
Vitu 11 Unavyotakiwa Kutoviweka Kwenye Mitandao ya Kijamii
Kuna taarifa nyingi tunazoweka kwenye mtandao; lakini je, sasa ni wakati wa kuweka mipaka juu ya ni lipi la kuweka na kutoweka kwenye mitandao? Ndiyo; huu ni wakati sahihi. Hivyo basi, tambua vitu 11 ambavyo haupaswi kuviweka kwenye mitandao ya kijamii.
1. Tarehe kamili ya kuzaliwa
Wakati mwingine unaweza kuvutiwa na namna marafiki zako wanavyoweka taarifa za kuzaliwa kwenye mtandao, au hata misisitizo ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook juu ya kukamilisha akaunti yako kwa kuweka tarehe ya kuzaliwa. Kuweka tarehe halisi au kamili ya kuzaliwa kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kutoa mwanya kwa wahalifu kupata taarifa zako muhimu na hata kufungua au kuingilia akaunti zako zinazotumia tarehe yako ya kuzaliwa. Mambo ya kufanya: Ficha au ondoa tarehe yako halisi ya kuzal...