
Mambo 25 Yakushangaza Kuhusu Mwili wa Binadamu
Inawezekana unatazama mwili wako kwa juu juu pekee bila kufahamu mambo mengi yaliyojificha kwenye mwili wako. Ni hakika kuwa mwili umeumbwa kwa namna ya pekee sana inayouwezesha kufanya kazi pamoja na kuonekana jinsi ulivyo. Naamini unapenda kupata maarifa kwa kuufahamu mwili wako vyema. Karibu ufuatilie makala hii ili nikujuze mambo 25 yakukushangaza kuhusu mwili wa binadamu.
1. Ubongo unatumia asilimia 20 ya oksijeni pamoja na kalori
Ni wazi kuwa utendaji kazi wa ubongo unahitaji oksijeni asilimia 20 pamoja na kalori kutoka kwenye mwili ili kufanya kazi jinsi ipasavyo.
2. Kila mtu ana harufu yake
Mbali na mapacha wa kufanana, kila mtu ana harufu yake ya pekee inayomtofautisha kati yake na mtu mwingine.
3. Uwezo mkubwa wa kufikiri unahusiana na kiasi cha ndoto mtu anazoota
In...