
Mambo 5 Yanayosababisha Biashara za Wanawake Kufa
Hivi leo wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahi na kufanyia kazi fursa mbalimbali. Fursa hizo ni pamoja na uwekezaji katika biashara ndogo na za kati. Ni dhahiri kuwa mama ndiye nayeumia zaidi pale familia inapokuwa na uchumi mbaya. Mama hapendi kuona watoto wanakosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu, matibabu n.k. Hivyo suala la kuboresha kipato cha familia limewafanya wanawake wengi kutafuta njia mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo njia ya kufanya biashara. Hata hivyo pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na wanawake, bado biashara zao ngingi hufa kutokana na sababu kadha wa kadha. Fuatana nami katika makala hii ufahamu mambo matano yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa.
1. Kukosa maarifa na elimu ya biashara
Kitu chochote au kazi y...