Fahamu Hili Archives - Page 7 of 20 - Fahamu Hili
Wednesday, March 18Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Podcast: Fahamu Hili

Madaraja 15 Makubwa au Marefu Zaidi Duniani

Madaraja 15 Makubwa au Marefu Zaidi Duniani

Maarifa
Kwa siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa maendeleo makubwa katika shughuli mbalimbali za binadamu. Sekta ya ujenzi na usafiri ni moja kati ya sekta ambazo binadamu amepiga hatua kubwa. Kila siku kumekuwa kukibuniwa na kufanyika maboresho mbalimbali katika miundombinu ya usafirishaji. Kumeshuhudiwa ujenzi wa barabara za kisasa, reli, viwanja vya ndege au hata kubuniwa kwa baadhi ya aina mpya za usafiri. Kutokana na hili, yapo madaraja mbalimbali yaliyojengwa sehemu mbalimbali duniani ili kuboresha usafiri wa barabara na reli. Karibu uongeze maarifa yako kwa kufahamu madaraja 15 makubwa au marefu zaidi duniani kwa sasa. 1. Daraja la Danyang–Kunshan Daraja la Danyang–Kunshan ndilo daraja refu kuliko yote duniani, lina urefu wa kilometa 164.8. Daraja hili linapatikana huko China kat...
Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Benki

Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Kuchagua Benki

Kipato
Benki ni taasisi muhimu ambayo siyo rahisi mtu kukwepa kuitumia kwa njia moja au nyingine. Kuhifadhi au kusafirisha pesa kwa njia za zamani kumepitwa na wakati; sasa ni wakati wa kutumia mifumo salama na ya kisasa. Kwa kuwa benki ni taasisi muhimu, huna budi kuchukua hatua kadhaa ili kupata benki nzuri kwa ajili ya shughuli zako za kifedha. Ikiwa unataka kupata benki nzuri, basi fahamu mambo 10 unayopaswa kuzingatia wakati wa kuchagua benki kwa ajili ya matumizi yako. 1. Usalama wa pesa zako Kwa kawaida kila benki husimamiwa na benki kuu ya nchi ili kuhakikisha usalama wa fedha za wateja. Hata hivyo kuna baadhi ya benki huanzishwa na kuendeshwa kinyemela bila kuwa chini ya benki kuu. Ni muhimu kuhakikisha benki unayotaka kuitumia imesajiliwa na inajiendesha kwa kuzingatia sh...
Vitu 10 Vinavyoharibu Maadili ya Watoto

Vitu 10 Vinavyoharibu Maadili ya Watoto

Mahusiano na Familia
Kwa miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa kuporomoka kwa maadili ya watoto kwa kiwango kikubwa. Hili limepelekea kuibuka kwa maswali mengi juu ya ni nini hasa chanzo cha tatizo hili. Hivi leo watoto wengi hawaheshimu wazazi wala waliowazidi umri, wanatumia pombe na madawa, wanaiba, wana kiburi, wavivu, n.k. Kwa hakika vipo vitu vinavyochangia katika kuporomoka kwa maadili ya watoto. Karibu nikushirikishe vitu 10 vinavyoharibu maadili ya watoto. 1. Wazazi kuwa mfano mbaya Wazazi wa karne hii wengi wanawalaumu watoto kuwa wana maadili mabaya, lakini chanzo cha tatizo hili ni wao wenyewe. Wazazi wamekuwa wakilewa, kutukanana, kupigana au hata kufanya mambo mengine machafu kama vile uzinzi mbele ya watoto. Kwa hakika tabia hizi zinapofanywa mbele ya watoto nao huziiga na kuzifany...
Sababu 11 za Kwanini Watu Hawakupendi

