Kornelio Maanga, Author at Fahamu Hili - Page 10 of 17
Friday, March 27Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Author: Kornelio Maanga

Kornelio ni mjasiriamali, mfuasi mkubwa wa masuala ya kompyuta na msanifu mtandao toka mwaka 2008. Amekuwa akifanya kazi mbalimbali zinazohusiana na Teknolojia ya Habari Mawasiliano (TEHAMA), bila kusahau uandishi wa makala kadha wa kadha katika tovuti na blog mbalimbali. Anapenda kujifunza na kuwafundisha watu wengine mambo mbalimbali pamoja na mbinu za kuboresha maisha ya kila siku.
Faida 10 za Kupumzika

Faida 10 za Kupumzika

Mtindo wa Maisha
Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, watu wengi hawapati muda wa kutosha wa kupumzika. Mara nyingi mtu anapozidiwa hupunguza zaidi muda wa kupumzika ili akamilishe majukumu yake. Ni wazi kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kupumzika, ndiyo maana hawatengi muda wa kutosha wa kupumzika. Ni ukweli usiopingika kuwa kupumzika kuna manufaa makubwa sana kwenye miili na utendaji wetu wa kazi kila siku. Ikiwa unataka kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida 10 za kupumzika. 1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu Ubongo wa mwanadamu unahitaji kupumzika ili uweze kujijenga na kufanya kazi vyema. Ikiwa mtu hatapata muda wa kutosha wa kupumzika, uwezo wake wa kutunza kumbukumbu utapungua. Pia utafiti uliofanyika umebaini kuwa kutokupumzika huongeza kiasi fulani...
Mambo 15 ya Kufanya ili Kuwa Bora Zaidi

Mambo 15 ya Kufanya ili Kuwa Bora Zaidi

Maendeleo Binafsi
Kama mtu mwenye shauku kubwa ya maendeleo binafsi, kila siku huwa nachunguza njia bora za kunifanya niwe bora zaidi. Naamini wewe pia unapenda kuwa bora zaidi ili uongeze tija na ufanisi wako. Karibu nikufahamishe mambo 15 ambayo unaweza kuyafanya kuanzia sasa ili uweze kuwa bora zaidi. 1. Soma vitabu Vitabu ni chanzo kikubwa cha hekima; Kadri unavyosoma vitabu ndivyo unavyozidi kupata hekima hii. Kupitia vitabu unaweza kujifunza mambo mbali mbali kama vile: Njia za kukabiliana na matatizo mbalimbali. Njia za kufanya mambo mbalimbali kwa ufanisi. Jinsi ya kuboresha maisha yako. Hamasa kutoka kwa waliofanikiwa n.k. Maarifa mapya usiyoyajua. Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo unaweza kujifunza au kuyapata kutoka kwenye vitabu. Hivyo ikiwa unataka kuwa bora zaid...
Faida 5 za Kusema “Hapana”

Faida 5 za Kusema “Hapana”

Tija
Ni muhimu kukumbuka kuwa “Hapana” ni jibu rahisi pia dogo sana lakini lina nguvu kubwa. Ni vyema kufahamu nguvu iliyoko kwenye jibu la “Hapana” ili tuweze kuboresha maisha yetu. Kila siku kwenye maisha yetu tunatakiwa kufanya maamuzi fulani ya kukataa au kukubaliana na mipango au jambo fulani. Ni wazi kuwa maamuzi tunayoyafanya kuhusu mambo na mipango hii, ndiyo huamua na kuatawala hali za maisha yetu ya sasa na baadaye. Karibu nikushirikishe faida 5 za kusema hapana katika mipango na mambo mbalimbali kwenye maisha yako. 1. Hukutenga na mipango mibaya Siyo kila mpango unafaa kwenye maisha yako. Mipango mingine inaweza kuangamiza ndoto na malengo yako. Kwa mfano mtu akakushawishi uingie kwenye biashara ya dawa za kulevya, je unafikiri utaweza kweli kupata manufaa ya uh...
Makosa 25 ya Kuepuka Unapotengeneza Tovuti (website) au Blog

