
Mambo 15 ya Kushangaza Kuhusu Afrika
Vita, njaa, vifo, maradhi - ni vitu ambavyo wengi wamevisikia na kuvifahamu kuhusu Afrika. Lakini sasa ni wakati wa kubadili mtazamo huu. Afrika ni bara la kushangaza ambalo ni tofauti kabisa na mabara mengine saba. Afrika ina utajiri katika urithi wa utamaduni wa kipekee, utajiri wa rasilimali za asili pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii. Nakukaribisha ufuatilie makala hii ili uweze kufahamu mambo 15 ya kushangaza na kusisimua kuhusu Afrika. Mlima Kilimanjaro unapatikana barani Afrika. Mlima huu una urefu wa takriban meta 5,895 kutoka usawa wa bahari. Mlima huu unapatikana kaskazini mwa Tanzania.
Zaidi la asilimia 25 ya lugha huzungumzwa Afrika. Inaaminika kuwa kuna takriban lugha 2000 zinazozungumzwa barani Afrika. Lugha zote hizi zinatambuliwa na umoja wa Afrika. Nigeri...