Sababu 11 za Kwanini Watu Hawakupendi

Maendeleo Binafsi
Kuna baadhi ya watu wanapendwa sana kwenye jamii au mazingira yanayowazunguka, kwa ujumla tunaweza kusema wanapendwa takriban na watu wote. Lakini wapo wengine wasiopendwa kabisa, na hata kama wanapendwa, basi wanapendwa na watu wachache sana. Kuishi katika jamii inayokupenda kunakufanya kuwa mwenye furaha na ufanisi katika yale unayoyafanya. Wapo baadhi ya watu wanatambua kuwa hawapendwi, lakini hawajui sababu za tatizo hilo wala njia ya kulitatua. Ikiwa unataka kufahamu kwanini baadhi ya watu hawakupendi, basi fahamu sababu 11 zinazosababisha watu wasikupende. 1. Siyo msikivu Kama unavyopenda kusikilizwa, ndivyo na watu wengine wanavyopenda kusikilizwa. Ikiwa huna muda wa kusikiliza mawazo au matatizo ya watu wengine, nao pia hawatakuwa na muda wa kupenda kukusikiliza. Epuka tabia z...
Faida 15 za Kufunga Kula Unazotakiwa Kuzifahamu

Faida 15 za Kufunga Kula Unazotakiwa Kuzifahamu

Mtindo wa Maisha
Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu kuwa kufunga kula kuna manufaa ya kiafya pia. Kufunga kula ni tendo lenye historia ndefu sana ambayo kimsingi chimbuko lake ni sababu za kiimani. Hata hivyo shuhuda na tafiti mbalimbali zimedhihirisha kuwa kuna manufaa mengine kemkem ya kufunga kula mbali na yale ya kiimani. Ikiwa basi unapenda kuongeza maarifa pamoja na kuboresha afya yako, fahamu faida 15 za kufunga kula. 1. Huboresha metaboli Metaboli ni mchakato ambao mwili hutumia virutubisho kutoka kwenye vyakula ili kujipa nguvu. Unapofunga kwanza unapumzisha mfumo wako wa umeng’enyaji, pili unaufanya mchakato wa metaboli kwenda vizuri kwani mwili utatumia vyema virutubisho vilivyoko mwilini tayari. 2. Huboresha mzunguko w...
Njia 10 za Kuepuka Majanga ya Moto Kwenye Nyumba

Njia 10 za Kuepuka Majanga ya Moto Kwenye Nyumba

Nyumba na Makazi
Kwa siku za usoni kumekuwa na matukio mengi ya majanga ya moto. Matukio haya husababisha uharibifu mkubwa wa mali au hata kugharimu maisha ya watu. Kwa hakika kuunguliwa na nyumba au mali zako unazozipenda ni jambo baya ambalo usingependa litokee. Kutokana na mazingira na miundombinu duni ya majengo, majanga ya moto yameendelea kuwakumba watu wengi. Hata hivyo zipo njia kadhaa unazoweza kutumia kukabili majanga ya moto. Karibu ufuatilie makala hii ili nikushirikishe njia 10 za kuepuka majanga ya moto kwenye nyumba pamoja na tahadhari unazoweza kuchukua. 1. Tumia mfumo bora na salama wa umeme Majanga mengi ya moto husababishwa na hitilafu zinazotokana na mifumo duni ya umeme. Kutokana na ukosefu wa elimu au uhaba wa pesa, watu wengi hutumia vifaa duni wakati wa kuweka umeme k...
Vitu 20 Usivyotakiwa Kusema Wakati wa Usaili wa Kazi (Job Interview)

Vitu 20 Usivyotakiwa Kusema Wakati wa Usaili wa Kazi (Job Interview)

Tija
Inawezekana una maarifa stahiki pamoja na uzoefu unaohitajika kwenye kazi fulani, lakini ukakosa kazi hiyo kutokana na vitu ulivyosema au kufanya wakati wa usaili wa kazi. Ni muhimu kufahamu kuwa lengo la usahili wa kazi siyo kukufahamu wewe au kufahamu matakwa yako, bali ni kutathimini kama unafaa kwenye kazi au kampuni husika. Hivyo ni muhimu kuhakikisha yale yote unayoyasema na kuyafanya kwenye usaili, yanaonyesha kufaa kwako kwenye kazi husika. Ikiwa unatafuta kazi au umeitwa kwenye usaili wa kazi, basi fahamu vitu 20 ambavyo hutakiwi kuvisema au kuvifanya wakati wa usaili wa kazi (Job Interview). Sipendi kazi yangu ya sasa au ya awali. (Kwa hiyo utachukia na hii unayoomba?) Mwajiri wangu wa awali ni mbaya. Kwa kusema hivi utaonekana utamchukia na huyu wa sasa. ...
Njia 9 za Kutangaza Biashara Yako Bila Pesa

