Mtindo wa Maisha Archives - Page 2 of 2 - Fahamu Hili
Tuesday, July 16Maarifa Bila Kikomo

Mtindo wa Maisha

Faida 10 za Kupumzika

Faida 10 za Kupumzika

Mtindo wa Maisha
Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, watu wengi hawapati muda wa kutosha wa kupumzika. Mara nyingi mtu anapozidiwa hupunguza zaidi muda wa kupumzika ili akamilishe majukumu yake. Ni wazi kuwa watu wengi hawafahamu umuhimu wa kupumzika, ndiyo maana hawatengi muda wa kutosha wa kupumzika. Ni ukweli usiopingika kuwa kupumzika kuna manufaa makubwa sana kwenye miili na utendaji wetu wa kazi kila siku. Ikiwa unataka kuboresha utendaji wako wa kazi pamoja na afya yako, fahamu faida 10 za kupumzika. 1. Huongeza uwezo wa kumbukumbu Ubongo wa mwanadamu unahitaji kupumzika ili uweze kujijenga na kufanya kazi vyema. Ikiwa mtu hatapata muda wa kutosha wa kupumzika, uwezo wake wa kutunza kumbukumbu utapungua. Pia utafiti uliofanyika umebaini kuwa kutokupumzika huongeza kiasi fulani...
Faida 11 za Push Up Kiafya Unazotakiwa Kuzijua

Faida 11 za Push Up Kiafya Unazotakiwa Kuzijua

Mtindo wa Maisha
Mazoezi ni njia moja wapo ya kutufanya tuwe vizuri na wenye afya njema. Kama unahitaji zoezi ambalo litanufaisha sehemu mbalimbali za mwili wako, push ups ni zoezi moja wapo. Push up ni zoezi ambalo linaweza kufanywa na wanaume na wanawake bila gharama yoyote; na faida zake ni zaidi ya kunyoosha tu misuli. Naamini unapenda afya njema pamoja na maarifa; fuatilia makala hii nikufahamishe faida 11 za zoezi la push up kiafya ikiwa utalifanya mara kwa mara. 1. Huboresha mkao na mwonekano wako Push up ni njia bora ya kuufanya mgongo wako unyooke. Push up huimarisha na kuweka sehemu mbalimbali za mwili wako kukaa jinsi ipasavyo; kwa njiaa hii huufanya mwili wako uwe na mwonekano mzuri. 2. Huimarisha misuli Unapopiga push up unahusisha misuli mbalimbali kwenye mwili wako; misuli hii ni ...
Njia 12 za Uhakika za Kuacha Pombe

Njia 12 za Uhakika za Kuacha Pombe

Mtindo wa Maisha
Pombe ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi pasipo hata kufahamu athari zake. Pombe ina athari mbalimbali kiafya na kisaikolojia. Wengi baada ya kuathiriwa na pombe hutamani kuacha matumizi ya pombe lakini ni wachache tu ndiyo hufanikiwa katika hili. Ikiwa unataka kuacha au kumsaidia mtu mwingine kuacha pombe, basi fuatilia njia 12 za uhakika za kuacha pombe. 1. Epuka watu watakaokushawishi kunywa pombe Mara nyingi kama wewe unapenda kunywa pombe utakuwa na marafiki wanaokunywa pombe pia. Ni wazi kuwa marafiki wanaokunywa pombe watakuhimiza kunywa hata kwa kukununulia au hata pengine kukukebehi na kukubeza juu ya uamuzi wako wa kuacha pombe. Hivyo ikiwa unataka kuacha kunywa pombe ni lazima uepuke marafiki au watu wanaoweza kukushawishi kunywa pombe. Unaweza kutafuta ma...
Aina 9 za Vyakula  Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona

Aina 9 za Vyakula Vitakavyoboresha Uwezo Wako wa Kuona

Mtindo wa Maisha
Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti. Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona. 1.Samaki Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3. 2.Mboga za majani Watu ...
Misamiati 20 ya Kiswahili Unayoitumia Kimakosa

Misamiati 20 ya Kiswahili Unayoitumia Kimakosa

Mtindo wa Maisha
Ni wazi kuwa watu wengi wamekuwa wakijitahidi kutumia lugha za kigeni kwa usahihi kuliko Kiswahili. Ni rahisi mtu kuona aibu kufanya makosa katika lugha kama vile Kiingereza na Kifaransa lakini siyo Kiswahili. Ni dhahiri kuwa yapo makosa mengi yanayofanywa na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutokana na kutotilia maanani swala la umahiri katika lugha. Makosa haya yasipotiliwa maanani yanaweza kukufanya uonekane duni katika uwezo wako wa kutumia lugha. Yapo makosa mbalimbali ambayo hufanywa na watumiaji wa lugha yakiwemo yale ya kimsamiati, kimatamshi, kimuundo n.k. Katika makala hii nitaonyesha misamiati takriban 20 ambayo pengine unaitumia au inatumiwa vibaya na wazungumzaji wa lugha hasa kutokana na makosa ya kimsamiati. 1. Lisaa na Masaa Lisaa na Masaa ni misamiati au...
Faida 9 za Kusikiliza Mziki

