambua umuhimu wa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, karibu nikushirikishe mambo 12 unayoweza kujifunza kutoka kwa Bill Gates. 1. Anza mapema kadri iwezekanavyo Bill Gates alianza kuj...