Njia 9 za Kutangaza Biashara Yako Bila Pesa

Biashara na Uchumi
Matangazo ni swala muhimu kwa kila biashara. Tatizo linatokea pale ambapo biashara inashindwa kumudu gharama za matangazo, hasa matangazo ya gharama kubwa. Naamini wewe kama mjasiriamali unafahamu kuwa kuna wakati bajeti ya biashara inakuwa imebana. Hivyo swala la kujitangaza linakuwa na changamoto. Fuatilia makala hii kwa karibu ili nikufahamishe njia 9 unazoweza kuzitumia kutangaza biashara yako bure au kwa gharama nafuu sana. 1. Tumia tovuti Tovuti au blog ni njia rahisi na ya gharama nafuu ya kujitangaza. Ikiwa una blog au tovuti ambayo inaidadi nzuri ya watembeleaji, unaweza kuweka tangazo la biashara yako hapo na likaonekana kwa watu wengi zaidi. 2. Tumia mitandao ya kijamii Kama ilivyo wenye njia ya blog, vivyo hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebo...
Madhara 8 ya Kunakili Machapisho kutoka Kwenye Blog au Tovuti Nyingine

Madhara 8 ya Kunakili Machapisho kutoka Kwenye Blog au Tovuti Nyingine

Tovuti na Blogu
Uandishi ni kazi ngumu na inayochosha, uandishi unahitaji kutafiti, muda, maarifa sahihi na hata rasilimali fedha. Kutokana na sababu hizi wamiliki wengi wa blog au tovuti hujikuta wakinakili maudhui kutoka kwenye blog au tovuti nyingine. Swala la kunakili maudhui kutoka kwenye blog au tovuti nyingine limekuwa likisababishwa pia na kukosa lengo, uvivu, kukosa ubunifu pamoja na kutokujua madhara ya kunakili. Ikiwa wewe ni blogger au mmiliki wa tovuti, basi karibu nikushirikishe madhara 8 yatokanayo na kunakili machapisho (post) kutoka kwenye blog au tovuti nyingine. 1. Hukufanya uonekane duni Unaponakili machapisho kutoka kwenye tovuti au blog nyingine, moja kwa moja unawaambia wasomaji wako kuwa huna cha kuwaambia kama usipomnakili mtu mwingine. Hivyo wasomaji wako watak...
Mambo 10 ya Kuepuka Unapokuwa Kwenye Nchi ya Kigeni

Mambo 10 ya Kuepuka Unapokuwa Kwenye Nchi ya Kigeni

Usafiri na Safari
Kila mahali pana taratibu na mambo yake. Mtindo wa maisha ulioouzoea kwenye nchi yako ya nyumbani, unaweza usikubalike kwenye nchi ya kigeni. Inawezekana umepanga kutembelea nchi ya kigeni hivi karibuni, au tayari uko kwenye nchi ya kigeni. Karibu nikufahamishe mambo 10 ambayo kama utayaepuka utaweza kukaa kwenye nchi ya kigeni bila tatizo. 1. Kukiuka utamaduni wa nchi husika Kila nchi ina tamaduni na taratibu zake. Kuna nchi haziruhusu kuvaa mavazi fulani au kufanya matendo fulani. Ni vyema ukahakikisha mambo unayoyafanya hayakiuki tamaduni za nchi husika. Kwa mfano nchi nyingi za Kiarabu haziruhusu kubusu au kukumbatiana hadharani baina ya mwanamke na mwanaume. Ukikamatwa ukifanya kosa hili, unaweza kuchukuliwa hatua kali. Soma pia: Maeneo 10 Ambayo ni Marufuku Kubusu au K...