Kornelio Maanga, Author at Fahamu Hili - Page 4 of 17
Monday, February 9Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Author: Kornelio Maanga

Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Faida 8 za Kuweka Akiba Unazopaswa Kuzifahamu

Faida 8 za Kuweka Akiba Unazopaswa Kuzifahamu

Kipato
Kuweka akiba ni kanuni mojawapo ya matumizi mazuri ya pesa. Hata hivyo kutokana na watu wengi kutokuwa na matumizi mazuri ya pesa, bado wengi wanashindwa kuweka akiba. Baadhi ya watu hufikiri kuwa ili uweze kuweka akiba ni lazima uwe na pesa nyingi, lakini ukweli ni kuwa kuweka akiba ni maamuzi tu na siyo kuwa na pesa nyingi. Ikiwa umekuwa ukipuuza suala la kuweka akiba na kuliona kuwa halina maana, basi fahamu faida 8 za kuweka akiba. 1. Uhuru wa kifedha Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani. Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye swala la uhuru wa kifedha, ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi. Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kuji...
Nukuu (Quotes) 25 za Malengo Zitakazokuhamasisha

Nukuu (Quotes) 25 za Malengo Zitakazokuhamasisha

Maendeleo Binafsi
Malengo ni muhimu sana kwenye maisha ili yatuongoze kufikia mafanikio yetu au kuwa yule ambaye tunapaswa kuwa. Kwa hakika, ikiwa huna malengo ni wakati wa kujiwekea malengo sasa; na ikiwa unayo basi ni wakati wa kutathimini kama unayaelekea. Kwa kutambua umuhimu wa malengo maishani, karibu nikushirikishe nukuu (quotes) 25 za malengo ambazo zitakuhamasisha kufikia malengo yako. Naamini umefurahia nukuu hizi pamoja na kuhamasika kuendelea kupigania malengo yako. Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazokuhamasisha Maishani Mwako Tafadhali andika maoni yako hapo chini kisha washirikishe wengine makala hii. Unaweza kutufuatilia kwa barua pepe au kwa kulike ukurasa wetu wa Facebook i...
Faida 8 za Kufanya Kazi Kwa Bidii Unazotakiwa Kuzifahamu

Faida 8 za Kufanya Kazi Kwa Bidii Unazotakiwa Kuzifahamu

Tija
Kuna fikra potofu zimejengeka miongoni mwa watu wakidhani kuwa kufanya kazi kwa bidii ni utumwa. Hii ni kutokana na dunia ya sasa kujaa watu wasiopenda kazi na wavivu. Kwa hakika kufanya kazi kwa bidii kuna manufaa mengi sana ambayo watu wengi hawayajui. Huu ni wakati wa kubadili mtazamo wako juu ya kufanya kazi kwa bidii kwa kufahamu faida 8 za kufanya kazi kwa bidii. 1. Utaweza kutumia muda vyema Huwezi kutumia muda vyema kama hutofanya kazi kwa bidii. Ukiwa na bidii katika kufanya kazi, unaweza kufanya kazi za siku nzima ndani ya saa moja au kazi za siku mbili ndani ya siku moja. Hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa bila kutumia muda vyema; muda ni mali, hivyo yakupasa uutumie vyema kwa kufanya kazi kwa bidii. Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumizi ya Muda 2. Kufiki...
Sababu 11 za Kwa nini Utumie WordPres Kwenye Blog Yako

Sababu 11 za Kwa nini Utumie WordPres Kwenye Blog Yako

Tovuti na Blogu
Mara unapotaka kutengeneza blog au tovuti, swali gumu linalokuja kichwani mwako ni njia, teknolojia, mfumo au programu ipi utakayoitumia kutengenezea tovuti au blog yako. Kwa hakika kuna teknolojia mbalimbali zinazoweza kutumiwa kutengeneza blog na tovuti, WordPress kama Content Management System ni mojawapo. WordPress ni programu ya bure (open source software) inayotumika kutengenezea tovuti na blogs ambayo unaweza kuisambaza, kuitumia au hata kuibadilisha bila kizuizi chochote. Unaweza kupakua WordPress na kuihost wewe mwenyewe au kwenye huduma yoyote nzuri ya kuhost website Karibu ufuatilie makala hii nikufahamishe sababu 11 za msingi za kwanini utumie WordPress kwenye blog au tovuti yako. 1. WordPress inatumiwa na zaidi ya asilimia 25 ya tovuti Zaidi ya asilimia 25 za to...
Mambo 8 Yanayosababisha Gari Kuwaka Moto na Jinsi ya Kuyaepuka

