
Njia 13 za Kupata Usingizi Mzuri/Kulala Vizuri
Usingizi wa uhakika ni jambo jema sana kwa ajili ya afya ya mwili wako. Lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, pamoja na kujengeka kwa jamii yenye mfumo wa maisha wenye shughuli nyingi, watu wengi hawapati usingizi mzuri. Namkumbuka rafiki yangu mmoja alipata kazi nyingi sana kwenye mtandao. Hivyo ikamlazimu azifanye zote kwa muda mfupi bila kulala wala kula ipasavyo. Matokeo yake ameugua kwa miezi minne sasa na bado afya yake haijaimarika kama awali. Hili linatupa umuhimu wa kuchunguza ni nini hasa manufaa ya kulala au usingizi mzuri? Huimarisha na kuboresha ukuaji wa mwili.
Hujenga na kuimarisha kinga mwili.
Hukuweka katika hali nzuri (mood).
Hukuongezea kumbukumbu.
Hurefusha maisha.
Huboresha tendo la ndoa.
Huondoa msongo wa mawazo. Ha...