Faida 9 za Kusikiliza Mziki

Mtindo wa Maisha
Kama unapenda kusikiliza mziki basi uko kwenye kundi zuri. Watu mbalimbali maarufu wamewahi kutoa maoni yao kuhusu mziki kama vile mwanabayolojia Charles Darwin aliyesema kuwa angepewa nafasi ya kushi tena angetengeneza kanuni ya kusoma mashairi na kusikiliza mziki angalau mara moja kwa wiki. Kwa upande mwingine Albert Einstein alikiri kuwa asingekuwa mwanafizikia basi angekuwa mwanamziki. Tafiti zinabainisha kuwa kusikiliza mziki kuna manufaa mengi kwa ajili ya afya ya mwili na akili. Tafadhali fuatana nami katika makala hii ili nikujuze faida 9 za kusikiliza mziki. 1. Mziki hutufanya tuwe na furaha William James alsisema “Siimbi kwa sababu ninafuraha, bali nafurahi kwa kuwa ninaimba” . Kusikiliza mziki huzalisha kemikali ya dopamane ambayo hutufanya tujisikie vizuri. Hii ndiy
Faida 7 za Kula Mayai Wakati wa Kifungua Kinywa

Faida 7 za Kula Mayai Wakati wa Kifungua Kinywa

Mtindo wa Maisha
Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai. Fuatana nami katika makala hii ili nikueleze faida 7 za kula mayai wakati wa kifungua kinywa. 1. Hutunza shibe Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano. 2. Husaidia kupunguza uzito Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilingani...
Njia 13 za Kupata Usingizi Mzuri/Kulala Vizuri

Njia 13 za Kupata Usingizi Mzuri/Kulala Vizuri

Mtindo wa Maisha
Usingizi wa uhakika ni jambo jema sana kwa ajili ya afya ya mwili wako. Lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, pamoja na kujengeka kwa jamii yenye mfumo wa maisha wenye shughuli nyingi, watu wengi hawapati usingizi mzuri. Namkumbuka rafiki yangu mmoja alipata kazi nyingi sana kwenye mtandao. Hivyo ikamlazimu azifanye zote kwa muda mfupi bila kulala wala kula ipasavyo. Matokeo yake ameugua kwa miezi minne sasa na bado afya yake haijaimarika kama awali. Hili linatupa umuhimu wa kuchunguza ni nini hasa manufaa ya kulala au usingizi mzuri? Huimarisha na kuboresha ukuaji wa mwili. Hujenga na kuimarisha kinga mwili. Hukuweka katika hali nzuri (mood). Hukuongezea kumbukumbu. Hurefusha maisha. Huboresha tendo la ndoa. Huondoa msongo wa mawazo. Ha...
Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Faida 10 za Kunywa Maziwa Usizozifahamu

Mtindo wa Maisha
Maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya yako. Wataalamu wa afya na wauzaji wa maziwa wamekuwa wakieleza faida kadha wa kadha za kunywa maziwa. Je umewahi kujiuliza hasa ni faida gani hizo zitokanazo na unywaji wa maziwa? Ni wakati wako sasa wa kujiuliza kwa kina juu ya faida zitokanazo na unywaji wa maziwa. Fuatana nami katika makala hii nikueleze faida 10 zitokanazo na unywaji wa maziwa. 1. Hujenga na kulainisha ngozi Je unamfahamu Cleopatra? Cleopatra alikuwa ni malikia wa Misri anaesadikiwa kuwa mzuri sana. Inaaminikia uzuri wa Cleopatra ulitokana na tabia yake ya kuogea maziwa mara kwa mara. Hivyo basi, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku. 2. Hu...
Tabia 10 zitakazobadili maisha yako

Tabia 10 zitakazobadili maisha yako

Mtindo wa Maisha
Mara nyingi umekuwa ukijiuliza ufanyeje ubadili maisha yako? Je umekuwa ukitamani kuboresha maisha yako kutoka kiwango cha chini kwenda katika kiwango bora zaidi? Kama jibu ni ndiyo basi una mawazo wazuri sana. Unatakiwa kuchukua hatua kadhaa ili basi uweze kuboresha maisha yako kutoka kiwango kimoja kwenda kingine. Katika makala hii nitakujuza tabia kumi ambazo kama utajitahidi kuwa nazo hakika utayabadili maisha yako na kuyafanya kuwa bora zaidi. 1. Epuka marafiki au watu wasiofaa Wahenga walisema “ndege wanaofanana huruka pamoja”. Je kwanini ukae na watu wavivu au wazembe kama wewe huna tabia hizo au zingine zinazofanana na hizo? Jijengee tabia ya kuwaepuka marafiki au watu wasiofaa katika maisha yako kwani hawatakusaidia kufikia malengo yako bali watakudidimiza. Tafuta watu