Mambo 8 Yanayosababisha Gari Kuwaka Moto na Jinsi ya Kuyaepuka

Usafiri na Safari
Gari ni kifaa au chombo kinachorahisisha usafiri, lakini kinapaswa kutumiwa kwa tahadhari kubwa. Ajali zinazotokana na magari kuwaka moto, mara kadhaa zimekuwa zikisababisha hasara kubwa au hata kugharimu maisha ya watu. Kwa hakika jambo hili si zuri, hivyo kila dereva au mtumiaji wa gari ni muhimu akachukua hatua za tahadhari mapema ili kukabili tatizo hili. Gari kuwaka moto kunaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, fuatilia makala hii kwa karibu ili ufahamu mambo 9 yanayosababisha gari kuwaka moto na jinsi ya kuyaepuka. 1. Kuvuja kwa mafuta Ikiwa gari litavuja mafuta  ni rahisi sana kuwaka moto. Kumbuka mafuta ya gari pamoja na mafuta lainishi (oil) ni rahisi sana kushika moto. Tafiti mbalimbali za ajali zimebaini kuwa kuvuja kwa mafuta ni chanzo kikubwa cha magari kuwaka...
Mambo 6 Unayoweza Kujifunza Kutoka Kwa Mashabiki wa Mpira wa Miguu

Mambo 6 Unayoweza Kujifunza Kutoka Kwa Mashabiki wa Mpira wa Miguu

Hamasa
Mchezo wa mpira wa miguu ulianza takriban kati ya karne ya 2 na ya 3 KB huko China. Mchezo huu umejizolea umaarufu mkubwa na kuwa chanzo cha kipato kwa watu wengi. Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa na watu wengi duniani, inakadiriwa kuwa mchezo huu una mamilioni ya mashabiki kote duniani. Kumeshuhudiwa mashabiki wa mpira wa miguu wakijitoa kwa dhati kushabikia timu zao; jambo hili limewagharimu pesa, muda au hata uhai wao. Kwa mtu yoyote mwenye shauku ya kupata maarifa, anaweza kujifunza kitu kutoka kwa mashabiki wa mpira wa miguu; Ikiwa unapenda maarifa, basi karibu nikufahamishe mambo 6 unayoweza kujifunza kutoka kwa mashabiki wa mpira wa miguu. 1. Mapenzi ya dhati Huwezi ukakosa swala la mapenzi ya dhati kwa timu pamoja na mchezo wenyewe kwa shabiki yeyote yule wa mpira...
Mambo Matano Muhimu ya Kuzingatia Kabla ya Kuomba Mkopo

Mambo Matano Muhimu ya Kuzingatia Kabla ya Kuomba Mkopo

Kipato
Kutokana na kipato cha watu wengi kutokutosheleza mahitaji yao, hujikuta wakilazimika kukopa. Wapo waliofanikiwa sana kwenye mipango yao kutokana na mikopo, lakini wapo pia waliofilisika kutokana na mikopo. Kwa hakika swala la mikopo linahitaji umakini mkubwa pamoja na mipango na mikakati stahiki ili lisije likakuingiza kwenye madeni yasiyokwisha. Ikiwa una mpango wa kukopa, basi fahamu mambo matano muhimu ya kuzingatia kabla ya kuomba mkopo. 1. Bainisha uwezo wako wa kifedha Ili upate na utumie mkopo vyema, ni muhimu ufahamu uwezo wako wa kifedha. Ikiwa uwezo wako wa kifedha ni shilingi milioni moja, ukikopa mkopo wa bilioni 1 hutoweza kuupata wala kuurejesha. Hakikisha unatathimini kipato chako pamoja na uwezo wako wa kutumia pesa ili usije ukatumbukia kwenye madeni. So...
Balabolka: Programu Inayobadili Maandishi au Vitabu Kuwa Sauti

