Eston J., Author at Fahamu Hili - Page 4 of 4
Saturday, August 30Maarifa Bila Kikomo
Shadow

Author: Eston J.

Eston ni mtafiti na mwandishi wa makala mbalimbali zinazohusu tija, maendeleo binafsi pamoja na afya bora. Analenga kuwahamasisha wengine pamoja na kuubadili ulimwengu kwa kupitia maarifa stahiki.
Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Mafuta ya Nazi Hatari kwa Afya

Afya
Watafiti wa afya nchini Marekani wamesema matumizi ya mafuta ya nazi si salama kwa afya kama ilivyo kwa nyama ya ng’ombe na siagi. Shirika la Moyo la Marekani (AHA), limeeleza kuwa mafuta yaliyoko kwenye nazi yanaweza kuongeza lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa AHA, wanadai kuwa kuna mafuta 82% katika nazi. Kuna zaidi ya 63% kwenye siagi, 50% kwenye nyama ya ng’ombe na 39% kwenye nyama ya nguruwe. Wataalamu hao wameongeza kuwa mafuta hayo yanaweza kusababisha lehemu (cholesterol) mbaya katika mwili wa binadamu. Baadhi ya watu hudai kuwa ulaji wa mafuta ya nazi una manufaa kwa afya ya mlaji lakini AHA wamesema madai hayo hayajadhibitishwa. Wamependekeza kuwa, watu wajitahidi kupunguza kiasi cha mafuta yenye lehemu wanayoyatumia kila siku katik...