
Fahamu Njia 6 za Kulinda Akaunti Zako za Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya kijamii ni kitu muhimu sana kwenye maisha binafsi na shughuli za kiuchumi kama vile biashara. Kutokana na umuhimu huu, kuna haja ya kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa salama. Je ulishawahi kufikiri nini kitatokea ikiwa mtu mbaya atapata nafasi ya kuingia kwenye akaunti zako? Ni wazi kuwa mambo kama haya hapa chini yanaweza kutokea: Kuiba wafuasi wako utakaokuwa umewakusanya muda mrefu.
Kutapeli watu mbalimbali wanaokufahamu katika mitandao ya kijamii kwa kutumia akaunti yako.
Kuchafua taswira yako; kumbuka mtu mbaya anaweza kuweka maudhui mabaya yatakayoshusha hadhi yako.
Kuiba ama kutumia vibaya taarifa zako binafsi zilizoko kwenye akaunti yako. Ni wazi kuwa ipo sababu ya kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa sal...