Balabolka: Programu Inayobadili Maandishi au Vitabu Kuwa Sauti

Teknolojia
Kwa kuwa vitabu ni kisima kikubwa cha maarifa, kila mara teknolojia inakuja na mbinu mbalimbali zitakazotuwezesha kuvuna maarifa haya. Ikiwa unapenda kusoma vitabu au una nia ya kusoma vitabu, basi fahamu programu ya Balabolka itakayokuwezesha kusoma maandishi au vitabu kwa sauti au kuvibadili kuwa sauti ili uvisikilize badala ya kuvisoma. Hivyo kwa kutumia programu hii unaweza kusoma vitabu pepe kwa urahisi kabisa na mahali popote bila kizuizi. Badala ya kusikiliza mziki siku nzima sasa unaweza kusikiliza vitabu. Sifa za programu ya Balabolka Ni programu ya BURE Inaweza kusoma vitabu vya lugha mbalimbali kama vile Kiingereza, Kiarabu, Kijerumani, Kifaransa, Kichina, n.k. Inaweza kubadili kitabu kuwa faili la sauti kama vile WAV, MP3, MP4, OGG au WMA Inaweza kusoma...
Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu

Faida 15 za Kusoma Vitabu Unazotakiwa Kuzifahamu

Maendeleo Binafsi
Ni watu wachache sana ndiyo wanaopenda na wanafahamu umuhimu wa kusoma vitabu. Watu wengi hasa waafrika hawapendi kusoma vitabu ikiwa hakuna kinachowalazimisha kufanya hivyo kama vile mtihani, kazi, n.k. Kwa hakika kuna maarifa mengi yaliyofichwa kwenye vitabu; hii ndiyo sababu watu wengi waliofanikiwa husoma au hata kuandika vitabu. Ikiwa unataka kupata maarifa na kuboresha maisha yako kwa njia ya kusoma vitabu, basi fahamu faida 15 za kusoma vitabu. 1. Hukuongezea marifa mapya Lengo kubwa linalowafanya waandishi wa vitabu kuandika vitabu ni kuweka maarifa yao kwenye maandishi. Hivyo kwa kusoma vitabu unapata maarifa mbalimbali yaliyowekwa kwenye kitabu husika. Hivi leo kuna vitabu vinavyohusu takriban kila kitu; kwa hiyo maarifa yoyote unayoyahitaji unaweza kuyapata kwenye...
Faida 7 za Kuwa na Ratiba Binafsi

Faida 7 za Kuwa na Ratiba Binafsi

Tija
Ratiba siyo muhimu tu kwa ajili ya taasisi fulani pekee; ni muhimu pia kwa mtu binafsi. Watu wengi hushindwa kutumia muda wao vyema kutokana na kutokuwa na ratiba nzuri inayoeleweka. Kuweka ratiba kutakuwezesha kupangilia kazi na mipango yako kwa namna ambayo utaweza kuitekeleza vyema. Ikiwa unataka kuwa mwenye tija na ufanisi zaidi, basi fahamu faida 7 za kuwa na ratiba binafsi. 1. Kutumia muda vyema Moja kati ya manufaa makubwa ya kuwa na ratiba ni kuweza kutumia muda vyema. Unapokuwa na ratiba ni vigumu kupata muda ambao haujapangiwa jukumu au kazi kwenye ratiba. Unapokuwa na ratiba muda wako wote utatumika vizuri tena kwa shughuli yenye tija iliyopangwa. Hivyo ni vyema kuhakikisha unajiwekea ratiba na unaifuata ipasavyo. Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa katika Matumiz...