Makosa 25 ya Kuepuka Unapotengeneza Tovuti (website) au Blog

Tovuti na Blogu
Kuna tovuti na blog nyingi zinazotengenezwa kila siku, lakini siyo zote zinakidhi viwango vya ubora. Hili linasababishwa na tovuti nyingi kutengenezwa bila kuzingatia kanuni muhimu za utengenezaji wa tovuti au blog. Zipo athari nyingi za kutengeneza tovuti zenye ubora mdogo kama vile kupoteza wasomaji au watembeleaji pamoja na kupata nafasi ndogo kwenye injini pekuzi. Ni muhimu ukafahamu kuwa  tovuti (website) au blog ni sura yako au ya biashara yako kwenye ulimwengu. Hivyo ikiwa hutozingatia utengenezaji bora wa tovuti au blog yako, basi utaharibu picha yako au ya biashara yako. Ikiwa unataka kutengeneza tovuti (website) au blog bora, basi fahamu makosa 25 yakuepuka wakati wa kutengeneza tovuti au blog. 1. Muundo mbaya wa tovuti au blog Kosa la muundo mbaya wa tovuti hufany...
Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa

Tabia 10 Unazotakiwa Kijifunza Kutoka kwa Watu Waliofanikiwa

Maendeleo Binafsi
Ikiwa wewe ni mjasiriamali unayeanza au umeajiriwa sehemu fulani, kuna tabia ambazo unatakiwa kuzifahamu na kuzifanya ili uwe na mafanikio. Watu wengi hufikiri kuwa mafanikio ni jambo linalotokea kwa bahati tu; lakini mafanikio ni matokeo ya tabia au mikakati inayofanywa mara kwa mara. Hivi leo kuna watu tunaowachukulia kuwa wamefanikiwa; watu hawa wana tabia fulani za msingi zinazofanana. Karibu nikufahamishe tabia 10 za watu waliofanikiwa ambazo unaweza kujifunza ili uweze kufanikiwa. 1. Wana mipango Watu waliofanikiwa hawafanyi kazi bila mipango madhubuti. Watu hawa hupanga mipango mbalimbali wanayotakiwa kuitekeleza; mwishoni hukagua kama mipango yao wameitekeleza jinsi ipasavyo. Ni muhimu kujifunza tabia hii ya kujiwekea mipango na kufanya mambo kulingana na mipango husika bi...
Nukuu (Quotes) 30 za Mafanikio Zitakazokuhamasisha

Nukuu (Quotes) 30 za Mafanikio Zitakazokuhamasisha

Hamasa
Kila mtu ana maana yake ya mafanikio. Ni wazi kuwa mafanikio ni kuweza kukabiliana na changamoto au kushindwa bila kukata tamaa au kuacha. Mara nyingi huwa napenda kusoma nukuu (Quotes) mbalimbali kwani huwa zinanipa hamasa kubwa ya kuzidi kufanyia kazi ndoto zangu. Naamini hata wewe unaweza kuhamasika na kupata ari zaidi kwa kusoma nukuu hizi 30 za mafanikio. Soma pia: Nukuu (Quotes) 50 Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako. Naamini umehamasika na kupata shauku zaidi ya kufanyia kazi malengo na ndoto zako ili ufanikiwe. Kila kitu kinaanza kwenye fikra zetu. Naamini umebaini wazi kuwa maana ya mafanikio ni pana; pia mafanikio siyo kutokukabiliana na cha...
Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani

Faida 10 za Kuwa na Malengo Maishani

Maendeleo Binafsi
Kabla hujakamilisha chochote maishani, ni lazima ufahamu unahitaji nini. Ni lazima ukae chini utafakari kama kile unachokifanya kina thamani kwako; ikiwa hakina thamani, basi tenga muda ujiwekee malengo yenye maana kwako. Kujiwekea malengo maishani kuna umuhimu mkubwa kwani hutufanya tujikite sawasawa kwenye kila tunachokifanya. Je uko tayari kuweka malengo? Karibu nikufahamishe faida 10 utakazozipata ikiwa utajiwekea malengo maishani mwako. 1. Hukupa mwongozo Awali ya yote, malengo hukupa mwongozo na mwelekeo maishani mwako. Malengo hukuwezesha kubaini kitu unachokilenga, na hukufanya uelekeze nguvu zako kwenye kitu husika. Badala ya kushika hiki na kile au kuwa huyu na yule, malengo yatakuwezesha kufahamu unatakiwa kufanya nini au kuwa nani. 2. Hukuwezesha kufanya...
Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu

Aina 70 za Hofu (Phobia) Unazotakiwa Kuzifahamu

Maarifa
Hofu ni hisia ambazo zinatulinda na vitisho vinavyotuzunguka. Kila mtu ana hofu, lakini viwango na aina ya hofu hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Wapo watu ambao huhofu juu ya vitu na mambo mbalimbali hadi kushindwa kuendelea na majukumu au maisha yao ya kawaida. Ikiwa unapenda kufahamu aina za hofu (phobia) ili pia uchunguze kama una aina hizo basi fuatilia makala hii nikufahamishe aina 70 za hofu. Pogonophobia – Pogonophobia ni hofu ya kuogopa ndevu au kukaa karibu na mtu mwenye ndevu. Hofu hii huwapata zaidi wanawake. Astraphobia – Hofu hii pia inajulikana kama astrapophobia, brontophobia, keraunophobia, au tonitrophobia; hii ni hofu ya kuogopa radi. Photophobia – Hii ni hofu ya kuogopa mwanga; mara nyingi husababishwa na matatizo ya kiafya ya macho. So...
Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi

Njia 10 za Kuamka Mapema Asubuhi

Tija
Kuamka mapema asubuhi kuna manufaa mengi sana. Unapoamka mapema asubuhi unaongeza ufanisi na tija katika utendaji wako wa kazi. Kumbuka pia muda wa asubuhi ndipo mtu anapokuwa na afya njema kiakili na kimwili; hivyo kuamka mapema kutakuwezesha kuutumia muda huu vyema. Pamoja na umuhimu huu wa kuamka mapema, siyo watu wengi wanaoweza kutimiza lengo lao la kuamka mapema. Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha tatizo hili kama vile matatizo ya kiafya, kisaikolojia na hata kimazingira. Ikiwa basi wewe ni mmoja wapo wa watu wanaotamani kuamka mapema, basi fahamu njia 10 za kukuwezesha kuamka mapema asububi. 1. Lala muda sahihi Muda wa kulala ni muhimu sana katika kukuwezesha kuamka mapema asubuhi. Hakikisha unalala mapema na unapata muda wa kutosha wa kulala. Kwa kawaida bina...
Application/Programu 10 Muhimu za Kuwa Nazo Kwenye Simu (2017)

Application/Programu 10 Muhimu za Kuwa Nazo Kwenye Simu (2017)

Teknolojia
Ni wazi kuwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya simu za mkononi hasa simu za kisasa (smartphone). Ni ukweli usiopingika kuwa yapo matumizi mengi ya simu za mkononi pamoja na programu zake (applications) ambayo bado hayajafahamika vyema kwa watumiaji wake. Fuatilia makala hi ufahamu programu 10 muhimu kuwa nazo kwenye simu yako ili uwe mwenye tija zaidi. 1. Google Drive Google drive ni zaidi ya hazina ya mafaili. Google Drive inakuwezesha kutengeneza ofisi yako ndogo yenye uwezo mzuri wa kuunda, kupanga, kuhariri na hata kusambaza mafaili mbalimbali kadri upendavyo. 2. Android Device Manager Ukizingatia kwamba simu ni muhimu sana kwenye maisha yetu, tunahitaji kitu cha kutusaidia ikiwa jambo litakwenda vibaya. Android Device Manager itakuwezesha kufanya mambo kama vile ...