
Namna ya Kuwa Mzungumzaji Hamasa (Motivational Speaker)
Ninapotaja wazungumzaji hamasa (Motivational Speakers) naamini unafahamu kuwa ni watu wanaowasaidia watu kuendeleza na kuwezesha maono au utoto wao wa ndani ili watu husika waweze kufanikiwa. Mzungumzaji hamasa anaweza kuzungumzia mada yoyote ile kulingana na uzoefu wake. Wengi hutamani kuwa wazungumzaji hamasa lakini wameshindwa kujua waanzie wapi. Jambo la msingi katika uzungumzaji hamasa ni shauku yako ya ndani katika mada unayotaka kuizungumzia. Kuwa mzungumzaji hamasa kunahitaji kubaini mada na walengwa wa mada yako bila kusahau kunoa uwezo wako wa kuzungumza mbele ya watu pamoja na kuielewa vyema mada husika. Kama unatamani kuwa mzungumzaji hamasa, fuatilia hoja jadiliwa hapa chini kwa makini ili sasa uweze kuwa mzungumzaji hamasa.
1. Bainisha mada utakayozungumzia
Huwezi ku...